Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,928
- 30,279
MJADALA WA WACHANGIAJI M1 JF Jukwaa la Historia 2013
Yericko Nyerere (pichani) miaka 11 iliyopita alifungua uzi JF kwa nia ya kupinga historia ya uhuru wa Tanganyika kama nilivyoieleza katika kitabu cha Abdul Sykes.
Huu ukawa mjadala mkali, mrefu uliokwenda kwa miezi sita mfululizo bila ya kusimama, uliopitiwa na wasomaji milioni moja.
Wasomaji waliosimama kama kundi moja wakimuunga mkono Yericko Nyerere walikataa kuwa Waislam na Uislam hauna cha kujivunia katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hawa walikuwa wakali kwa lugha na wakati mwingine walitoa vitisho na matusi.
Wachangiaji wachache hawajai kiganjani waliniunga mkono wakishikilia kuwa nimeandika historia ya kweli ambayo imefuta historia iliyokuwa haina ithibati.
Mimi nilisimama kwenye ukweli kuwa historia niliyoandika ndiyo historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika na historia ya kweli ya Julius Kambarage Nyerere katika uhusiano wake na wenyeji wa Dar es Salaam.
Mjadala kama huu haujapata kutokea tena na umeweka rekodi ya pekee sasa muongo mmoja umefika.
Leo nimeshangaa kuona uzi huu umewekwa JF Jukwaa la Historia na mwanachama anaejiita "Ubongokid," akiomba mnakasha ule wa watu milioni moja ufanywe kitabu.
Yericko Nyerere