isajorsergio
Platinum Member
- Apr 22, 2018
- 4,125
- 6,253
Habari 👋🏾
Kumekuwa na hali ya watu wengi kupuuza na kutokuchukua tahadhari ya ugonjwa wa UVIKO na wengine wakienda mbali kudai hakuna ugonjwa kama huo. Napenda kuwaambia COVID-19 deadly Delta yupo Tanzania na kila mahali, nimepatwa na ugonjwa ilhali nipo eneo lilotengwa na pembezoni katika nchi.
Toka juzi jioni najihisi vibaya, napumua kwa shida, nimebwana kifua, mafua na kikohozi. Uwezo wa kusikia na kuona umepungua sana, nahisi maumivu katika mifupa na maungio ya mwili. Homa na koo kukabwa, kuwashwa, kuhisi damu ya baridi, jaws (tezi) kuwa na maumivu makali na ngozi kuakisi rangi ya bluu na kizunguzungu ni hali ninazopambana nazo.
Namna nahisi afya yangu kwa sasa, niseme nisengelikuwa mtu wa mazoezi parapanda ingekwisha imbwa. Sio kwamba sikuchukua tahadhari lah! Nimekuwa nikizingatia taratibu zote toka mlipuko huu kutokea Wuhan lakini nimekwamishwa na jamii ya watu walionizunguka.
Nimeorodhesha dalili na hali kuweza kusaidia mamlaka na watu kufahamu hali ilivyo. Hali ikiendelea hivi itatuchukua miaka 10 kupambana na COVID-19 ikiwa tumezungukwa na watu wenye mentality za hovyo na wasiojali wala kuchukua tahadhari.
Sergio 🐰