Namna ya Kupata Virtual Credit Cards & Debit Cards

HabariTech

Member
Sep 1, 2019
8
21
Umeshawahi kusikia maneno credit cards na debit cards? Inawezekana umekutana nayo katika mitandao ya kijamii, umesikia rafiki/ndugu wakiyatamka au kuyasikia kwenye movie, hasa movie za Marekani. Kama umewahi kusikia, huenda unafahamu kwamba huwa zinatumika kufanya malipo mtandaoni. Wazungu wanaitwa cashless payments.

Kama hufahamu kwa undani credit cards ni nini unaweza kusoma hii makala inayoongelea credit cards na bank accounts kwa undani, ili tusikuache nyuma.


Kwa ufupi credit card ni card ambayo inakuwezesha kufanya malipo mtandaoni, bila kutumia pesa zinazokuwepo kwenye account yako kuu ya pesa. Endelea kusoma zaidi hapa

Credit Cards & Debit Cards Zinatumika Wapi​

Tunaishi Tanzania, hivyo hatuwezi kushangaa sana kama asilimia 70% ya Watanzania hawafahamu credit card ni nini na wapi inatumika. Mimi mwenyewe sikuwa nazielewa vizuri mpaka kufikia mwaka 2019. Nilikuwa na tabia ya kuagiza vitu kutoka Kikuu.

Ilikuwa ni soko langu pendwa la mtandaoni mpaka pale walipokuja kunipoteza mzigo wangu ambao ilkuwa zawadi ya mtu kwa ajili ya Valentine day.

Hivyo nikaanza kutumia AliExpress na eBay. Huku nilikutana na kipingamizi cha kutumia Credit Card au Debit Card ili kufanya malipo. Sikuwa nafahamu hizi ni nini na hata namna ya kuzipata. Kila nilipojaribu kutumia namba za card yangu ya CRDB ziligoma.

Ilinibidi niende benki ili card yangu ipewe ruhusa ya kufanya malipo mtandaoni. Hii card iliniwezesha kufanya malipo baadhi ya sehemu za chakula walizopokea cards, kulipia huduma za mtandaoni kama spotify na mara nyingine niliitumia hata super market kufanya malipo.

Credit Cards zina sehemu nyingi sana zinaweza kutumika ukiacha hizo nilizotaja hapo juu. Mfano sasa hivi kuna watanzania kama Charles Venny, Baraka Mafole na Ally Msangi ambao wanauza eBooks zao mtandaoni. eBooks zao wanauza kupitia mtandao wa gumroad. Charles Venny na Ally Msangi

Hizi ni eBooks ambazo unaweza kununua kwa kutumia Credit Cards pekee. Hivyo kama huna credit utakosa maarifa yaliyomo ndani ya hizi eBooks.

Usalama wa Credit Cards & Debit Cards​

Nilikwambia kwamba credit yangu ilikuwa inawasiliana moja kwa moja na akaunti yangu ya benki. Hivyo kila nilipokuwa nikifanya muamala ilikata pesa ndani ya akaunti yangu. Bahati mbaya kuna wakati kulikuwa na huduma ambazo zilikuwa zikijilipa automatically kila mwezi bila mimi kujua.

Mwanzo nilidhani naibiwa kwa kuwa nakuta miamala ambayo mimi sikuruhusu. Shida nyingine ilikuwa kuna uwezekano wa credit card kudukuliwa na wataalamu wa mitandao.

Hivyo kilichobaki ni kutafuta njia salama ya kuwa kutumia credit cards. Mimi ni mtumiaji wa Vodacom tangu naanza kutumia simu. Sababu kubwa ni uwezo mkubwa wa internet yao na huduma isiyo na wasiwasi.

Katika kufatilia niligundua kwamba Vodacom kipindi kile walikuwa wanatoa Master Debit Cards. Ni card ambayo inadumu kwa muda wa mwaka mmoja na ni rahisi kuitengeneza kwa kuwa inahitaji uwe na M-Pesa tu. Baadae Airtel pia walikuja na hii huduma.

Hii ni njia ambayo iko salama na rahisi kutumia, kwa sababu pesa hazitoki moja kwa moja kwenye akaunti yangu ya benki. Ili kutumia pesa za card hii ilikuwa lazima niweke pesa kwenye card ndipo nifanye miamala. Kwa maana hiyo hata pesa zangu zilizopo M-Pesa zilikuwa salama, na hata ile miamala ya kila mwezi isingewezekana kama hakuna pesa kwenye hii card.

Tangu hapo nikaona ni vyema nitumie hii M-Pesa Master Card ambayo sasa hivi imekuwa M-Pesa Visa Card. Na sijawahi hangaika tena katika suala la kufanya malipo mtandaoni.

Unazipataje Hizi Virtual Credit/Debit Cards?​

Kila mtandao wenye hii huduma una namna yake ya kupata hii huduma na viwango vyake vya makato. Mfano M-Pesa Visa Card wanakata 4% kama tozo ya kila muamala unaofanya kupitia card yao. Kupata hizi cards fuata maelekezo haya.

Watumiaji wa Vodacom M-Pesa​

Watumiaji wa Vodacom M-Pesa wako wa aina mbili. Kuna wanaotumia USSD Menu na wale wanaotumia M-Pesa app.

Vodacom USSD Menu​

  • Piga 150*00
  • Chagua namba 4 “Lipa kwa Simu”
  • Chagua namba 6 “M-Pesa VISA Card”
  • Chagua namba 1 “Create Card”
Baada ya hapo utatumia ujumbe wenye taarifa za card yako. Ujumbe ambao utakuwa na Card number, Expiry date na CVV code. Hizi ndizo taarifa utazitumia wakati unafanya malipo kwa njia ya card. Ikitokea umesahau hizi taarifa unaweza kufata hizo hatua baada ya hatua ya nne utachagua namba 5 “My card”.

Baada ya hapo itabidi uweke pesa kwenye card yako ili uweze kufanya malipo mtandaoni. Ili kuweka pesa kwenye card yako fuata hatua hizi.

  • Piga 150*00
  • Chagua namba 4 “Lipa kwa Simu”
  • Chagua namba 6 “M-Pesa VISA Card”
  • Chagua namba 3 “Prefund Card”
Kisha jaza kiasia unachotoa kwenye M-Pesa kuingia kwenye card.

Vodacom M-Pesa App​

Ndani ya Mpesa App fuata hatua hizi.

  • Nenda kwenye Services
  • Chagua M-Pesa Visa Card
  • Create Card
  • Kisha Jaza pesa kwenye card yako mpya kwa kuchagua “Add Money”
  • Taarifa za card unaweza kuziona kwa kugusa button iliyopo juu kwenye ile picha ya card.

Watumiaji wa Airtel​

Kwa watumiaji wa Airtel fuata maelekezo haya

  • Piga Airtel Money USSD: *150*60#.
  • Chagua #6. Financial services.
  • Chagua #1 Airtel Money Mastercard.
  • Chagua #1. Create Airtel Money Mastercard.
  • Weka PIN kwa ajili ya Airtel Money Mastercard (Hii PIN itatumika kuruhusu malipo mtandaoni)
  • Utapokea ujumbe wenye link ya taarifa za Mastercard yako ya Airtel Money.

Jaribu Kufanya Malipo​

Kufikia hapo unaweza jaribu kutumia card yako kufanya malipo mtandaoni kwa kununua vitu mbali mbali kama hizi eBook za wataalamu. Unaweza kuchagua yoyote unayoona ni rafiki kwako au inafaa kusomwa ili kuongeza maarifa. Charles Venny na Ally Msangi
 
Mpesa wana makato makubwa mno nimeshanunua almost mara, mbili ali express muhamala wa 400k wanakata inagine 20k
 
Back
Top Bottom