JamiiTalks "NAFASI ZA MITANDAO YA KIJAMII NCHINI" - Yaliyojiri katika Mdahalo wa Wanachuo New Africa Hotel

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
631
960


Katika kuchangia ongezeko la Wataalam wengi katika Sheria na Kanuni za Mitandao ya Kijamii, JamiiForums ikishirikiana na Freedom House iliandaa mdahalo kuhusu nafasi ya Kimtandao (Cyberspace) nchini (Kwa taarifa zaidi - MDAHALO (Sheria za Kimtandao): Maalum kwa Wanachuo na Wahitimu wa Kitivo cha Sheria).

Mdahalo huu ulifanyika Jijini Dar es Salaam Hotel ya New Africa Tarehe 3 Agosti na ulihusisha wanafunzi wa Shahada ya Sheria, wakisimamiwa na wanasheria wabobezi na wadau wa Mtandao nchini.

Fuatilia hapa kilichojiri moja kwa moja katika ukumbi huo..

======
03 Aug 2018 JamiiFourms Debate & Discussion

Topic: Are the Laws Governing the cyberspace making it a better & safe place for netizens

Venue: New Africa Hotel, Dar es Salaam.


UTANGULIZI

Maxence Melo - Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media

Habari za mchana, nichukue muda huu kuwakaribisha wote, nawapongeza wote kwa kuja.

Sababu kubwa ya kuanzisha hiki kitu, tulikuwa na mijadala kati ya wanahabari zaidi zaidi na tulikuwa na mijadala kati ya watetezi wa Haki za Binadamu. Tulifikiri tunaweza kujenga mawakili na viongozi tarajiwa sehemu tofauti wenye uelewa na haya mambo ya kimtandao. Sasa tunataka kuwaandaa kuwa wenye uwezo wa kubishana kwa hoja.

Wengi ni vijana na ambao wanaweza kuwakosoa friendly huku wakijifunza. Tunahamasisha wakina dada kushiriki. Ambao mmeshiriki leo tunaomba muweze kuwashawishi na wenzenu kushiriki midahalo inayokuja.

Katika kuchangia leo, tujaribu kujali muda sababu tumepewa dakika mbili mbili.Kama tutapata muda baadae tutaweza kushiriki mdahalo wa kwetu pia hapa mbele... Kuna vitu ambao mnasoma vyuoni, lakini hawa wanaokwenda mahakamani wanaona vitu tofauti na vile vya vyuoni. Kumbuka katika huu mjadala, anayekupinga kwa hoja hana nia mbaya na wewe.

Karibuni sana hapa, hapa ni JamiiForums.

Kuna sheria nyingi zinazohusiana na Mitandao, usipokamatwa na Cybercrime utakamatwa na CPA, EPOCA au sheria ya Usalama wa Taifa. Katika mjadala huu, tunaangalia uwezo wako wa kusimama kwenye point yako na kuitetea. Hapa kutafanya ufanye kazi zako za uwakili kwa kujiamini, onesha uwezo wako ili kujenga mabalozi wazuri.

Kwa mujibu wa TCRA watu wanaotumia internet wamefika Milioni 23. Hawa ni hadhira kubwa hatuwezi kuwapuuza. Mi naona ni jambo jema kuwazingatia.

Tunatarajia kuona mdahalo fikirishi na fikrapevu. Tusione ajabu kuona vijana hawa wakishika nafasi mbali mbali. Tunatarajia kuona mwanasiasa na kiongozi ajaye, tunatarajia wengine wataingia serikani kama mahakimu na nafasi nyingine nyingi kutoka katika kundi hili.

UTAMBULISHO

Aikande Kwayu - Nafanya kazi mbalimbali kwa kujifunza, ushauri elekezi, nafundisha na nafanya utafiti.​
Jeremia Mtobesya - Wakili wa kujitegemea, nimekuwa nikifanya kazi kwenye Human Rights na Cyber cases.​
James Marena - Wakili na mhariri wa zamani​
Benedict Ishabakaki - Wakili wa kujitegemea na wakili wa JamiiForums​
Jebra Kambole - Mwanaharakati wa Haki za Binadamu na wakili wa kujitegemea.​
Dawson Msongaleli - Afisa wa Polisi kwenye kitengo cha Cybercrimes​
Joseph Ngwegwe- Mwandishi na ndiye moderator wa mdahalo.​


UPANDE UNAOKUBALIANA NA HOJA (Wanaokubaliana na uwepo wa Sheria ya Mtandao)


Mchangiaji namba 2 anasema;

Kama mada yetu inavyosema hapo juu. Unatakiwa ujue cyberspace= Ulimwengu wa kimtandao ambao kuna sheria tofauti.​
Umuhimu wa sheria hizi ni nini?​
Sheria hizi zimetokea wapi? Hizi sheria zimetokea kimataifa zikaja Afrika na sasa Tanzania​
Katika Tanzania nusu ya watanzania wana access ya mtandao. Hapa tunazungumzia raia wa mtandaoni, kuna sheria ambazo zinamuongoza. Yapo ya kufanya na kutokufanya. Na yote atakayoyafanya itabidi awajibike nayo. Ulinzi wa mtumiaji unaambatana na suala zima la usajili ili kulinda kwenda kinyume na maadili​


Mchangiaji namba 6 anasema;

Mitandao ya kijamii imeleta athari kwenye jamii mfano Misri. Sasa kama mitandao ya kijamii kama isipodhibitiwa inaweza kuleta matatizo makubwa​
Ni muhimu kuwa na hizi sheria za kimtandao ili kuilinda jamii.​

Mchangiaji namba 8 anasema ;

Tukiangalia mila na desturi, Sheria ya mtandao inakataza picha za ngono kwenye mitandao. Ukiangalia sheria imeweka adhabu ya mil 5 au kifungo miaka 7 kama utasambaza picha za ngono. Hii yote ni katika kulinda maadili yetu. Hizi sheria za mtandao zinasaidia sana kutunza maadili.​
Mchanguaji namba 5 anasema;

Naongelea Cyberbullying.​
Wamesema angalau watu mil 23 wanatumia mitandao ya kijamii. Hapa tunaangalia pia na watoto chini ya miaka 18. Hawa wanapata tabu sana ya cyberbullying. Hii imesababisha watu wengi kujiua kutokana na picha za mitandaoni. Watoto wanatumiwa taarifa ya kutisha na kufanyiwa unyanyasaji.​
Ni vizuri tukawa na hizi sheria ili kusimamia mambo kama haya.​


Mchangiaji namba 7 anasema;

Sheria ambazo tunazo ni bora na zinamlinda mtumiaji wa kimtandao. The Electronic Transactions Act, 2015 inasema; inaweka mashaiti kuhusiana na utambuzi wa miamala ya kieletronic, imeweka vigezo vya kupokelewa ushahidi wa kieletroniki, vilevile kutambuliwa kwa data. Uhalali wa miamala na inamlinda mtumiaji wa mitandao kifungu cha 28 cha The Electronic Transactions Act, 2015. Hii ni baadhi ya malengo ya sheria hii.​
Sheria ya makosa ya kimtandao inafaa kuwepo ili kumlinda mtumiaji.​

Mchangiaji namba 4 anasema;

Ni kweli tupo salama kwenye cyberspace sababu sasa hivi watu wengi wanauza na kununua vitu kutumia mitandao. Sheria ya cybercrime inamlinda mtumiaji wa mitandao. Wengi wanatumia mitandao na kufanya biashara mfano facebook na twitter gulio, watu wanafanya biashara kupitia forex, Jumia, Amazon na wote hawa wanalindwa na hizi sheria. Watumiaji wa mitandao tupo salama​

Mchangiaji namba 1 anasema;

Sheria hizi hazina ubaya mkubwa kama zinavyoelezwa. Sheria yoyote ambayo inakinzana na Katiba sio sheria, sasa ukiangalia kwenye cyber kuna privacy na password. Hizi sheria hazina ubaya wowote.​

UPANDE WA MAWAZO MBADALA (Wasiokubalina na kuwepo kwa sheria ya mitandao)


Mchangiaji namba 1 anasema;

Sikubaliani na Sheria ya Mtandaoni sababu ya uhuru wa kujieleza. Hizi sheria hazitoi uhuru wa watu kujieleza hasa kama ukiongelea mambo ya kisiasa au mambo yanayo ikosoa Serikali. Vile vile haitoi Haki ya faragha. Serikali yetu inafuatilia na kuingilia mawasiliano ya watu kitu ambacho kinaingilia haki ya uhuru wa kujieleza.​


Mchangiaji namba 2 anasema;

Napinga uwepo wa sheria za kimtandao si rafiki, sababu mchakato mzima wakati wa uundaji haukuwa rafiki kwa mtumiaji hata ukiangalia uundwaji. Sheria hizi zimepitishwa kwa hati ya dharura zikiwa na lengo la kubana baadhi ya watu fulani. Mamlaka husika inapoamua kutunga sheria hizi ni vizuri kushirikisha jamii.​


Mchangiaji namba 3 anasema;

Hizi Sheria za mtandao sio rafiki na wala si salama​
Hii sheria ya Mtandao, ushahidi imekubali kwenye makosa ya jinai peke yake ndo imekubali lakini ikakataa masuala Civil law na ikakubali masuala ya benki​
Hii sheria ya Mitandao ina vifungu vinavyoingilia haki ya mtu. Nasema hizi sheria sio rafiki wala sio salama.​


Mchangiaji namba 5 (Joseph) anasema;

Hizi sheria sio rafiki kwa watumiaji. Imewapa hawa waandaa maudhui (contents provider) wamepewa majukumu makubwa sana. Mtu akisema kitu ambacho hakifai anayehukumiwa ni huyu contents Provider.​
Wananchi hatuna haki ya kupokea taarifa. Wanasema napaswa kuwa na password, lakini wanataka nitoe password nimpe mhusika ila hawasemi ni mhusika yupi? Polisi au TCRA? Sheria hii haijaweka wazi. Hii sheria kuna sehemu haitoi ufafanuzi hivyo inatutatanisha.​


Mchangiaji namba 6 anasema;

Hizi sheria sio sahihi, Kwanza hii sheria inapingana na Sheria nyingine. Hawajatoa ni mahakama gani inatakiwa ishughulike na Makosa ya kimtandao. Hii sio salama zilitungwa makusudi kuzingatia maslahi ya watu fulani​
Vile vile hawajaweka court order. Polisi wanaweza kuja kuchukua computer, data muda wowote. Na haijatoa haki ya mtu kusikilizwa, unaweza hukumiwa bila kusikilizwa.​
Hizi content regulations zina tatizo, Publisher hawajasema maana yake ni nini sababu huku wanasema computer. Zinatakiwa zitungwe upya ili kuongezwa usiri na gharama za kujisajili zipunguzwe.​


Mchangiaji namba 7 anasema;

Sheria za mitandao hazifanyi watu kuwa watumiaji salama​
Zile mbio za kutunga ndio zilifanya hizi sheria zisiwe salama​
Kuna makosa yanakwenda kwenda kwenye civil nature na penal code law.​
Hizi sheria ni duplicate, unaweza ukakamatwa na sheria tofauti sababu wamechukua sheria kwenye sheria nyingine na kuzipachika hapa. Kuna haja ya kuzifuta hizi sheria na kuunda upya Sheria za Mtandao​
Hizi sheria zinaweza kufanya windowshopping ya haki. Huwezi jua sheria wameitoa wapi.​


MZUNGUKO WA PILI

UPANDE UNAOKUBALIANA NA HOJA (Wanaokubaliana na uwepo wa Sheria ya Mtandao)

Mchangiaji namba 2 anasema;

Najibu hoja ya Uhuru wa kujieleza;​
Uhuru wa kujieleza umewekewa sheria, hakuna haki ya kujieleza isiyo na mipaka. Mipaka mingine inahusiana na miiko ya kulinda mila na desturi. Tusipoweka mipaka haki za watu wengine zinaweza kuvunjwa na mila na desturi zitavunjwa.​
Haki ya usiri ipo katika Katiba lakini haki hiyo imewekewa sheria. Tunaweka haki ya siri ili kuzuia watu wasiingiliwe kwenye usiri wao. Siracusa principles​
Je, katika jamii yetu tunaruhusu kutukana? Sisi watanzania sio kama Marekani, tuna maadili yetu.​


Mchangiaji namba 7 anasema;

Naomba ifahamike hizi sheria zinamlinda mtumiaji wa mtandao.​
Sheria kupitishwa kwa hati ya dharura sio dhambi. Soma sheria za kibunge za kupitisha sheria za dharura. Haimanishi wadau hawajasikiliza kwani kamati ya kudumu ya bunge lazima iitishe wadau.​
Sheria ya cybercrime kwamba imerudiarudia sheria nyingine.​
Kabla ya mwaka 2015 tulikuwa hatujajitosheleza kwa sheria za kimtandao. Kwamba upatikanaji haukuwa rafiki kwamba wadau hawakushirikishwa. Sio kweli. Wadau na asasi za kiraia zilishirikishwa pale ukumbi wa Mwalimu Nyerere.​
Hizi Sheria hazijatungwa kwaajili ya watu fulani hapana. Kama wadau hawakwenda kutoa maoni yao walipoitwa ni uzembe wao.​


UPANDE WA MAWAZO MBADALA (Wasiokubalina na kuwepo kwa sheria ya mitandao)

Mchangiaji namba 2 anasema;

Haimanishi kwamba sababu wewe umekiona kitu ni mwiko ukafikiri na mimi ni mwiko hapana. Kila mmoja ana haki sawa mbele ya sheria. Sheria inatakiwa itende haki kwa wote bila kubagua​


Mchangiaji namba 3 anasema;

Kuna jamaa kasema hizi sheria ni nzuri. Unakuta mtu amekosea kwenye civil matter anakuwa criminalised. Hudhani kwamba hii itamuathiri mlengwa?​


Mchangiaji namba 5 anasema;

Kwa mara nyingine napinga hizi sheria. Je nani anadetermine kwamba hizi ni habari za kweli au sio za kweli?​
Juzi kuna mtu alisema kitu kimepotea, wengine wakasema kipo. Sasa nani mkweli? Aliomba msamaha? Alifanywa nini?​
Hizi sheria zilitakiwa kuhimiza vijana wawe wabunifu.​
Kifungu cha 64 cha Katiba kinaipa mamlaka bunge kutunga sheria. Sio kila sheria inayotungwa inatungwa kwa madhumuni ya kutusaidia sisi bali nyingine zinatungwa kuwasaifia waliopo madarakani. Hizi sheria zitakuja zikukute au zimkute mwanao, ipo siku itamkuta. Sheria ilipitishwa na wabunge wachache halafu unaitetea. Wabunge wapo zaidi ya 300 lakini sheria ilipitishwa na wabunge 23.​

Mchangiaji namba 7 anasema;

Makosa mengi ya cybercrime yameachwa hewani yaani hujui nini ni nini. duplicate ya sheria nyingine. Kilichotakiwa ni kufanyia marekebisho ya sheria zilizokuwepo sio kutengeneza sheria hizi.​

Mchangiaji namba 5 anasema;

Mamlaka iliyopewa kusimamia hizi sheria ni TCRA ambayo ipo Dar tu. Wamiliki wa Radio wanalipa laki mbili lakini blogger analipa milioni 1 hii ipo sawa? TCRA waongeze maofisa. Mtu anatoka Kigoma anakuja Dar kusajili kablog.​


HITIMISHO

UPANDE UNAOKUBALIANA NA HOJA (Wanaokubaliana na uwepo wa Sheria ya Mtandao)

Mchangiaji namba 6 anasema;

Maadili ya jamii tunayoyazungumzia ni yale yanayogusa jamii fulani. So tunaangalia hizi sheria zinavunja maadili ya watu fulani. Sheria haitendi haki kwa wote.​
Kuna waliosema kwamba hizi sheria zisaidie ubunifu. Hizi sheria ni za kukataza mabaya sio kuhimiza ubunifu.​
Kuna aliyosemea gharama. Kwenye internet kuna matangazo na internet inaenda dunia nzima lakini radio ni nchi tu. Internet ina nguvu sana.​


Mchangiaji namba 7 anasema;

Ntaongelea haki bunifu. Hii sheria inamlinda moja kwa moja, mtu akikuta amevunja kufungu cha 24 atalindwa na hii sheria.​
Kuna mtu kasema TCRA ijiongeze. TCRA ipo kila sehemu kikanda. Hii sheria lazima isomwe kipengele cha 31. Kama hii ipo kimya tunatumia sheria ya makosa ya jinai. Kuna sheria inaongoza masuala ya sheria na ukamataji.​


Mchangiaji namba 3 anasema;

Inakuaje mimi maadili yangu yatakuwaje maadili yako? Kwa jamii ya Tanzania yanafanana kila sehemu. Kumpiga mzee wako hakuna anayeruhusu.​


Mchangiaji namba 2 anasema;

Uhuru wa maoni naona watu hawajaielewa. Kuna uhuru wa kutoa maoni bila kuvunja sheria za nchi​

UPANDE WA MAWAZO MBADALA (Wasiokubaliana na kuwepo kwa sheria ya mitandao)

Mchangiaji namba 4 anasema;

Hakuna sheria inayozungumzia maadili, hata katiba ya Tanzania hamna kitu kinachozungumzia maadili. Yanabakia kuwa ni mambo ya mijadala hata wanaopiga picha mbaya hamna anayepelekwa mahakamani.​
Bunge ndo chombo cha kutunga sheria. Wabunge wapo 300 lakini wabunge 23 ndio waliopolitisha sheria. Nashauri Wabunge watunge sheria ambazo hazivunji haki za binadamu.​
Hizi sheria zimeleta makosa ya jinai na madai humu. Naomba hizi sheria zifutwe na kama kuna vifungu vinafaa sheria nyingine zifanyiwe malekebisho ili viingizwe.​
Hizi sheria za 2015 na 2016 zinamuachia mahakama/hakimu kuamua adhabu atakayokupa. Adhabu mbayo si chini ya miaka 3 au si chini ya faini ya mil 4 lakini hawajaweka kikomo. Hivyo hukumu itategemea hakimu ameamkaje.​


Mchangiaji namba 1 anasema;

Kuna mtu amezungumzia TCRA, hawapo popote zaidi ya Dar es salaam.​
Ukitaka uweke sheria ya matakwa yako ambayo si matakwa yangu unakuwa unanionea. Kwenye sheria hatutakiwi kuwa na sheria zinazopendelea upande mmoja na kuumiza mwingine.​
Mfano twaweza walikuja na utafiti kwamba Kukubalika kwa rais kumeshuka. Imekuwa mjadala na kitimoto wamepewa. Je twaweza wangesema umaarufu umepaa, je twaweza wangepata misukosuko?​
Hawa wanaopitisha sheria ni chama tawala, hawawezi kupitisha sheria ya kumupendelea mpinzani. Sheria imepitishwa na wabunge 23 huku wengine wakikatazwa kuzungumza bungeni.​
Watu wanatoa wito bila kufuata sheria. Hayo ni maadili?​
Zitto aliitwa kwenye matamko ya kisiasa naye akasema wafuate sheria. So hizi sheria zinatumika kisiasa.​


MAJAJI

Maxence
Nawapongeza watu wengi wameongea vizuri. Umeona kwanini hatujaenda live? Siku nyingine tutaenda live kuna watu walikuwa hawakusoma wala kujiandaa.

Mdahalo wa pili mutaongeza kujiamini na kusoma. Mdahalo ujao msome msome itapendeza. Nataka majaji watoe maoni yao.


Benedict Ishabakaki

Mmefanya vizuri.​
Wanaokubali uwepo wa Sheria mko vizuri. Yaani mlijiandaa. Kuna watu nmeshindwa kuelewa wapo upande gani... Mumekuja na vitu vipya kama kanuni za bunge. Timu inayokataa sheria ni timu nzuri.​
Maandalizi mmefanya 80% lakini hamjatumia muda vizuri kwani mlikuwa mnabakiza dakika. Mwanasheria ukipewa muda hutakiwi kuuacha.​
Cybercrime haipo wazi.​
Mmefanya vizuri. Lakini hamjajiandaa vizuri kama wenzenu. Mngekuja na takwimu wangapi wamefungwa. Mngesema zinawaathiri vipi Wanafunzi.​
Kuna watu ambao ni wazuri kujieleza na wanajiamini, tutawachukua kwenye law firm zetu​

Jebra Kambole

Nimependa mnavyojiamini.​
Mmejitahidi kufanya utafiti lakini sio sana, kitu ambacho hujui bora unyamaze kuliko kuongea kitu isixhokijua. Upande mmoja wanapokuwa wanaongea wengine muwe mnanote vitu ili muwezi kujibu vizuri. Mfano kusema "Kuna jamaa kule kasema". sio vizuri, kuweni makini. Fanya utafiti. Cyberspace bado ni changamoto. Ni sehemu ambapo tunakutana bila kibali wala kuomba ruhusa mtu. Tuna sheria zinabana offline na oline. Mimi niwapongeze sana.​
Arguments ndo suala la msingi katika kazi hii. Uzungumze unachokiamini lakini unachozungumza inaweza isiwe na maana kwenye sheria. Mnachokisimamia ni kizuri. Mlijipanga vizuri.​

Dawson Msongaleli

Upande wa wanaopinga Sheria, mje na utafiti. Lazima ujiandae. Kwenye sheria kusoma ni lazima. Jiandaeni. Nikwambie kitu Max, hawa vijana hata ungeweka live, hawa jamaa wamejiandaa. Kila mtu kazungumza anachojiamini.​


Jeremiah Mtobesya

Kama mnatakiwa muwe mawakili, kujiandaa ni muhimu. Hawa wanaokubaliana wamejiandaa sababu sheria zipo upande wao. Nyie mnaopinga hamjajianda hamkufanya kazi kitimu.​
Mwanasheria huwa hakosei bali anakuwa na error tu. Amini kwenye kesi yako.​
Jiamini, Jaji ukimletea maneno ya kujikanyaga mtaonekana mnaboa.​
Jaribu kuwa teamwork. Hawa upande wa yes walikuwa teamwork na nyie hamkuwa teamwork.​
Nimesikia mnazungumzia vifungu vya Katiba, ndo mnaanza lakini kuna baadhi ya vifungu kwenye Katiba vina chujio. Wasomeni wakina Mbushuu, Daud Pete, Mjomba Mjomba nk. Hata kama Katiba imekatazwa ina kipimio chake. Mmefanya vizuri.​


Aikande Kwayu

Msome sana. Jitahidi kusoma sana pia historia, Mfano huyu mwenye shati jekundu kasema sheria zimeanzia Ulaya. Lazima usome kwamba sheria Ulaya zilianzaje​
Nimefurahi kuhusu lugha. Kuna watu wametumia kiswahili na kiingereza, muhimu kuelewa lugha.​
Max na Asha naomba siku nyingine waongee lakini walete na maandishi sababu ni kitu tunahitaji.​
Time management inatakiwa.​
Siku nyingine hawa watu wa JamiiForums wawachanganye.​


Dawson Msongaleli

Naomba nituoe ufafanuzi. Mimi hapa sijaja kama msemaji wa Polisi bali nimekuja kama watu wengine kushiriki mjadala.​
Kitu kingine naomba niondoe dhana potofu eti Polisi hawajasoma. Polisi kuna wasomi wengi sana tena wa Masters tu. Kuna wasomi wengi hadi mkuu anashindwa awape vipi motisha.​
Nashukuru kwa mjadala ambao ulikuwa na tija.​
1. Kitu cha kwanza ni kujiamini. Sisi askari tunafundishwa kujiamini.​
2. Mlikuwa mna tatizo la kuelewa mada. Discussion yetu mmebase Tanzania tu. Ilitakiwa iwe ya kitaifa. Panueni mawazo.​
3. Nyie mnaotetea cyberbullying lakini hamji mkasema sheria inamlindaje mtu asifanyiwe makosa. Wanaokubali mmejipanga lakini hamkuwa na takwimu.​
Mlitakiwa mseme watu wameguswaje. Hamna takwimu wala data. Hamjashawishi.​
Waandaaji, dakika mbili hazitoshi. Siku nyingine ongezeni muda.​


Asha D. Abinallah, Meneja Mikakati na Uendeshaji wa JamiiForums

Asanteni sana kwa mjadala mzuri na kwa wote walioweza kufika hapa na kushiriki. Mapendekezo yote yaliyotolewa tutayafanyia kazi. Naomba kutoa angalizo kwamba makundi haya mawili ya mdahalo (Affirmation na Negative) tuliyatenga na kupanga wenyewe, hivyo watakapo fanya tena mdahalo makundi yatapangwa upya. Nawapongeza sana vijana kwa waliokuwa wamejitokeza kushiriki. Inatia faraja. Inshaallah hadi wakati mwingine, Asanteni.​


Picha za washiriki na majaji

1.jpg

Kutoka Kulia ni Dawson Bukombe kutoka kitengo cha Police Cyber Crime Department, Wanasheria Jebra Kambole na Benedict Ishabakaki, Maxence Melo Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Mwanasheria James Marenga, Dr. Aikande Kwayu na Mwanasheria Jeremiah Mtobesya
(Jopo la Majaji)

2.jpg

Kundi lililokuwa likiwakilisha Wanaokubaliana na uwepo wa Sheria ya Mtandao


3.jpg

Kundi lilikokuwa likiwakilisha Wasiokubaliana na uwepo wa sheria ya mtandao
 
1.JPG

Maxence Melo - Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media

2.jpg

Joseph Ngwegwe msimamizi wa mdahalo akitoa mwongozo

3.jpg

Asha D. Abinallah, Meneja Mikakati na Uendeshaji wa Jamii Media

4.jpg

Dr. Aikande Kwayu

5.jpg

Wakili Benedict Ishabakaki


6.jpg

Wakili Jebra Kambole


7.jpg

Wakili Jeremia Mtobesya


8.jpg

Dawson Msongaleli, Afisa wa Polisi kwenye kitengo cha Cybercrime


9.jpg

Kiiya Joel, Mtendaji Mkuu wa C-Sema


10.jpg

Washiriki wasiokubaliana na uwepo wa sheria ya mitandao wakijadili jambo kabla ya kuwasilisha hoja zao


11.jpg

Baadhi ya washiriki wanaokubaliana na uwepo wa sheria ya mitandao wakijadili


12.jpg

Mshiriki anayekubaliana na uwepo wa sheria ya mitandao akiwasilisha hoja zake


13.jpg

Mshiriki asiyekubaliana na uwepo wa sheria ya mitandao akiwasilisha hoja zake


14.jpg

Mshiriki asiyekubaliana na uwepo wa sheria ya mitandao akiwasilisha hoja zake


15.jpg

Mshiriki anayekubaliana na uwepo wa sheria ya mitandao akiwasilisha hoja zake


16.jpg

Mshiriki anayekubaliana na uwepo wa sheria ya mitandao akiwasilisha hoja zake


17.jpg

Mawakili Kambole na Ishabakaki wakiteta


18.jpg

Mshiriki wa mdahalo akiuliza swali

19.JPG

Baadhi ya Washiriki katika Mdahalo huo

20.jpg

Baadhi ya Washiriki katika Mdahalo huo​
 
Nilipata nafasi ya kushiriki huu mdahalo, nilijifunza mengi sana na bado ninajifunza mengi kuhusu nafasi ya sheria hizi kwa jamii. Mijadala ya namna hii yenye tija inatakiwa ifanyike mara kwa mara na isiishie kwenye miji tu. Hata huko vijijini wanatumia mitandao na nina uhakika ndio kuna wahanga wengi wa sheria za mtandao maana elimu sahihi haijawafikia.

Nawapongeza sana JF na washiriki wote.
 
Sheria kandamizi hutungwa na viongozi madikteta kwa sababu hofu. Huwezi kuzuia uhuru wa social media kwa kutunga sheria kandamizi nilitamani ningeshiriki huu mdahalo sikupata nafasi Hongera sana uongozi wa Jamii Forum kwa kuandaa huu mdahalo.
 
Mi nafikiri ni kweli sheria hii ilitungwa mahsusi kwa watu fulani. Watu wanaotumia mitandao vibaya! Basi. Hakuna sheria isiyotungiwa watu fulani. na hao watu fulani, bila shaka ni wale wahalifu! La sivyo tuambiwe kwamba kuna kundi maalum ambalo ni wateule wa kutumia mtandao na wengine hawana haki hiyo na ambao ndio wametungiwa sheria hii.
Kumbukeni mwisho wa uhuru wako ndio mwanzo wa uhuru wangu na kwamba hakuna uhuru usio na kikomo!
Aidha lazima tujiulize kwamba, kama wabunge 23 ndio waliopitisha mswaada huu, je, kanuni za bunge zinasemaje juu ya akidi hitajika katika upitishwaji wa miswaada?
 
Nimependa sana mdahalo huu, spirit yake, malengo yake. Walioandaa kila la heri na endeleeni na jitihada hizo kwa maslahi ya taifa letu. by the way, MASLAHI YA TAIFA ni jambo lililopotoshwa sana na wanasiasa. ninyi mnaangalia MASLAHI YA KWELI YA TAIFA
 
Sawa, ni vizuri sana sheria kuwekwa ila zisiwekwe sheria kandamizi hasa kwa kulenga kundi fulani na hii ndo inayoleta tafasiri mbaya kwa hizi sheria.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom