Mpaka leo shule za Tanzania hazifundishi watoto IT, majirani wanaonesha nia wanapewa grants kujipanua na kulamba mishahara takehome milioni 20+ majuu

gearbox

JF-Expert Member
Apr 20, 2024
244
702
Wenzetu jirani Kenya, Uganda, Rwanda wamestuka kwamba Technology is the future, hawana budget kubwa kama mbele ila si haba wanapambana wasipitwe sana, wanaandaa watoto shule za msingi kujifunza kutenegendeza programs, mifumo ya computer, robots, n.k. mtoto anajengewa msingi imara kuvijua vitu mapema sio mpaka aanze kwenda chuoni

Ukija hapa kwetu darasa la computer ni mambo yale yale ya zamani how to switch off computer, double click, n.k.

Wenzetu wameonesha nia wanapewa funds kujipanua, Kuna hubs / kambi kibao za vijana wenye interest na mambo haya kukutana hii inapelekea haya mashirika ya nje kuwasaidia kifedha kufanya projects,

majirani wanapewa uzito kuzidi sisi kwenye scholarships za kwenda kusoma mamcho ya IT huko majuu maana hata vyuo vinaona wana jitihada kutuzidi, mtu anaomba scholarship anaonesha kaanza kujifunza programming tangu shule ya msingi. wakipaata magamba huko majuu hupata kazi makampuni makubwa kama Google, Microsoft, Facebook, n.k. Mishahara milioni 20+ kila mwezi baada ya makato

USHAURI:

Bajeti ya mwaka kwa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ni Trilioni 1.6,

Shilingi Bilioni 5 ikitengwa inaweza kuleta walimu zaidi ya 130 kutoka nchi za nje kama India na kuwalipa mishahara ya milioni 3 kila mwezi kwa mwaka mzima, katika hao walimu wanaweza kusambazwa wanne kila shule kwenye shule 30 zinazotumia mitaala ya kiingereza.
 
Wenzetu wamekuja na idea ya science projects. Hapa wanafunzi wanakuja na uvumbuzi. Kisha wanaandika procedures from step 1 hadi ya mwisho kuufafanua uvumbuzi wako. Kwenye hizi projects, wanafunzi hupresent mbele ya lectures na kupewa marks. Hizi science spheres huanza kwa level ya kata, wilaya, mkoa, kitaifa, kanda then kimataifa. Nimeshuhudia hili. Kweli kwa Wenzetu, wanafunzi hufunzwa katika angles zooote. Kusoma hadi raha. Sisi uku kusoma ni kujinyima na kuteseka.
 
Umeandika kitu cha maana sana. Tatizo la kwanza kabisa ni lugha ukiachana na mazingira ya kujifunzia na ukosefu wa walimu. Huwezi kusoma programming kwa Kiswahili.
Kuna english mediums kibao tu zikiwemo za serikali

Kuhusu walimu ni suala la kuelewana mishahara unaweza kuwalata hata wahindi

Bilioni 1 pekee ambayo ni tone kwenye bajeti ya elimu inaweza kutengwa kulipa walimu 40 shilingi milioni 2 kila mwezi kwa mwaka mzima, zitafutwe hata shule 20 tu kila shule kuwe na walimu wawili mambo ya IT.
 
Mfumo wetu wa elimu ni WA hovyo sana ndiyo maana huwezi kumuona moto wa wazuri,rais ,mkuuwa wilaya&mkoa,mkurugenzi au yeyote mwenye uwezo akahangaika mwanae asome hizi shule.Maana wanajua kabisa hizi shule hamna kitu.kwa ulaya mototo yeyote wa kiongozi au masikini wanasoma shule za serikali wengi tu Kwa kuwa shule zao wameziboreshwa sana.kama unakaa mpakani ni Bora watoto wakasomea nje ya Nchi zinazotuzunguka kuliko kupata makapi ya elimu ya hapa Tanzania
 
Lugha siyo tatizo
Kama unashindwa kujifunza kwa sababu ya lugha ujue uwezo wako ni mdogo
Kwa watumiaji wa kiswahili, lugha ni tatizo mana mifumo haijatengenezwa kwa lugha ya kiswahili. Mataifa yaliyoendelea kama China na Russia wao wana mifumo yao ambayo inatumia lugha zao.
 
Hamna haya kufundisa watoto IT. Watoto wafundiswe matumizi ya bidhaa za IT (software, matumuzi ya computer etc)


Class 1 - 7 wasome basic, secondary wasome advance ( script language). Adavnce wasome core programming (baadhi ya shule zinafundisha)


IT sio programming tu, kuna vitu vingi ndani yake.


Niianza kujifunza programming HS
 
Uliziona tahasusi (combinations) mpya za kidato cha sita zilizopendekezwa? Nyingi zinahusu mambo ya dini (Islamic Studies na Divinity). Hapo unategemea nini?

Acha tushabikie Simba na Yanga angalau 😁😁🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️

IMG-20240410-WA0160.jpg
 
Back
Top Bottom