Musukuma: Kikokotoo cha 33% kitazalisha Watumishi wezi, hawatajli tena kazi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,435
8,254
DODOMA: Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma amesema Setikali inatakiwa kufanyia kazi malalamiko ya Watumishi kuhusu suala la Kikokotoo cha 33% vinginevyo wataanza kuiba kwasababu wanajua wakistaafu hawatalipwa mafao yao yote.

Amesema "Kuna vitu vinazungumzwa tunaona kama haviwaumizi wananchi, yaani natakiwa nistaafu nikajitegemee sina nyumba halafu naenda kupata 30% lazima niondoke na mzigo liwalo na liwe. Watumishi wanalia na kikokotoo Serikali iwasikilize".

Kauli ya Musukuma inafuatia mvutano unaondelea Bungeni na Makazini kuhusu madai ya Watumishi kutaka asilimia za Kikokotoo ziwe kati ya 50% hadi 60% ya Mafao ya Kustaafu wakati kwasasa kiko 33%.

Soma LIVE - Joseph Musukuma: Kikokotoo kinawaumiza wananchi, tunatengeneza taifa la wezi
 
Musukuma Yuko sahihi....mifuko ya hifadhi ya jamii inawakandamiza sana wastaafu. Ingewezekana wapewe hela yao yote wakafie mbali maana iko wazi mshahara ya watumishi haitoshi.
Kusiwepo kisingizio eti wanatunziwa....mnawajengea watu uoga mpaka kwenye kutunza hela zao wenyewe
 
Hiki kikokotoo ni cha hovyo mpaka basi. Nadhani watetezi wake watakuwa na matatizo ya akili kwenye vichwa vyao.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Kwa upande mm naona, sasa ivi hili bunge la chama kimoja linakaa pembeni na kuandaa agenda nyeti zinazowagusa watu, wanazijadili kwa muda mrefu kwenye muelekeo ambao watu hawautaki, then baada ya muda anajitokeza kiongozi wao na kutoa maamuzi muelekeo wa wananchi, so lengo ni kutupanga kuelekea kwenye chaguzi zilizo mbele yetu ili wapate kura kuonekana wanajali wananchi.

So haya yote yanayoendelea yanalenga uchaguzi mkuu.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Kutokana na Serikali kutokutoa Elimu ya Kutosha kwa Watumishi wa Umma na Wastaafu watarajiwa na kusababisha Mslumbano makali nadhani sasa ndio muda sahihi kwa Serikali kutoa ELIMU na FAIDA zitakazopatikana kwa KIKOKOTOO KIPYA Faida ambazo hazikuwepo kwenye KIKOKOTOO cha Awali.Kufanya hivyo kutasaidia Wahanga kukielewa KIKOKOTOO KIPYA tofauti na Sasa kila mtu anatafsiri yake juu ya KIKOKOTOO.
Wapo wanaosema Mafao ya Mstaafu ya kila Mwezi ni Asilimia 75% ya Mshahara aliostaafia
Wapo wanaosema Mstaafu akifariki Mafao yake inapewa Familia yake tofauti na KIKOKOTOO cha Zamani.Mambo kama haya SERIKALI inapaswa ITOE ELIMU kupitia VYOMBO vya HABARI ili Wahusika waelewe na ikibidi WAULIZE MASWALI na KUJIBIWA.
 
Musukuma Yuko sahihi....mifuko ya hifadhi ya jamii inawakandamiza sana wastaafu. Ingewezekana wapewe hela yao yote wakafie mbali maana iko wazi mshahara ya watumishi haitoshi.
Kusiwepo kisingizio eti wanatunziwa....mnawajengea watu uoga mpaka kwenye kutunza hela zao wenyewe
Wakati inapitishwa alikuwa Bungeji au hakuwepo?
 
Kutokana na Serikali kutokutoa Elimu ya Kutosha kwa Watumishi wa Umma na Wastaafu watarajiwa na kusababisha Mslumbano makali nadhani sasa ndio muda sahihi kwa Serikali kutoa ELIMU na FAIDA zitakazopatikana kwa KIKOKOTOO KIPYA Faida ambazo hazikuwepo kwenye KIKOKOTOO cha Awali.Kufanya hivyo kutasaidia Wahanga kukielewa KIKOKOTOO KIPYA tofauti na Sasa kila mtu anatafsiri yake juu ya KIKOKOTOO.
Wapo wanaosema Mafao ya Mstaafu ya kila Mwezi ni Asilimia 75% ya Mshahara aliostaafia
Wapo wanaosema Mstaafu akifariki Mafao yake inapewa Familia yake tofauti na KIKOKOTOO cha Zamani.Mambo kama haya SERIKALI inapaswa ITOE ELIMU kupitia VYOMBO vya HABARI ili Wahusika waelewe na ikibidi WAULIZE MASWALI na KUJIBIWA.
Unadhani hiyo elimu watumishi hawana au hawafahamu? You guys stop pretending as if watumishi ni kundi fulani la wapumbavu
 
serikali ya majizi na machawa , wao kula hela ni halali lakini kwa watumishi wao ni haramu, BONGO BAHATI MBAYA SANA
 
hawa waheshimiwa wawili; Msukuma na Kishimba nawaelewa sana
Wanaupeo wa hali ya juu wa kuelewa na kuchanganua mambo na ujue ni wa darasa la saba
Ukichambua hoja zao pole pole, utagundua kuwa, hawa watu hasa Kishimba ni super genius. Ningekuwa Waziri, Kishimba ni kati ya watu ningewaweka kwenye baraza langu la ushauri la uwekezaji...
 
Watumishi 80% ni wezi, wazembe , wanafiki, waoga ndo maana nchi haipigi hatua. Kwa sifa zao hizo hata hiyo 33% wasipewe .
 
Back
Top Bottom