MO na GSM wako kimya suala bandari Rostam amewawakilisha

Rege

Senior Member
Jul 9, 2022
113
142
Kuna mjadala nimeukuta mahali watu wanahoji kwanini Mfanyabiashara Maarufu Mohamed Dewji maarufu MO na Mfanyabashiara Maarufu Gharib Mohamed Maarufu GSM ambao ndiyo wadau wakubwa wa bandari kuingiza mizigo nchini kwamba mbona hawajasema chochote kuhusu mjadala wa DP Wold kuhusu Bandari.

Mimi nadhani Rostam Aziz ameshaongea kwa niaba ya wafanyabishara sidhani kama kuna ulazima Mo Dewji na GSM nao waitishe Press kuzungumzia bandari, sidhani. vinginevyo kama wataona inafaa labda kwa kuhojiwa na vyombo vya habari ili kupata mtazamo wao kuhusu uwekezaji huo.


mo-e1540004637141-804x607.jpg

Mohamed Dewji MO


gsm-pic-data.jpg

Gharib Said Mohamed GSM

Rostamaziz.jpg

Rostam Aziz
 
Mo na GSM wana akili, hili pekee ndio jibu, Rostam ana pesa sawa ila akili zake zina shida, kina Mo hata kama wana support ila hawawezi kutaka kuonekana vilaza
 
Kwanini mbona Rostam amezungumza
Rostam kafanya sana siasa anaijuwa CCM vizuri sana ila kama unakumbuka kwenye ile sherehe ya Yanga kama sikosei Rais Samia alitupa kijembe kwa GSM kuwa nakuachiachia mambo yako yaende najuwa na wewe unafanya nini, hapo utajuwa Rais anajuwa kila kitu ni ile funika mwana haramu apite.
 
Tujitahidi pia kiuchumi angalau wazawa nao wawe na nguvu ya kushika rasilimali za nchi mkuu

Ova
Mzawa aliyetutoa kimasomaso ni marehemu Mengi ajabu hao weupe waliwatumia wanasiasa wetu kumdidimiza,waafrika jamii ya hovyo sana!
 
Back
Top Bottom