Mlango Unaojifungua Wenyewe Katika Kitabu Cha Mzee Mwinyi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,058
30,401
MLANGO UNAOJIFUNGUA KATIKA KITABU CHA MZEE MWINYI

Mzee Mwinyi Mashaallah hodari wa kuchekesha.

Katika kitabu chake, "Mzee Rukhsa..." anahadithia alivyokuwa mwanafunzi Uingereza alivyoshtuka kuona mlango anaotaka kuufungua ukijifungua wenyewe hata hajaushika wala kuufikia.

Nami naweka hapo chini mkasa wangu:

"Nilikuwa Glasgow Scotland mwaka wa 1991 nimekwenda kumtembelea kaka yangu akisomesha University of Glasgow.

London nimepita wima nimepanda bus Liverpool Coach Station kuja Glasgow, Uskochi.

Ikanijia hamu nikiwa Glasgow kwenda Edinburgh nikaone chuo alichosoma Mwalimu Nyerere.

Ndani ya behewa tuko abiria kiasi cha watano mtu mweusi mie peke yangu.

Nimeingia msalani.
Nimemaliza haja.

Nikiwa nimekaa naangalia flush nivute nisafishe choo ndiyo ninyanyuke nikiwa msafi.

Sioni kitu.
Kila ninapotupa jicho sioni kitu.

Hofu kubwa imeniingia.
Nitatokaje msalani nipaache pachafu?

Abiria mwengine akiingia si atasema choo kachafua huyu Mwafrika?
Nikawa nimepwelewa.

Lakini nitakaa msalani naogopa kutoka mpaka lini?
Nisubiri hadi siku ya kiama?

Nikanyanyuka kusimama.
Nasikia maji yanatiririka kwa mvumo na kishindo choo kinajisafisha.

Hii ndiyo "cultural shock," inayowakumba wengi wanapofika Dunia ya Kwanza wakitokea Dunia ya Tatu.

Mikasa mfano wa huu ulionifika mimi iko mingi na ya kila aina."

1709495922187.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom