Mkumbushe Mjomba Wako wa Miaka ya 80 Asikariri Misemo Nyakati Zinabadilika

Sweya Makungu

JF-Expert Member
Jun 11, 2023
481
560
Mkumbushe Mjomba Wako wa Miaka ya 80 Asikariri Misemo, Nyakati Zinabadilika.

Ule Msemo wa 'Nyumba ni Choo', Wapangaji Wanauzingatia Kuliko Mwenye Nyumba.
💫💫💫💫💫
© Mwl. Makungu Ms
0743781910

Binamu, mwambie mjomba kuwa, misemo yao siyo ya kwetu. Maana nyakati zao ziliishia kwao hazipo tena kwetu.

Mwambie mjomba awaambie wazee wenzake kuwa , Mliokuwa mnatusema tutakufa na kilo mbili, siku hizi tunakufa na kilo 80 na tunapendeza kuliko nyinyi. Asikariri misemo, zama zinabadilika.

Mdokeze mjomba wako, kijiwe cha miaka ya 90 siyo kijiwe cha miaka ya 2000. Pale tulipokuwa tunapaita kijiwe kama mahali pa kupotezea muda kupiga stori ,siku hizi ni kijiwe cha kujipatia riziki. Siku hizi vijiwe ni ofisi za watu. Mwambie hata kijiwe cha kahawa ni biashara ya mtu. Kwahiyo asidharau vijana wa vijiweni.

Mwambie mjomba wako, ulokole siku hizi siyo jina la utani bali ni utambulisho kamili. Yale aliyokuwa anayaita makanisa ya kilokole kama jina la utani miaka ya 90 siku hizi yanaitwa makanisa ya kiroho. Tena mwambie ulokole wa siku hizi umepiga hatua. Wale walokole waliokuwa wanaonekana kama wamechanganyikiwa, siku hizi ni kimbilio la wasomi na wote wenye matatizo.

Mkumbushe mjomba asikariri misemo. Mwambie kuwa, ule msemo wa watu wazima wa miaka yao "ponda mali kufa kwaja" , siku hizi ni msemo wa vijana na wameubadilisha wanasema "maisha yenyewe mafupi niache nife na ujana. Nakesha kama popo nakula ujana". Sasa sijajua kama ni wao ndiyo wanakula ujana au ujana ndiyo unawala wao!

Mwambie mjomba asikariri misemo mambo yanabadilika. Mwambie matumizi ya ugolo siku hizi siyo kilevi cha mabibi kizee na wanawake wasio na hamu ya tendo la ndoa. Siku hizi ugolo ni kilevi cha vijana tena wa kiume.

Mwambie mjomba wako kuwa, misemo mingine ya zamani ilikuwa ni kama misemo ya watu waliojikatia tamaa, kwahiyo imepoteza uhalisia na maana. Kusema "aliyeko juu mngoje chini" ilikuwa ni kama ushirikina wa kuombeana mabaya. Ni nani aliwaambia watu wa zamani kila aliyeko juu lazima atafeli arudi chini?
Siku hizi hatuwangoji chini, tunapambana kuwafata huko huko juu.

Mwambie mjomba kuwa ule msemo wa "angalia utaokota makopo" siku hizi hauna maana. Siku hizi hata vichaa wenyewe hawaokoti makopo maana makopo ya kuokota hayapo. Kuokota makopo siyo ukichaa tena bali ni ajira za watu.

Mkumbushe mjomba kuwa ule msemo wa "subiri , kuwa mwaminifu, ukishindwa tumia kinga" tuliishausahau. Siku hizi ukishamtumia na ya kutolea, mnatumiana halafu ndiyo mnatumia kinga. Yaani siku hizi hatuogopi ukimwi tunaogopa mimba. Kwahiyo kinga ni baada ya matumizi ndiyo maana vidonge vya p2 vinaisha madukani.

Mnong'oneze mjomba wako awe makini, maana jinsi ukimwi ulivyotulia utasema haupo. Mwambie kama watu tulioathirika tutakosa mioyo ya upendo , basi dawa zinazotusaidia kupunguza makali ya ukimwi zitakuwa ndiyo dawa zinazotusaidia kuongeza maambukizi ya ukimwi kwa kasi zaidi. Maana jinsi ukimwi ulivyotulia, utadhani haupo.

Mwambie mjomba akija mjini asishangae sana mambo yamebadilika. Wale aliokuwa anawaita mama ntilie hawapo tena kuna mama lishe. Mwambie machangudoa waliisha, kuna madada poa. Na ili kupunguza ukali wa maneno, malaya tunawaita viswaswadu na wanaojiuza wanajiita wadangaji.

Mwambie mjomba zama zimebadilika, siyo kama zamani. Ule msemo wao wa 'mama huruma, soya maharage ya mbeya, maji mara moja, hata hauwezi kufanya kazi tena. Siku hizi ni ngumu sana kutofautisha kati ya mwanamke mgumu na mwepesi. Maana kwa wengi japo siyo wote, mahusiano yamekuwa ni kama fasheni tu. Leo anavaa gauni kesho jeans. Tumejuana leo tumepatana leo tumalizane leo. Ukimuacha asubuhi jioni kashapata mwingine na anapita naye mtaani.

Mwambie mjomba asilete mambo yake ya kizamani atakamatwa na serikali. Siku hizi hatuwafukuzi mabinti waliopatia ujauzito nyumbani. Tunawatia moyo wajipange kuendelea na maisha maana hata wanaume wenyewe wa kuoa hawapatikani. Kwahiyo kuzalia nyumbani siku hizi imekuwa siyo aibu wala laana bali ni kawaida ya jamii kwenda na wakati.

Mwambie mjomba wako, alimnukuu vibaya mrisho mpoto. Ule msemo wa "nyumba ni choo" ili kuboresha makazi ya watu, vijana wameupotosha kwa sababu ya tamaa zao za mwili. Wanasababisha madada zetu kujiongezea shepu.

Mwambie mjomba wako aliyeko basata na wizara ya sanaa, ule msemo wa sanaa ni kioo cha jamii waubadilishe hauna maana tena. Siku hizi sanaa siyo kioo cha jamii bali kichocheo cha jamii. Badala ya kuonesha mambo yaliyopo kwenye jamii, wao wanatuletea mambo mapya ya hovyo na kuichochea jamii iwaige kuyafanya. Wanatuharibia kizazi kwa tamaa zao za kijinga.

Mwambie mjomba, Ule msemo wa "tajiri na mali zake maskini na wanangu" umeanza kupotea. Siku hizi habari ya mjini ni uzazi wa mpango. Zaa idadi ya watoto unayoweza kuimudu vizuri. Asijidanganye na umaskini wake kuzaa watoto wengi asioweza kuwamudu matokeo yake ni kuwarithisha shida na njaa na kuwaingiza katika mnyororo wa umaskini.

Mwambie mjomba asikariri mambo asije kugombana na wapwa zake bure. Mkumbushe kuwa ule msemo wa "kuolewa ni sheria kuzaa ni majaliwa" umeanza kupotea masikioni. Siku hizi siyo tu kuzaa ni majaliwa, bali kuolewa pia ndiyo imekuwa zaidi ya majaliwa.

Mchekeshe mjomba kidogo, ule msemo wa 'ndoa ni ndoano' yaani ikinasa haiachii hautumiki tena. Siku hizi kwenye harusi wazazi wasio na hekima wana msemo 'yakikushinda rudi nyumbani haujaua'. Kwahiyo talaka ni za kufikia tu. Tunaoana jumamosi tunaachana jumapili.

Naamini mjomba akisikia hii atahuzunika sana. Mwambie kuwa ule msemo wa 'mtoto wa mwenzio ni wako' uliishia zama zao tu. Siku hizi mtoto wa mwenzio ni mkubwa mwenzako. Na ukisubiria maembe yaive wenzako wanakula na chumvi".

Mwambie mjomba mimi sina nia mbaya ya kumkumbusha ya zamani, lakini nataka ajue kuwa ule ustaarabu wa 'mpende jirani yako kama unavyojipenda' umebakia kwenye biblia tu. Zamani tuliwajua majirani zetu wote, lakini siku hizi hatujuani na tunaogopana na kinachotukutanisha ni msiba wa mtaani.

Nitashangaa sana kama mjomba bado ana mawazo ya 'mzigo mzito mpe mnyamwezi'. Mwambie maisha yamekuwa magumu mpaka wazaramo na wakwere wanapambana kariakoo sokoni badala ya vibarazani.

Mwambie mjomba, siku hizi kilimo siyo tena uti wa mgongo wa nchi yetu. Ni uti wa mgongo wa kwake na familia yake. Apambane kujikwamua na kizazi chake. Nchi ina vyanzo vingi vya kipato.

Mwambie mjomba kuwa, tulizoea kungwi mtu mzima au shangazi ndiye huwafundisha mabinti jinsi ya kuishi na mume, lakini siku hizi mabinti wadogo ndiyo wanawafundisha mashangazi jinsi ya kumuhudumia mume.

Mueleze kuwa, ukiwa mjini siku hizi hata neno lenyewe tu 'shangazi' ukilitaja linakuwa na utata. Mashangazi wamejaa kila kona na wanahitajika kweli kweli.

Msisitize mjomba akija kututembelea mjini asiwaite watu mashoga. Wale mashoga wa miaka yao siyo mashoga wa siku hizi. Ikiwezekana abaki tu kijijini..

Mwambie mjomba, tulizoea kuhubiriwa kanisani ya kuwa tukifika mbinguni tutapewa miili mipya. Siku hizi miili mipya dada zetu wanaipata uturuki india na china. Ni yeye tu na hela zake.

Mchekeshe mjomba kuwa, wakati natafuta mchumba alinishauri kuwa 'polepole ndiyo mwendo' nikajikuta nimemkosa mchumba niliyemtaka. Maana vijana wa siku hizi wajinga hawalazi damu, wanakwambia 'chelewa chelewa utakuta mwana si wako'.

Makungu Ms
0743781910
JM 4 Nov 2023
 
Usisahau kumwambia mjomba kuwa akija mjini hatamkuta tena shangazi aliyemuacha nyumbani maana wahuni mtaani wanajilia kwa zamu, mjomba ajipange upya tu kuvuta dogo dogo mpyaa.
 
Mkumbushe Mjomba Wako wa Miaka ya 80 Asikariri Misemo, Nyakati Zinabadilika.

Ule Msemo wa 'Nyumba ni Choo', Wapangaji Wanauzingatia Kuliko Mwenye Nyumba.

Mwl. Makungu Ms

Unaonekana Huna kazi ya kufanya na ni mtoto wa 2000 halafu unaishi kwa shemeji(alikoolewa dada yako)...unawezaje kuandika mambo mengi hivyo ambayo ni useless kabisa!..da!
 
Wewe umepata wapi muda wakusoma mambo useless??
 
Watu wanazihaka sana, ila mim nnae mjua makungu wala sio mtoto. Huyu ni mwalimu wa kemia pale UDSM. Sasa sijui alieandika nie yeye au ndugu yake ila nimefurah kukutana na mwalimu wangu JF hakika jF N ZAID ya mtandao.

Msemo wa Makungu ambao sijii kuusahau ni "ukuta unamasikio mjomba" hahahahah hapo ujue mshafel nusu ya darasa hahahahahabab
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom