Mradi Stigler's Gorge haujawahi kusimama na hautasimama

Apr 4, 2020
16
7
Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani amewaondoa hofu Watanzania kuwa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya mto Rufiji wa Julius Nyerere haujawahi kusimama na hautasimama kabla ya kukamilika, kama iinavyodaiwa na baadhi ya watu.

1586156910992.png
Na kwamba mvua zinazonyesha katika maeneo mbalimbali nchini pia hazijaathiri shughuli zozote za mradi huo uliokwishakamilisha kazi zake kwa zaidi ya asilimia 78. Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri Kalemani baada ya kutembelea kwa mara ya 11 mradi huo na kujionea shughuli mbalimbali zinazoendelea na kueleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi ambapo akamuagiza Msimamizi wa Ujenzi huo shirika la Umeme Tanesco na mkandarasi anayejenga mradi huo kuhakikisha barabara zote za ndani na nje ya mradi zilizo ndani ya mkataba zinakarabatiwa na kupitika wakati wote.

Akabainisha msisitizo mkubwa kuhakikisha unafanywa kwa makalavati na madaraja ili mizigo iweze kupita bila mashaka yeyote na kwamba eneo la Fuga la kushusha mizigo kwa njia yaTreni limekuwa msaada mkubwa kwa kubeba vifaa na mizigo ya mradi huo wa Umeme na eneo hilo limekuwa ni roho ya mradi huo kwa sasa. Kalemani ametoa wito kwa Shirika la Reli Tazara kuendelea kushirikiana na Shirika la Umeme nchini(Tanesco) pamoja na TECU kusimamia vizuri njia hiyo.


1586156960117.png

Aidha amewataka Wakala wa Barabara nchini TANROADS kuanza mara moja ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya kutoka stesheni ya fuga hadi eneo la mradi ya kilometa 35.8 ili kusaidia uletaji wa vifaa vizito eneo la mradi.

Katika ziara hiyo, Waziri Kalemani ameyatembelea maeneo matano katika mradi huo ikiwemo eneo la njia ya kufua Umeme, Eneo la kuhifadhi maji yatakayokwenda kwenye mtambo wa kuzalisha umeme, eneo la kusaga kokoto za mradi na Mtambo wa kufua Umeme utakaokuwa na mashine tisa kwaajili ya shughuli hiyo, akamtaka Mkandarasi kuhakikisha kazi hizo zinakamilika ndani ya muda uliopangwa na kwa wakati.


1586157019278.png

1586157039320.png
1586157059740.png

1586157077380.png


Katika hatua nyingine Kalemani ameeleza kuwa hivi karibuni amelazimika kurudisha nondo tani zaidi ya elfu mbili zilizoletwa na mkandarasi wa ujenzi huo toka nje ya nchi na kusisitiza malighafi na vifaa vyote vinavyopatikana nchini kuagizwa ndani ya nchi ikiwemo saruji, nondo,bati na vyakula.
 
Huyo mkandarasi hakupewa masharti ya mkataba kuwa materials zote anunue nchini?
Kama alipewa na amekaidi kwa nini mkataba usivunjwe?
Au kuna siasa na kutafuta kiki kusema kwamba zaidi ya tani elfu mbili za nondo zimerudishwa??
 
Maendeleo Kwanza1,
Amerudisha nondo? Kwa sababu tu hazitoki nchini? Nondo nyingi zinazotengenezwa nchini hazikidhi kiwango na bei zake ziko juu mno. Aidha, uwezo wa viwanda vyetu kutosheleza mahitaji ya mradi huu pamoja na miradi mingine mikubwa inayoendelea ni wa kutilia shaka. Hivi boma liki fail na sababu ikionekana ni quality mbovu ya vifaa tutakimbilia wapi?

Hakuna Mkandarasi anaetaka hasara kwa hiyo kama hivyo vifaa vingekuwa vinapatikana kwa viwango vinavyotakiwa, bei inayolipa, idadi ya kutosha na kwa muda muafaka wangevinunua nchini. Tusiingize siasa kwenye mambo mengine.

Amandla.......
 
Maendeleo Kwanza1,
Usicheze na wapiga polishi na wachoma mishikaki hapa walipo wanafikiria jinsi gani watupake corona, ili wapate cha kusema rejea issue ya mgonjwa moja ambaye hakutaka kujitenga na Familia na jamii pia
 
Nadhani kwenye hili wamemnukuu vibaya huyu Mheshimiwa. Haingii akilini kuwa alirudisha mzigo wa nondo ulioishafika na kulipiwa badala ya kusema utumike ila wasiagize tena kutoka nje.

Kama amewaambia warudishe basi amempa mwanya Mkandarasi kuomba nyongeza ya muda pamoja na gharama zinazotokana na ucheleweshaji huo. Kwa hizi picha, huu mradi haujafika hata asilimia 50, acha 78.

Amandla.....
 
Amerudisha nondo? Kwa sababu tu hazitoki nchini? Nondo nyingi zinazotengenezwa nchini hazikidhi kiwango na bei zake ziko juu mno. Aidha, uwezo wa viwanda vyetu kutosheleza mahitaji ya mradi huu pamoja na miradi mingine mikubwa inayoendelea ni wa kutilia shaka. Hivi boma liki fail na sababu ikionekana ni quality mbovu ya vifaa tutakimbilia wapi? Hakuna Mkandarasi anaetaka hasara kwa hiyo kama hivyo vifaa vingekuwa vinapatikana kwa viwango vinavyotakiwa, bei inayolipa, idadi ya kutosha na kwa muda muafaka wangevinunua nchini. Tusiingize siasa kwenye mambo mengine.

Amandla.......

Kwa hiyo wewe ulitaka nni, viagizwe nje sio? kisha akija kiongozi wako akasema serikari aimeshindwa kujari viwanda vya ndani na ajira za watanzania pia uanze kutoa povu humu kuwa serikari haijari watu wake?

Nyie ndo watu msiojulikana maana kila upande hampo. Na haijulikani mnataka nni.
 
Kwa hiyo wewe ulitaka nni, viagizwe nje sio? kisha akija kiongozi wako akasema serikari aimeshindwa kujari viwanda vya ndani na ajira za watanzania pia uanze kutoa povu humu kuwa serikari haijari watu wake? Nyie ndo watu msiojulikana maana kila upande hampo. Na haijulikani mnataka nni.
Kajifunze kwanza kuandika

Amandla....
 
Back
Top Bottom