Breaking News: Mshukiwa wa shambulio la Westgate 'atekwa nyara na watu waliojihami' baada ya kuachiliwa Kenya

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,240
4,768
Liban Abdullahi Omar hakupatikana na hatia za makosa ya ugaidi siku ya Jumatano

Mtu mmoja ambaye hakupatikana na hatia katika shambulio la kigaidi la West Gate nchini Kenya ametekwanyara alipokuwa akielekea nyumbani.

Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kwamba Liban Abdullahi Omar alikuwa ndani ya teksi na dada zake wakati watu waliojihami kwa bunduki waliposimamisha gari lao na kumtekanyara.

Wakili wake Mbugua Mureithi , aliambia Chombo cha habari cha AP kwamba watu hao walijitambulisha kama maafisa wa usalama. Polisi imekataa kutoa tamko.

Walidaiwa kumkamata na kumweka katika eneo la nyuma la gari lao mbali na kuchukua funguo za teksi hiyo.

Omar ambaye ni mkimbizi wa Somalia nchini Kenya alikuwa anatoka katika kitengo cha maafisa wa kukabiliana na ugaidi mjini Nairobi wakati alipotekwanyara kulingana na Khelef Khalifa mkurugenzi wa shirika la haki za kibinadamu la Kiislamu Muslim For Human Rights.

Alikua ameachiliwa kutoka katika jela ya kamiti na kwamba alikuwa anajaza stakhabadhi za kumwachilia huru kama ulivyo utaratibu wa washukiwa wa ugaidi katika afisi za maafisa wa kukabiliana na ugaidi..

Bwana Khalifa alisema kwamba watu waliojifunika uso waliovalia nguyo nyeusi waliizuia teksi iliokuwa imembeba bwana Omar.

Wakili wake Mbugua Mureithi aliambia runinga ya NTV kwamba watu hao wlaijitambulisha kuwa maafisa wa usalama.

Alishtakiwa pamoja na watu wengine wawili.

Wote wawili walipatikana na hatia ya kuwasaidia washukiwa wa shambulio hilo na kwamba watahukumiwa tarehe 22 mwezi Oktoba.

hapa ndio utajua sio kila wakati utawala wa sheria unatoa haki.

yaani hapo hatua za kimahakama na maamuzi yake yamepishana na upelelezi.watu wa usalama wanaona jamaa ana deni la kulipa,mahakama imekosa ushahidi wa kumkuta na hatia.

ndio hapa kauli maarufu ya polisi wa bongo huibuka"ameuwawa alipojaribu kuponyoka akiwa anakwenda kuonyesha wenzie walipo"imeisha hiyooo.
 
Sheria siyo uhakika wa haki kutendeka.
Sheria hazikumkuta na hatia lakini haki ya waliohathirika na ughaidi haikutendeka kwa kuachiwa huru Kama kweli alihusika.

As the famous colonel from TZ said "sadism is inevitable when the situation is alarming"
 
Liban Abdullahi Omar hakupatikana na hatia za makosa ya ugaidi siku ya Jumatano

Mtu mmoja ambaye hakupatikana na hatia katika shambulio la kigaidi la West Gate nchini Kenya ametekwanyara alipokuwa akielekea nyumbani.

Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kwamba Liban Abdullahi Omar alikuwa ndani ya teksi na dada zake wakati watu waliojihami kwa bunduki waliposimamisha gari lao na kumtekanyara.

Wakili wake Mbugua Mureithi , aliambia Chombo cha habari cha AP kwamba watu hao walijitambulisha kama maafisa wa usalama. Polisi imekataa kutoa tamko.

Walidaiwa kumkamata na kumweka katika eneo la nyuma la gari lao mbali na kuchukua funguo za teksi hiyo.

Omar ambaye ni mkimbizi wa Somalia nchini Kenya alikuwa anatoka katika kitengo cha maafisa wa kukabiliana na ugaidi mjini Nairobi wakati alipotekwanyara kulingana na Khelef Khalifa mkurugenzi wa shirika la haki za kibinadamu la Kiislamu Muslim For Human Rights.

Alikua ameachiliwa kutoka katika jela ya kamiti na kwamba alikuwa anajaza stakhabadhi za kumwachilia huru kama ulivyo utaratibu wa washukiwa wa ugaidi katika afisi za maafisa wa kukabiliana na ugaidi..

Bwana Khalifa alisema kwamba watu waliojifunika uso waliovalia nguyo nyeusi waliizuia teksi iliokuwa imembeba bwana Omar.

Wakili wake Mbugua Mureithi aliambia runinga ya NTV kwamba watu hao wlaijitambulisha kuwa maafisa wa usalama.

Alishtakiwa pamoja na watu wengine wawili.

Wote wawili walipatikana na hatia ya kuwasaidia washukiwa wa shambulio hilo na kwamba watahukumiwa tarehe 22 mwezi Oktoba.

Moderator hii habari mpaka leo hii ni breaking news?
Tafadhali rekebisheni hili.
 
Back
Top Bottom