Nashukuru sana kwa ushauri mzuri nimekuelewa vyema...sema hapo mwisho sasaSina ujuzi sana ila acha nijaribu. Mtu wa kumanage fedha anatakiwa awe mwaminifu na ni nzuri ukamuweka mke ama ndugu wa karibu. Sometimes wanaweza wasiwe watu bora, basi vyema ukamuweka mtu mzima kidogo maana vijana bado wanatafuta maisha. Asije akanyanyuka na wewe huku wewe mwenyewe unataka kunyanyuka.
Upate m/wapishi wazuri. Vyombo vyako viwe vizuri. Mazingira yawe safi so ununue dawa za kufanyia usafi kuepusha wadudu mbalimbali. (Kuna sehemu nilishawahi kwenda kula Mwenge, mende walikua wanatoka chini ya meza). Sali upate wahudumu wazuri kuanzia muonekano mpaka kauli hasa kauli. Mhudumu akiwa na hekima utapata raha sana. Na pia kuwe na daftari maalum la kuonyesha mauzo yanayotoka na bei ili kila siku ufunge na kufungua hesabu. Hii itakusaidia kuona wapi panahitaji umakini na adjustments za kufanya.
Mwisho kwa sabbu ndo unaanza kama vipi jitahidi sana uwepo kila siku atleast kwa miezi 3 ya mwanzo ili uone mambo yataendaje katika hiyo biashara. Chanzo cha pesa chochote kinalelewa kama mtoto. Umakini na Uthabiti plus juhudi vinahitajika mno.
NB: Natafuta kazi.
Nimesubiri sana ushauri wako bossNakuja baadae kukupa ushauri
Kwanza ni sehemu gan unategemea kufungua? Kama ni Arusha naweza kukusaidia Zaid kwa vitendo
Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Sahihi mkuu nashukuruKama una mtaji, location ya biashara yako ndio factor nyingine kwakuwa huyo itaonyesha kuwa umelenga ku capture wateja wa aina gani na kama utawapata.
Sio unaenda kufungua hiyo classic restaurant uswahili wakati watu wa huko menu yao ni utumbo na speed/reki za kuku.
Asante sana kwa wazo bomba mkuuMigahawa inalipa sana,kazi ngumu ni kubalance chakula na wale wasaidizi wako wasikuibie hela na wasisahau kuchukua hela kwa wateja maana kuna wakati huwa naona wanabug hesabu
Mfano wahudum wengi wameshazoea ukiagiza chai na chapati wanajua chapati zilikuwa mbili hata kama uliagiza tatu
Mtaji kiasi gani wa kuanza nao hususani Arusha na ni maeneo gani hot kwa Arusha?Habari mkuu,
Hongera kwa wazo Bomba kabisa
Wazo Hilo ni mojawapo Kati ya mawazo yangu
Fanya hivi broo,
1, tafuta wafanyakazi wenye Nia ya kufanya kazi, dispiline, na wanaojali kazi
Tengeneza menu Pana (vyakula vya Bei RAHISI na vya Bei ghali pia)
Kuwa tofauti na washindani wako kw promotion za mara kwa mara
Ukiweza weka free wi-fi Ila yenye limit time
Tafuta mpishi anayejua kupika vizuri ili uwe tofauti na wenzio
2:funga CCTV camera kwa ajili ya usalama wa Mali zako na za wateje
3; jua udhaifu wa washindani zako
4 usafi ni jambo ambalo kila mteja atataman kuwa sehemu safi kuanzia
Watu wa service na mazingira kwa ujumla
Wapende wafanya kazi wako hasa kwa kuwapa mishahara kwa wakati
Wajali pia kwa kuwapa offa kila wanapofanya vizuri kwa kufanya hivyo utakuwa karibu nao kila jambo kabla halijatendeka utajulishwa
Tengeneza loyalty card kwa ajili ya wateja wako wa kila mara kupitia loyalty card utawapa offa hasa kahawa, au chai
Ni hayo tu
Hili lizangatiwe sana!Migahawa classic bongo hailipi,watu wanapenda sehemu kocal za kawaida ndio utapata wateja,ukizidisha mbwembwe wanakimbia ,zingatia sana huu ushauri
Ukipata muda nenda singida nyuma ya TRA ulizia karestaurant ka mama mmja anaitwa mama clare nenda ufanye survey utajifunza kitu paleWapendwa kama ambavyo nimeandika hapo, naomba msaada wa kitaalamu jinsi ya kuendesha biashara hii.
Sijafungua ila nimesha fanya maandalizi ya chumba pamoja na vifaa baadhi, ishu kubwa itakuwa kwenye kumanage pesa na wafanyakazi nk.
Wapendwa kama ambavyo nimeandika hapo, naomba msaada wa kitaalamu jinsi ya kuendesha biashara hii.
Sijafungua ila nimesha fanya maandalizi ya chumba pamoja na vifaa baadhi, ishu kubwa itakuwa kwenye ku-manage pesa na wafanyakazi nk.
Inategemea na ukubwa na standard ya mgahawa wakoMtaji kiasi gani wa kuanza nao hususani Arusha na ni maeneo gani hot kwa Arusha?