Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,223
- 4,216
Jeshi la Polisi mkoa wa Geita linawashikilia Joyce Julius na Juma Charles (wanandoa), kwa tuhuma za kumuua mama mkwe wao Butamo Igionzela (70) ambaye ni mama mzazi wa Joyce mkazi wa Bungezi kata ya Ihanamilo wilayani Geita wakimtuhumu kumuua mtoto wao kwa njia ya kishirikina.
Akiongea na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Berthaneema Mlay amesema watuhumiwa hao wamefanya tukio hilo baada ya kuambiwa na mganga wa kienyeji kuwa mama yao alimuua mtoto wao.
Aidha Mlay ameitaka jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi badala yake watoe taarifa kwenye vituo vya Polisi ili watuhumiwa waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
=====
Watu wawili wanashikiliwa na Polisi Mkoani Geita kwa tuhuma ya kumuua kwa kumchinja Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Butamo Igonzele (70) Mkazi wa kijiji cha Bumegezi Kata ya Ihanamilo Mkoani Geita.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Berthaneema Mlayi amesema Watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya uchunguzi wa awali kuonesha wanaweza kuhusika katika mauaji hayo huku jitihada zikifanyika katika kujiridhisha kupitia uchunguzi wa awali.
Watuhumiwa hao ni Joyce Julius ambaye ni Mtoto wa Marehemu na Juma Charles ambaye ni Mkwe wa Marehemu (Mume wa Joyce) ambapo inadaiwa walikuwa wanamtuhumu Marehemu (Mama yake Joyce) kuhusika na kifo cha Mtoto wao ambaye alifariki wiki moja iliyopita huku kifo chake kikihusishwa na ushirikina.
Tukio hilo limetokea February 22, 2023 usiku katika Kijiji hicho cha Bunegezi Kata ya Ihanamilo Wilaya ya Geita Mkoani humo ambapo watuhumiwa hao wanadaiwa kumuua Mama yao.