Wakili anaingiaje hapo wakati hapo swala ni upelelezi na vidhibiti hafifu?
Walaumiwe Polisi
Tatizo watu wanachanganya haki na taaluma. Mbele ya sheria kila mtu ana haki (hata muuaji) ya kupewa Wakili wa Kumtetea. Tena Wakili anakwambia useme ukweli wa kilichotokea then baada ya hapo anatafuta weak points ili Mteja wake ashinde kesi. Kwenye kesi hii Wakili aliyekuwa anamtetea Mtuhumiwa hana shida. Tatizo lipo kwa Wapelelezi na Waendesha Mashtaka wetu. Yawezekana hawajajengewa uwezo wa kutosha wa kupambana kisheria na Mawakili Binafsi ambao ni Wabobevu.
 
Hiki ndicho kilisababisha wife agome watoto kusoma sheria! Sasa nimeshamwelewa! Kama mbingu ipo, mawakili hawataiona!

Hapana mkuu ni kuwafanya wawe waadilifu. Wasisimamie mkosaji kumnasua kwa kisingizio cha kisheria.

Kuna wanasheria wakishajua ukweli tu, wanakukataa. Hawapo tayari kutetea uovu kisa kuna uwazi wa kisheria.
 
Hiki ndicho kilisababisha wife agome watoto kusoma sheria! Sasa nimeshamwelewa! Kama mbingu ipo, mawakili hawataiona!

Wife wako hakuwa sawa.

Mimi nimesomea sheria na nimegundua mambo kadhaa.

1. Elimu ya Sheria ni fani kama zilivyo fani nyingine.

2. Baada ya udakari, fani ya sheria inafuata kwa umuhimu wake kwa jamii.

3. Kesi za jinai ni aina ya kesi ambazo mtuhumiwa ana uwezekano mkubwa kushinda.

4. Jamuhuri ndiyo huchukua jukumu la kufungua kesi za jinai dhidi ya mtuhumiwa/watuhumiwa.

5. Jamhuri ndiyo yenye mzigo mzito wa kuthibitisha mashtaka dhidi ya mtuhumiwa/watuhumiwa.

6. Mtuhumiwa anatakiwa kuonyesha shaka kwenye ushahidi wa jamuhuri na siyo kupinga.

7. Kwenye jinai, chembe kidogo ya shaka, hata kama ni tofauti ya tarehe, itamfanya mtuhumiwa kuachiwa.

8. Katika kesi ya Miriam Mrita ushahidi ulikuwa wa mazingira na siyo wa moja kwa moja, na pia hati ya mashtaka ilikosewa na hivyo kufanya watuhumiwa kukwepa adhabu.
 
Nani kakudanganya ushahidi ndio kila kitu? Ni lazima uwe na mawakili mazuri hasa kwenye mahojiano na Cross examination ya ushahidi, utetezi, exhibits kama hauwezi tetea hoja vizuri hata kama una ushahidi utaanguka. Mfano Sabaya ushahidi ulikuwepo cha ajabu kosa lilikua kwenye aina ya mahakamai iliyosikiliza kesi! Mambo ya hovyo kabisa mawakili wa serikali.

Ifike kipindi ofisi ya DPP na DCI labda wapewe Dp world iendeshwe kiufanisi zaidi maana hawa mawakili wa mishahara hawana cha kupoteza
Daaaah!
 
Hapana mkuu ni kuwafanya wawe waadilifu. Wasisimamie mkosaji kumnasua kwa kisingizio cha kisheria.

Kuna wanasheria wakishajua ukweli tu, wanakukataa. Hawapo tayari kutetea uovu kisa kuna uwazi wa kisheria.
Acha uongo!

Hakuna mwanasheria anakataa kesi kwa sababu anajua ukweli wake.

Ni kama useme daktari kukataa kumtibu mgonjwa* kwa kuwa anajua mgonjwa haponi bali atakufa.
 
Nani kakudanganya ushahidi ndio kila kitu? Ni lazima uwe na mawakili mazuri hasa kwenye mahojiano na Cross examination ya ushahidi, utetezi, exhibits kama hauwezi tetea hoja vizuri hata kama una ushahidi utaanguka. Mfano Sabaya ushahidi ulikuwepo cha ajabu kosa lilikua kwenye aina ya mahakamai iliyosikiliza kesi! Mambo ya hovyo kabisa mawakili wa serikali.

Ifike kipindi ofisi ya DPP na DCI labda wapewe Dp world iendeshwe kiufanisi zaidi maana hawa mawakili wa mishahara hawana cha kupoteza

Acha maneno maneno yako bwana!

Kesi ya jinai ni sawa na ugonjwa, na mtuhumiwa ni sawa na mgonjwa.

Wakili wa utetezi ni sawa na daktari.

Wakili wa serikali ni sawa Israeli mtoa roho, na Hakimu ni kama PILATO.

Kwa hiyo mpambano hutokea, sasa mtuhumiwa ashinde au asishinde inategemea na ni nani mwenye nguvu, na siyo nani ana makosa.

Mawakili wa serikali wana kazi ngumu sana kwa sababu wao ndiyo wanaibeba kesi kwa asilimia 90.

Siwatetei ila ninajua kwa sababu na mimi nimefanya hayo majukumu.[/I]
 
Hiki ndicho kilisababisha wife agome watoto kusoma sheria! Sasa nimeshamwelewa! Kama mbingu ipo, mawakili hawataiona!
Acha upumbafu hadhari eti wife kagoma watoto wasisome sheria

Ujinba sna umeleta hapa wife wako ndio anapanga nin mnakula na kusoma hyo familia mam ndio mwenye akili

Kwanza litoto linaweza kusoma hyo sheria na bdo akashindwa kutoboaa law school akaishi kuwa muuza duka la mangi au mtendaji wa kata

Sheria uwendi kilaza

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mawakili wa serikali hamna kitu kabisa, kesi ilikua wazi kabisa ila wanashindwa kuwa serious. Sijui nini ambacho wanaweza hawa watu!! Na hata wangeshinda kesi wangeenda kubwagwa kwenye rufaa.
Kufa kwa mgonjwa hakumaanishi kwamba daktari ni dhaifu.

Halafu Mawakili wa pande zote, yaani wa utetezi na wa Serikali, pamoja na Jaji, ni Maafisa wa Mahakama, ambao jukumu lao linafanana na si lingine bali kusaidia haki ipatikane.

Hilo ndilo jukumu kuu.

Sasa huwezi tena kuja hapa kusema Mawakili wa Serikali hawajui kazi. Siyo sahihi!
 
Tatizo watu wanachanganya haki na taaluma. Mbele ya sheria kila mtu ana haki (hata muuaji) ya kupewa Wakili wa Kumtetea. Tena Wakili anakwambia useme ukweli wa kilichotokea then baada ya hapo anatafuta weak points ili Mteja wake ashinde kesi. Kwenye kesi hii Wakili aliyekuwa anamtetea Mtuhumiwa hana shida. Tatizo lipo kwa Wapelelezi na Waendesha Mashtaka wetu. Yawezekana hawajajengewa uwezo wa kutosha wa kupambana kisheria na Mawakili Binafsi ambao ni Wabobevu.
Watu wanamlaumu wakili wakati hata mtuhumiwa ana haki ya kutetewa hata kama amefanya kweli na kukutwa na wananchi. Hapo ni upande walioshitaki ndo shida.

Sema kuna maeneo, I wish kama mawakili waongozwe na kaubinadamu hasa Kwa wadhulumati maana unakuta nyumba au arfhi si yake lakini anakomaa ni yake na ukienda Kwa vyombo vya Sheria unakuta wakili anakomaa na vipengele vya kisheria vilivyokosewa mpaka mdai anakata tamaa. Natamani hata wangekuwa wanawaambia wateja wao kwamba "hii kesi hutoboi ila ninakomaa nikunasue ila jitahidi kukaa mezani hata umrudishie gharama zake". Maana Kuna wakati wanajua kabisa mteja wake kayatimba na kadhulumu lakini anampambania amashinda anavuta mkwanja alafu huyo anasepa anamwacha mteja wake na Mali ya dhuluma
 
Back
Top Bottom