Mkurugenzi wa Habari Ndugu Mobhare Matinyi amka uongeze speed ofisi yako imepoa sana kuelekea uchaguzi

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
926
4,343
Mobhare Matinyi nipo hapa kukumbusha majukumu yako ila siyo kushurutisha ukafanye kwa mbinu gani. Napenda kukumbusha kwamba wananchi wanasema ofisi yako haina mchakamchaka wa ubunifu kuelekea uchaguzi. Ofisi imekaa kimya kama wizara ya mambo ya Nje. Hapana changamsha nchi kwa makala na habari sisimuzi kuhusu utendaji wa serikali

Sijaja kukumbusha kazi ila nimekuja kukuwazisha uone ni wapi unafanya vizuri na wapi ufanyi vizuri. Apparently, upepo wa kisiasa umeongezeka na miundombinu imeharibika sana kwa mvua. Wenzenu wanaokosoa serikali wapo kazini wakitembea kwenye shida za wananchi na kuzipigia kelele. Amsha maafisa habari wakafanye kazi yao.

Bunge linaendelea lakini ni kama vile hakuna bunge ; si suala zuri sana kiafya ya uchumi na kisiasa. Waulize wenzako katika Muhimili wa nne kwanini bunge limekosa mvuto mtaani? Kwanini matangazo ya bunge yamesusiwa? Kama na wizara ya habari mjiulize lakini kusanyeni maoni ya wananchi na kufahamu wanachotaka

Mwisho; ni hatari kisiasa kuwa na jamii iliyokinai habari za serikali. Lazima urudishe morali ya jamii kuangalia na kufuatilia habari za serikali . Tengenezen hata midahalo ya kimkakati itakayovuta hisia.....oohooo sory; sitaki kukupa mbinu nafahamu unazo nyingi
 
Nchi hii haina UCHAGUZI bali ina UCHAFUZI huwezi kusema una UCHAGUZI wakati Mmoja wa WAGOMBEA ndio Anateua WASIMAMIZI wa Uchaguzi Anawalipa Mishahara na Posho.
Huwezi kusema kuna Uchaguzi wakati Tume ya UCHAGUZI sio huru Wajumbe wake Wanateuliwa na mmoja wa wagombea URAIS na ndiye anawalipa Mishahara
Ili TANZANIA iwe na UCHAGUZI ni LAZIMA tuwe na TUME huru ya UCHAGUZI Wajumbe waka Wasitokane na TEUZI la mmoja wa Wagombea Urais
Pia tuwe na KATIBA MPYA.
 
Back
Top Bottom