jerryempire
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 5,442
- 9,317
umechelewa sana mkuuWakuu,
Binafsi huwa na Bet sana na bahati nzuri nimemuotea muhindi kama M 40
Na sasa nataka kubet kwenye kilimo
Mwaka huu naingia shambani kweli kweli sio utani, naingia FRONT na sio simu
Nakwenda kulima ekari 50 za alizeti MBUGANI kisha nikitoa naweka dengu
Eneo SINGIDA kwetu kabisa
Matumizi (makadirio ya juu kabisa) kwa ekari 50
Kukodi shamba m 2.5
Kulima shamba m 2.5
Kupanda m 1
Kupalilia shamba m 2.5
Mbegu lk 7
Uvunaji/upakiaji m 2
Mengineyo m 2
Jumla milion 13.2
Jumlisha hidden cost jumla iwe milioni 15
MAVUNO (makadirio ya chini)
Eka moja gunia 7 badala ya 15 za wataalamu
Ekari50 x Gunia 7
Jumla inakua gunia 350
Wastani gunia moja hutoa mafuta dumu 2 bei makadirio ya chini sh elf 50 kwa dumu( dumu linakwenda hadi laki+)
350 x 2 inakua dumu 700
Dumu700 x elf50 unapata Sh M35
Hapo nime assume mashudu yamelipia gharama ya ukanuaji
JUMUISHO
M35 -M15 = M20 Faida
DENGU
Ukitoa tu alizeti unavizia nvua za mwishoni kabisa unalima dengu shamba hilo hilo hulipi gharama za kukodi tena
Kulima m 2.5
Mbegu m 2
Kupanda lk 5
Madawa (emergency) m2
Kuvuna/kupakia 2m
Mengineyo m 1
Jumla m 10
Hidden cost m 2
Jumla m 12
MAUZO
Wastani gunia 4 kwa eka badala ya gunia 8 hadi 10 kwa eka za wataalamu
Ekari50 x Gunia 4 unapata gunia 200
Gunia la dengu lina wastani wa sh Laki 1
Laki 1 x gunia 200 unapata M 20
JUMUISHO
M20 - M12 = M8 Faida
FAIDA KUU (alizeti na dengu)
M20 +M8 = M28
NB
Nimeweka makadirio ya juu sana kwenye matumizi
Na nikaweka makadirio ya chini sana kwenye mavuno na bei
Dua zenu jamani
Ntaleta MREJESHO iwe nime Lost au nime Win
MREJESHO 24/03/2022
Wakuu kwema
So far mkeka wangu wa kilimo cha Alizeti unakwenda vizuri sana baada ya zile ODDS kubwa na ngumu kutick
ODDS ngumu kabisa zilikua ni MVUA na PALIZI
SHAMBA EKARI 20
Mpaka sasa nimelima ekari 20 tu...... hii ni baada ya wadau mbali mbali kushauri ekari 50 is too risk ikiwa huna UZOEFU na ikizingatiwa mamlaka ya hali ya hewa ilitabiri mvua zitakua chache
MBEGU (ASA)
Baada ya mchakato wa kitaalamu nikashauriwa nitumie mbegu za Serikali ASA na nilinunua mfuko wa kilo 2 kwa sh 5,000 tu, nilipata mchongo huu kwakuwa nilinunua kwa wingi
Sijatumia MBOLEA yoyote wala sijatumia viatilifu vyovyote kwasababu nimelima MBUGANI aridhi imeshiba na Alizeti haishambuliwi sana na magonjwa
Leo hii nimemalizana na PALIZI na mimea inakwenda vizuri kwa sehemu kubwa
Mpaka sasa SIJAKUTANA na gharama yoyote ambayo imenishtua kwa maana ya kwamba labda ni gharama ambayo sikuifikiria au gharama kuwa kubwa zaidi ya nilivyo KADIRIA
Zaidi mbegu imenipa UNAFUU mkubwa sana, nilipanga kutumia Hysuan Kg 2 kwa 35,000
Lakini nimetumia ASA Kg 2 kwa sha 5,000 na nilinunua mifuko ya Kg2 mifuko 80, yaani eka moja kwa mifuko 4, hapo nime save karibu 2m...... Naishukuru sana serikali kwa hili
Ingawaje sijajua ubora wake baada ya mavuno
Ntaleta tena Mrejesho baada ya KUVUNA
MREJESHO WA GHARAMA
Shamba ekari 20
20 x 30,00 = 600,00
Shamba lilikua safii
Kulima
20 x 40,000 = 800,000
Mbegu (ASA)
80 x 5,000 = 400,000
Kupanda
20 x 30,000 = 600,000
Palizi
20 x 50,000 = 1,000,000
Mengineyo
1,000,000
Jumla kuu 4,500,000
Hadi sasa nimelaza shambani 4.5M
Bado gharama za kuvuna kupepeta na kuhifadhi
MREJESHO
kuna kama eka nne na nusu nililima mwishoni naona zimepelea mvua maana mvua ndio imeindoka haijarudi na alizeti ndio inaanza kufunga maua
View attachment 2203797
ilibidi oale pale scarcity ya cooking oil ilipotokea ungefanya maamuzi.wengi wanaotamba na alizeti kwa sasa ni wale waliohifadhi alizeti kwenye maghala kusubiria demand iwe high and sure this time hesabu imeangukia uoamde wao