Mdude_Nyagali
Member
- Dec 11, 2022
- 62
- 1,246
Tayari DP World wameshachukua udhibiti wa bandari ambayo ni urithi wetu kutoka kwa Mungu.
1. Mpaka sasa Rais hajaweka wazi Tanzania itapata Tsh. ngapi kwa mwezi kupitia mapato ya bandari ambayo kuanzia sasa yatakusanywa na DP World kama taarifa ya TPA niliyoambatanisha hapa inavyoeleza.
2. Kwamba hapo awali mapato yetu pale bandarini yalikuwa wazi ila kwa sasa yatakuwa siri kati ya DP World na Samia.
3. Pamoja na uboreshaji wa bandari hizo kupitia pesa zetu na mkopo kutoka WB bado Samia na serikali yake hawajaweka wazi kwamba hao DP World wamewekeza kiasi gani zaidi ya kuja kuvuna shamba ambalo tumelilima kwa jasho na damu kwa ajili ya watoto wa Tanganyika na Tanzania.
4. Mpaka sasa Samia na serikali yake wamekataa kuweka wazi mikataba ya kukabidhi bandari hizo kwa waarabu wa DP World. Tunaambiwa ni uwekezaji lakini hatuoneshwi mikataba hiyo ili tuipitie tuone kama uwekezaji huo una faida au hasara.
Samia anapaswa kupingwa na kila mtu mwenye akili timamu na mzalendo wa taifa hili. Sisi hatuna nchi nyingine isipokuwa hii Tanganyika aliyotupa Mungu. Sasa kama Samia atakuwa anaendelea kuingia mikataba ya siri na mibovu ya kuuza rasilimali nitakuwa tayari kwa lolote kulinda rasilimali na ardhi ya nchi yetu.
Mungu bariki Tanganyika.
Mungu bariki Zanzibar.
Mungu bariki Tanzania.
Mdude Mpaluka Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.