LoyalTzCitizen
JF-Expert Member
- Sep 15, 2010
- 2,234
- 883
kWANZA HABARI ZA MISHUGHULIKO WAKUU!
Najua humu kuna wakuu wenye knowledge, skills na peofessionals tofauti na ndio maana tukaitwa great thinkers. Sasa mategemeo yangu pia nitapata mawazo mazuri yanayoeleweka na yenye manufaa sababu nipo katika njia ya panda na niko desperate sana ya kuomba msaada wa kuanzia wapi ili niokoe kiwanja changu na nyumba yangu ambayo nataka kuporwa! naama! KUPORWA na waumini wa dini ya Kiislamu ambao wamenitia majonzi sana na kuninyima usingizi.
Wakuu baada ya kuhangaika sana nilibahatika kununua kiwanja KIBAHA Mkoani ( Low density) kama 18 years ago. Nika mjengea mama yangu mzazi kanyumba kadogo ili ajisitiri na aliishi hapo kama 17 years sasa. Na Ila pia nimeamua kumjengea kanyumba kakubwa kidogo( 3 bedrooms) ili ajinafasi zaidi sababu ya uzee wake.
Sasa mwisho wa mwaka jana ni akavamiwa na waumini wa dini ya kiislamu ambao walivamia hilo eneo na kumega sehemu ya mbele ya kiwanja na kuanza ujenzi haraka sana wa msikiti!. Kuniambia hivyo mimi na sister wangu mkubwa tukaanza mchakamchaka kufuatilia hilo swala maana waumini wale walikuwa hawatupi maelezo ya kueleweka na walikuwa si wakarimu. Misafara ikaanza kuanzia Ardhi, serikali za mitaa, wilayani, mkoani mpaka mahakamani!..
By the way kiwanja kina kila kitu na nyumba zinalipiwa ada ya jengo kila mwaka na ramani zote ninazo za nyumba na mtaa. Ila baada ya muda kama kati ya mwaka jana ilitoka order ya wao kusitisha ujenzi maana wamevamia hapo ni baada ya kuhangaika sana! maana maafisa wa ardhi walikuwa wanatuzungusha sana. Baada ya hapo roho ikatulia na lakini hawakuja kubomoa msingi uliojaa zege mpaka last week waliporudi tena na kasi mpya na kuanza kujenga tena. Kuwauliza wanasema wamepata kibali cha ikulu, kitu ambacho mimi binafsi kinanichanganya kama ni kweli na naomba isiwe kweli maana nitafedheheka sana.
Na leo hii kwenda Ardhi cha kushangaza docs zote za kiwanja hazionekani yaani zimetoweka na wakati kati kati ya mwaka jana zote zilikuwapo na nimepatwa na mshituko mkubwa mno! At this point sielewi nianzie wapi tena maana nachanganyikiwa na utesaji kwa kweli na kila kitu ktk hii nchi! Wakuu naomba ushauri wenu wenye mwanga! huyu bi mkubwa presha isije ikamuondoa. Nini nikifanye sasa ili haki itendeke!? sasa siamini vyombo maana naona kuna kitu kinatendeka underground! Please ktk michango naomba tuheshimu dini ya mwenzako na toa mchango wako bila kutukana au kudhihaki dini tafadhali,. Ahsanteni!
Kama inavyoonekana ktk picha hapo mbele ni msikiti uliomega kiwanya na unajengwa ktk barabara.