Hagwila
Member
- Apr 18, 2019
- 80
- 97
Jana tarehe 25/1/2022 wazazi wenye watoto Shule ya Msingi Magu walikuwa na kikao ambacho kiliitishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Shule kwa taarifa kupitia kwa watoto.
Kikao kilihudhuriwa na wazazi wengi (japo siyo wote); lakini mwitikio ulikuwa wenye kuridhisha.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mhe. Diwani na Afisa Mtendaji wa kata ya Magu mjini.
Mengi yalizungumzwa kwa mujibu wa agenda zilizokuwepo; na kwa ufupi mengi yalikwenda vizuri isipokuwa mawili matatu ambayo hayakuafikiwa.
Moja ya masuala ambalo lilikuwa mwiba wa kikao hicho ni kuhusu VYUMBA VITATU VYA MADARASA VILIVYOJENGWA KWA NGUVU ZA WANANCHI KUPOKWA NA MKURUGENZI MTENDAJI H/W MAGU NA KUFANYIA UMALIZIAJI (FINISHING & FURNISHING) KWA KUTUMIA FEDHA SHS MILIONI 40 ZA EP4R
Kwa faida ya wote, EP4R ni kifupi cha Education Program for Results. Hii program inafadhiliwa na Benki ya Dunia (WB), ambapo fedha kwa ajili ya maendeleo ya shule (kupitia mfumo wa fedha wa kiserikali), zinaelekezwa moja kwa moja kwenye eneo husika ili kuepusha uchepushaji.
Shule nyingi zimenufaika na program hii ikiwa ni pamoja na urekebishaji wa ikama (idadi ya waalimu vituoni), ujenzi wa vyumba vya madarasa, vyoo vya wanafunzi na waalimu n.k.
Kwa bajeti ya EP4R, chumba kimoja cha darasa lililokamilika kuanzia ujenzi mpaka kuweka madawati ni Tshs milioni 20, hivyo kwa vyumba viwili vya madarasa Shule ya Msingi Magu zililetwa Tshs milioni 40 ambazo zilikadiriwa kukamilisha ujenzi wa vyumba hivyo viwili vya madarasa mpaka kuweka madawati.
CHA KUSHANGAZA, baada ya fedha hizo milioni 40 kupokelewa, badala ya kujengwa madarasa mapya mawili, Mwalimu Mkuu aliyekuwepo wakati ule Mary Maganga kwa kushirikiana na viongozi wa ofisi ya Elimu (W) Magu pamoja na DED aliyekuwepo wakati huo Lutengano Mwalwiba akishauriwa na Mhandisi wa wilaya ya Magu, waliamua kutumia fedha hizo za EP4R milioni 40 kumalizia vyumba viwili vya madarasa kati ya vyumba vitatu ambavyo tayari vilikuwa vimejengwa KWA NGUVU NA MICHANGO YA WANANCHI KWA 100% mpaka hatua ya kukamilika kwa maboma.
Walibomoa kona mbili na ukuta wa upande mmoja, wakaongeza upana kidogo, wakapunguza idadi ya madirisha, wakaongeza pavement, wakapiga lipu, wakaweka tiles, wakapaua, wakapiga rangi, wakaweka milango na madirisha; milioni 40 kwisha!!😮😮
Hayo yakifanyika, Mwalimu Mkuu aliiweka pembeni Kamati ya Shule, akawa anafanya kazi ya kusimamia mafundi mwenyewe na baadhi ya waalimu wake, huku akipata backup ya ofisi ya Elimu (W) na ofisi ya DED Magu, hususani Mhandisi wa wilaya; na baada ya kumaliza kazi hiyo, madarasa hayo mawili yakaandikwa "DONATED BY EP4R 2021"
Huo ni wizi wa kimachomacho, ambao umefanywa na huyo Mwalimu Mkuu aliyekuwepo kwa kushirikiana na viongozi wa wilaya wa idara ya Elimu na ofisi kuu ya DED Magu.
Diwani wa Kata ya Magu mjini Mhe. Mashaka amelipambania sana suala hili, maana nguvu za wananchi wake zimepokwa na hao niliowataja hapo juu; wametumia kiasi kidogo cha pesa kupoka kazi ya wananchi, badala ya kuanzisha kazi yao mpya kwa pesa ambazo walipokea kama utaratibu wa EP4R unavyoelekeza.
Darasa moja limetelekezwa kati ya hayo matatu.
Jana kikao cha wazazi kimempa DED Magu siku 7 akamilishe umaliziaji wa darasa hilo.
Tunajua DED aliyeko Magu sasa siye aliyekuwepo wakati madudu haya yakifanyika; lakini kwa sababu hiyo ni kazi ya kiofisi ni lazima achukue hatua, bila kujali mtangulizi wake alijikoroga vipi.
Tunajua pia kwamba TAKUKURU Magu wanachunguza suala hilo; lakini pamoja na uchunguzi huo ukiendelea, ni lazima DED Magu achukue hatua ili kuepuka kuwavunja moyo wananchi.
Lakini pia, mamlaka zinazohusika na uchunguzi huo wakiwemo TAKUKURU na Wakaguzi wa OR TAMISEMI ambao walifika kuangalia hali halisi na kubaini kwamba ni kweli wahusika ambao wote ni watumishi wa umma akiwemo Mwalimu Mkuu aliyekuwepo (Mary Maganga) na baadhi ya watumishi wengine wa idara ya Elimu na ofisi kuu ya DED Magu, ni lazima wawajibishwe.
Madudu ni mengi sana ofisi ya Elimu Magu, lakini kwa leo niishie tu hapa. Povu ruksa!!😏