Mkuu wa Mkoa Arusha Paul Makonda: Kiongozi Mzima Kujieleza Hujui, Mnapataje Hizi Nafasi TARURA?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
44,688
51,554
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paulo Makonda amemshangaa Meneja wa TARURA Mkoa wa Arusha Kwa Kushindwa kutoa maelezo yanayoeleweka hujisu utendaji kazi wa taasisi yake katika Kuhudumia Barabara.

Bwana Makonda amepigwa na Butwaa na kuhoji watu wasioweza kujieleza na wanaojiita Wasomi inakuaje wanapata vyeo husika?

View: https://youtu.be/nr2JCzzytU4?si=ciVZZOnhK0uNFmYn

My Take
Naunga mkono hoja.

Hawa wamesoma communication skills Toka Wakiwa Sekondari Hadi vyuoni,inakuaje washindwenkujieleza? Mbona wengine wanaweza jieleza?

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemshukia vikali Meneja wa TARURA Mkoa wa Arusha, Lainas Sanya kuhusu kazi ya TARURA na barabara wanazozisimamia na kueleza kwamba kama hata kujieleza hawezi alipataje nafasi hiyo?

 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paulo Makonda amemshangaa Meneja wa TARURA Mkoa wa Arusha Kwa Kushindwa kutoa maelezo yanayoeleweka hujisu utendaji kazi wa taasisi yake katika Kuhudumia Barabara.
Kwani yeye Bashite anajuwa nini kwani? Yaani mtu aliyefoji cheti cha Paul C makonda leo anaponda watu wenye elimu zao!! Ila sishangai hiyo ni kawaida ya mijitu bogus kuponda waliosoma.
 
Kuzungumza ni kipaji ndugu yangu .kasome hata habari za Musa na haruna na alichosema Mungu juu ya mtu kuzungumza mbele za watu. Wengine ni watendaji wazuri ila ukimwambia azungumze unaweza hata muonea huruma. Kikubwa aangalie na kuzingatia utendaji kazi na utekelezaji wa majukumu yao. Kikubwa ni kuwaelewa vyema watumishi walio chini yako na namna walivyo na kujaribu kuwajengea uwezo na kujiamini.
 
Sasa amewezaje kuwa kiongozi tena meneja wa mkoa halafu kujieleza hajui anawaongoza vipi watu wake bila kujua kujieleza kwa ufasaha?Kama kazi yake ni ya utendaji kwa mikono yake kwenye saiti ya kazi hapo hakuna tatizo tutaangalia tu alichokitengeneza saiti.
Meneja wa mkoa?huoni kwamba alipachikwa tu na mtu fulani hata bila interview,ni aibu hii
 
Back
Top Bottom