Frank Wanjiru
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 22,358
- 40,040
Msemaji wa timu ya Tabora United FC, Christina Mwagala amemjia juu Mchambuzi wa Soka, Jemedari Said kufuatia kauli aliyoitoa juu ya kinachoendelea kwenye timu hiyo.
"Nafikri wewe kibabu Jemedari Said kuna kitu unakitaka ndani ya klabu yetu ya Tabora UTD muda sio mrefu utakwenda kukipata, Ila kwa kukusaidia kaa mbali kabisa na hii timu.
"Tabora sio sehemu ya kufuga machawa, sasa nakuonya kwa mara nyingine kaa mbali na hiii timu., mimi siongei sana na watu wapumbavu, isipokuwa nakuonya kwa mara nyingine tena kaa mbali na Tabora United FC." ameandika Christina baada ya Jemedari kuandika ujumbe huu (chini).
Aliyoandika Jemedari "Hali kwenye klabu ya Ligi Kuu ya NBC Tabora United FC inazidi kuwa mbaya baada ya Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wake kujiuzulu leo asubuhi. Thabiti Kandoro ameandika barua kwa uongozi wa klabu akiomba kuondoka klabuni hapo baada ya mazingira ya kufanya kazi kuwa magumu kupita kiasi.
Habari ambazo Bin Kazumari imezipata inasema klabu inakabiliwa na madeni kila kona kutokana na UKATA MKUBWA ambao iko nao. Katika hali isiyo ya kawaida inasemekana klabu hiyo ya Ligi Kuu imeondokewa na sehemu kubwa ya watendaji wake (sekretarieti) kwakuwa hawalipwi hali iliyopelekea kubakia na CEO na Afisa habari pekeyao, hata hivyo habari zaidi zinasema Bi Christina Mhagala MCO vifaa vyake vimezuiwa kwenye lodge moja mjini Tabora kwa kudaiwa pango.
Baadhi ya vifaa kama jezi za klabu zimezuiwa kwenye lodge nyingine ambayo mmiliki wake ni mwanamke naye anaidai klabu, hali iliyopelekea klabu hiyo kucheza mechi zake 3 za mwisho ikiwa imevaa jezi za rangi ya buluu bila kubadilisha kwakuwa zingine zimezuiwa lodge. Katika mechi dhidi ya Coastal Union, Dodoma Jiji na KMC klabu hiyo haikubadili jezi sio kwa kutaka bali jezi nyingine zimezuiwa.
Timu ya U20 ilicheza mechi Bukoba tarehe 24 Machi 2024, ikalazimika kukaa mpaka tarehe 26 ikisubiri pesa ya mafuta, ilipotumwa wakaja mpaka njiani gari ikaisha mafuta wakadandia malori ya mizigo, klabu ya wakubwa wana siku 3 wanaenda mazoezi kwa miguu kwakuwa hakuna gari. Wakati huu wa mapumziko ya ligi wenzao walio katika hatari ya kuteremka daraja wako kambini wao wanahangikia pesa ya kula. Aliyosema kocha Kapunovic yote yalikuwa yana ukweli ndani yake."