Naombeni data kwa aliyepimwa na mlinzi akakutwa na korona

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,260
10,288
Tangu ugonjwa wa korona uingie kuna maeneo mbalimbali kabla ya kuingia unapimwa na mlinzi kama hauna dalili za korona kwa kuangaliwa joto la mwili.

nauliza haya maeneo kama bank maofisini shopping mall viwanja vya ndege, hivi kuna aliyegundulika na korona kwa kutumia kipimo hiki cha walinzi?
 
Kipindi ndo corona iko hot Apr.2020 siku naenda likizo nikawa natafakari namna ya kuepuka kuwapelekea ugonjwa nyumbani kwetu

Basi kufika Dar nikaamua kutulia kama siku 4 hivi kujisikilizia halafu siku ya kuchomoka nikawa nimejipeleka na kujipitisha sehemu kadhaa wanazotumia hako kakipimo eti kutoka hapo nikaenda nyumbani comfortably...

Cha ajabu sasa kufika home... huwezi amini watu walikuwa wananinyanyapaa balaa niliumia sana aisee. Yaani nilikuta watu wanaoshuka kwenye basi zinazotoka A.Town na Dar hatuna rafiki tunatengwa halafu wahuni mtaani ni kama wanaambizana vile yaani ukitua tu ushajulikana

Nilishawahi kujiuliza hivi kale kakipimo ni tofauti na kipimo cha corona kile kilichokuwa kinalipiwa lakimoja? Halafu ni kweli kabisa hata mimi katika hayo maeneo niliyojipitisha nikapimwa kulikuwa na watu wengi sana lakini sijaona hata mmoja akizuiwa apelekwe karantini!

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Kuna siku asubuhi niliwahi na bodaboda bank kufika mlangoni mlinzi akanipima akakuta -5, akaniuliza umemeza barafu? Nimamwambia hapana nilikuwa nakula koni pale kwenye kiosk ajasema ngoja dakika kumi iyeyuke alivyorudia joto likawa sawa
 
Tangu ugonjwa wa korona uingie kuna maeneo mbalimbali kabla ya kuingia unapimwa na mlinzi kama hauna dalili za korona kwa kuangaliwa joto la mwili.

nauliza haya maeneo kama bank maofisini shopping mall viwanja vya ndege, hivi kuna aliyegundulika na korona kwa kutumia kipimo hiki cha walinzi?
Una maswali magumu sana

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Tangu ugonjwa wa korona uingie kuna maeneo mbalimbali kabla ya kuingia unapimwa na mlinzi kama hauna dalili za korona kwa kuangaliwa joto la mwili.

nauliza haya maeneo kama bank maofisini shopping mall viwanja vya ndege, hivi kuna aliyegundulika na korona kwa kutumia kipimo hiki cha walinzi?
Swali fikirishi
 
Back
Top Bottom