Mokwena: Tunaiheshimu Yanga. Kwa watu waelewa hii kauli ni mbaya

Tariq f

JF-Expert Member
Dec 11, 2021
233
345
Habari wakuu,

Tuanzie hapa,
" Haina maana ya kufanya defense, mpira ni mchezo wa burudani inayovutia mashabiki. Tunaenda kucheza mpira kama ilivyo kawaida yetu. Tunaiheshimu Yanga, hivyo tutahakikisha tunakuwa vizuri ili kukabiliana nao bila kufanya mabadiliko yeyote makubwa."
Kocha wa Mamelodi Sundowns ( Rulani Makwena)

Hayo ni maneno ya Kocha wa wababe toka Africa kusini Mamelodi Sundowns ( Masandawana ) kuelekea mchezo wao dhidi ya Dar Young Africans panapo March 30.

Bila kusahau kwenye ulimwengu wa Soka hii ni kauli mbaya sana kwa Yanga iliyotolewa na mpinzani wake huyo. Mpinzani anapokuheshimu ina maana anaenda kukuwekea silaha zote za mauaji tayari kwa vita na hataki kukuletea utani.

Bila shaka Yanga inatakiwa kuwa makini sana kuelekea mtanange huu, hii ni baada ya kila dalili mbaya kuonekana upande wao.

11328111-1683909721.jpg
 
We kenge kuna mtu anaenda vitani asipeleke siraha zake zote?. Kwa hiyo kama kauli yake ni mbaya kwa hiyo wewe umekuja kumsemea unamtisha nani? YANGA? Halafu ukimtisha YANGA,afanyeje? Asiende kucheza?.
Mikia mna matatizo. Kwa akili zenu mnatamani mkamchezee nyie YANGA,ili mupigwe hata 5. Huyo unaemsemea nakutuma tena nenda kamwambie alete timu uwanjani. Vitisho havina nafasi. Mpira ni dakika 90 uwanjani
 
Mamelodi huwa wanafungika nyi msiojua mpira wakicheza na hao Petro tu huwa wanasumbuka mno mno Mvala anaishia kula red card kwa kufanya faulo huku akiwa mchezaji wa Mwisho...beki za kati za Mamelodi zikipata kashikashi zinamtegemea Williams ndio awasaidie..Mamelodi wapo vizuri beki zote za kulia na kushoto pamoja na viungo wao na hao washambuliaji wao ila beki yao ina utata kidogo ni wakina Key wafunguke tu wale wanafungika ingawaje Mpira utachezwa kweli hapo daslm...
 
Habari wakuu,

Tuanzie hapa,
" Haina maana ya kufanya defense, mpira ni mchezo wa burudani inayovutia mashabiki. Tunaenda kucheza mpira kama ilivyo kawaida yetu,
Tunaiheshimu Yanga, hivyo tutahakikisha tunakuwa vizuri ili kukabiliana nao bila kufanya mabadiliko yeyote makubwa."
Kocha wa Mamelodi Sundowns ( Rulani Makwena)

Hayo ni maneno ya Kocha wa wababe toka Africa kusini Mamelodi Sundowns ( Masandawana ) kuelekea mchezo wao dhidi ya Dar Young Africans panapo March 30.

Bila kusahau kwenye ulimwengu wa Soka hii ni kauli mbaya sana kwa Yanga iliyotolewa na mpinzani wake huyo.
Mpinzani anapokuheshimu ina maana anaenda kukuwekea silaha zote za mauaji tayari kwa vita na hataki kukuletea utani.
Bila shaka Yanga inatakiwa kuwa makini sana kuelekea mtanange huu, hii ni baada ya kila dalili mbaya kuonekana upande wao.View attachment 2944908
Ndugu waache hao vyura.Watakusingizia umewaponza.Cheki komenti zao sasa!🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ila u mbumbumbu ni kipaji, kwaiyo ulitaka kocha wa Mamelodi asemaje!!, ulitaka aseme hatowaheshimu wapinzani?

Si jajua ukiwa mbumbumbu unafiriki kwakutumia kiungo gani cha mwili!!
 
Mamelodi anawatisha watu ambao hawaujui mpira wa africa ukoje.

mazembe tu ya mwaka huu iliyojichokea kamtoa jasho mamelodi agreggate 1 - 1 mechi 2. na hapo mamelodi kapewa penalty
Kaka Mazembe ya msimu huu imechoka tuache ushabiki kikubwa tujiandae naamini Yanga kumfunga hapa Mamelod sio swala la kuuliza Kwa ninavyojua fitna za Mpira wa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom