Zero One Two
JF-Expert Member
- Sep 16, 2007
- 9,347
- 3,023
Nilifika Jana TNG saa 9 kasoro ivi, bahati mbaya ni mala yangu ya kwanza kufika pale, basi katika uliza uliza kuna binti mmoja ni mrembo hata beyonce hatii mguu pale, akasema eti na yeye ni Jf member ametumwa kunipokea, mie nikakubali akabeba ka mzigo kangu, nilikua nazawadi za Arushaone, Filipo, na watu8 pamoja na PJ. Cha ajabu tukaingia kwenye nyumba moja ivi nikakuta watu wengi nikasema duh! Hawa wote ni wana CC nikafurahi kimoyo moyo, cha ajabu yule binti akaniingiza kwenye chumba kulikua na wazee kama wa 4, then akanitambulisha mie ndie mwenye ujauzito alio nao lol! Hapo hapo ukaletwa ubani na tukafungishwa ndoa, asubuhi ya leo wakatupa kiwanja cha kuanzia maisha na mtaji, na wameniambia nikajiribu kukimbia mimba itahamia kwangu na ikifikisha miezi 9 nitakufa. Jamani njooni mniokoe huku mwenzenu