TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigamboni

Aug 9, 2016
13
67
Mradi wa Tushirikishane (JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane") umeanza rasmi jimbo la Kigamboni chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Dr. Faustine Engelbert Ndugulile Dr F. Ndugulile

WhatsApp Image 2016-10-31 at 7.50.42 PM.jpeg

Washiriki wa Warsha ya Tushirikishane Kigamboni katika picha ya pamoja na timu ya Jamii Media baada ya kumalizika kwa warsha ya siku tatu ya mradi huo.
Tokana na misingi ya TUSHIRIKISHANE iliyoelemea katika kuwawezesha wabunge wa kuchaguliwa kutekeleza ahadi zisizopungua 4 kati ya jumla ya ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi kwa urahisi kwa kushirikiana na wananchi; mada hii itatumika kuwasilisha, kujadili na kupeana taarifa ya kile kinachojiri Kigamboni.

Katika Warsha ya Kigamboni, Mh. Ndugulile alikubaliana na jumla ya ahadi 5 zilizokubaliwa na wananchi ndani ya mradi huu.

WhatsApp Image 2016-10-31 at 7.50.44 PM.jpeg

Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mh. Faustine Ndugulile (Kushoto) na Mwanzilishi mwenza na mmoja wa Wakurugenzi wa Jamii Media Mike Mushi (Kulia) baada ya kusaini makubaliano ya kushiriki katika utekelezaji wa Mradi wa Tushirikishane.

TUSHIRIKISHANE – AHADI ZA MBUNGE
KIGAMBONI

1. Kukarabati vivuko vilivyopo pamoja na kupata kivuko kipya.

2. Kuongeza miundombinu ya umeme na kujenga kituo kipya cha kufulia umeme Kigamboni.

3. Ujenzi wa barabara ya Darajani- Kibada- Mjimwema kwa kiwango cha lami.

4. Kukomesha uvuvi haramu, kuwawezesha wavuvi kwa kuwapa nyenzo za kufanya uvuvi wa kina kirefu (Deep sea fishing) na kupunguza utitiri wa leseni kwa wavuvi.

5. Kujenga hospitali ya wilaya na kuboresha zahanati na vituo vya Afya.

Mada hii itatumika zaidi na Wana Kigamboni kutupa taarifa.

Baadhi ya Washiriki watakuwa:-

1. Mh. Mbunge Dr. Faustine Ndugulile Dr F. Ndugulile
2. Afisa habari Kigamboni, Vedasto Prosper Vedasto Prosper

Na washiriki wote wa Warsha hiyo na wale wote wenye mapenzi ya Maendeleo ya Kigamboni.

Karibuni.

[HASHTAG]#Tushirikishane[/HASHTAG] [HASHTAG]#Kigamboni[/HASHTAG]

Kufahamu majimbo mengine yenye mradi huu tembelea - JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane"

========

Akaunti za mradi wa Tushirikishane katika mitandao ya Kijamii:

Tushirikishane (@tushirikishane) • Instagram photos and videos

Tushirikishane | Facebook

Tushirikishane (@tushirikishane) | Twitter
 
Kigamboni ni moja kati ya maeneo yanayokua kwa kasi hapa nchini Tanzania ,kila uchao eneo hili hupokea idadi kubwa ya wakazi na wawekezaji wapya hivyo kupitia vipaumbele hapo juu kwa kuvitekeleza kwa wakati na kupitia mradi huu wa Tushirikishane naamini jimbo hili litapiga hatua kubwa sana kimaendeleo.
 
kile kipande kilichobaki bila lami kutoka darajani kinakera sana,halafu fanya mpango charge ya daladala zinazoenda machinga complex ipungue toka 5,000 walau hadi 3,000 sababu wanatupakia kama mikungu ya ndizi kufidia..
Kile kipande bwana kinaharibu shoo yote ya daraja! Yani kweli walishindwa kukimalizia? Nina imani kitawekwa lami ndani ya mradi huu wa Tushirikishane
 
kile kipande kilichobaki bila lami kutoka darajani kinakera sana,halafu fanya mpango charge ya daladala zinazoenda machinga complex ipungue toka 5,000 walau hadi 3,000 sababu wanatupakia kama mikungu ya ndizi kufidia..
Sasa hivi Kigamboni ni Wilaya. Najua kuna changamoto katika uanzishaji wa Wilaya mpya, lakini kwa hivi vipaumbele vyao, hakika watafanikiwa. Kila la heri.
babeney mathematics
 
Pale Kigamboni kuna viwanja vya miradi vimepimwa kama Geza Ulole, Kibada, Muongozo nk, ni wakati muafaka huduma za jamii kama barabara, Umeme na Maji vikafikishwa haraka ili maeneo hayo yaendelezwe. Inakuwa haina maana wala motivation kama maeneo ya miradi ya serikali yanakuwa sawa na squatter.

Kuna tatizo lingine sugu la kuchelewesha vibali vya ujenzi. Yaani pale Temeke Luna watu wameomba vibali vya ujenzi hawajapata kwa zaidi ya miezi sita, kila ukienda eti Baraza la Madiwani halijakaa kupitisha vibali. Sasa sijui kati ya Madiwani na Engineers nani anatakiwa kutoa kibali?? Na ukianza ujenzi utawaona manispaa hao wamefika wanakutaka u-stop ujenzi. Rushwa tupu.

Sasa unajiuliza, kwa nini ukanunue Kiwanja kilichopimwa halafu kupata kibali cha ujenzi upate usumbufu kiasi hiki?? Why not opt for squatter?? Unajenga bila kumfuata mtu. Ndio maana nasema hakuna motivation, its very discouraging
 
hello, wana mradi vipi mbona hakuna mpya? afsa habari wa mradi wa tushirikishane nini kinaendelea katika kutimiza ahadi za mbune wa kigamboni dhidi ya ahadi zake nne, zilizopewa kipao mbele?
 
kile kipande kilichobaki bila lami kutoka darajani kinakera sana,halafu fanya mpango charge ya daladala zinazoenda machinga complex ipungue toka 5,000 walau hadi 3,000 sababu wanatupakia kama mikungu ya ndizi kufidia..

Nashukuru Ndugu Nyabhingi kwa maoni yako. Kimsingi, michoro kwa ajili ya kipande kilichobaki imekamilika. Tunatarajia kazi kuanza muda wowote.

Suala la tozo pamoja na ufanisi wa huduma pale darajani ninaendelea kulifuatilia. Kumekuwa na kutupiana mpira kati ya NSSF, Wizara ya Ujenzi na SUMATRA kuhusiana na nani mhusika mkuu katika kufanya mapitio ya tozo. Naamini tutapata ufumbuzi hivi karibuni.
 
Pale Kigamboni kuna viwanja vya miradi vimepimwa kama Geza Ulole, Kibada, Muongozo nk, ni wakati muafaka huduma za jamii kama barabara, Umeme na Maji vikafikishwa haraka ili maeneo hayo yaendelezwe. Inakuwa haina maana wala motivation kama maeneo ya miradi ya serikali yanakuwa sawa na squatter.

Kuna tatizo lingine sugu la kuchelewesha vibali vya ujenzi. Yaani pale Temeke Luna watu wameomba vibali vya ujenzi hawajapata kwa zaidi ya miezi sita, kila ukienda eti Baraza la Madiwani halijakaa kupitisha vibali. Sasa sijui kati ya Madiwani na Engineers nani anatakiwa kutoa kibali?? Na ukianza ujenzi utawaona manispaa hao wamefika wanakutaka u-stop ujenzi. Rushwa tupu.

Sasa unajiuliza, kwa nini ukanunue Kiwanja kilichopimwa halafu kupata kibali cha ujenzi upate usumbufu kiasi hiki?? Why not opt for squatter?? Unajenga bila kumfuata mtu. Ndio maana nasema hakuna motivation, its very discouraging

Kigamboni ni Halmashauri Mpya. Tunarajia ucheleweshaji na urasimu utoaji wa vibali kutokuwepo.
Kama ulipeleka maombi yako Temeke na haujapata kibali, bado ninaweza kukusaidia. Wasiliana nami.
 
Asan
Niko makini. Nashukuru kwa Ushirikiano ambao wananchi wa Kigamboni wanaendelea kunipa katika kusimamia maendeleo ya Kigamboni.
Vyema mkuu, najua unachanga moto nyingi ila jitaidi kutupa update, hasa unapokutan ana vikwazo mfano ilo la NSSF, na wizara, maana tusipojua sisi tunaisi umesinzia kumbe upo update, tenga walau mora moja kwa wiki kutueleza unafanya nini dhidi ya ahadi zako, hasa zile nne ulizo zipa kipao mbele, natambua kuwa ili utekeleze kwa haraka zote zitegemea only ufatiliaji, kwa watumishi usika, najua unafatilia kwa umakini sasa jitaidi kutujuza. jioni njema!
 
Mwisho, nadhani kuna kauzembe kwa afsa habari wa jf,jimbo la kigamboni hawajibiki ipasavyo kutupa update, maana ilo ni jukum la msingi, anatakiwa kuwasiliana na wewe Mh au kama unaweza unamweka kwenye kamati mtendaji ili awe sehemu ya wafatiliaji na wasimamizi wa miradi, mbona wale wa kigoma ,a bukoba wana tupa news.
 
Ninaamini Maxence Melo AshaDii watalifanyia kazi suala hili. Taarifa zote muhimu zipo.
 
MRADI WA TUSHIRIKISHANE JIMBO LA KIGAMBONI:

Taarifa fupi ya Maendeleo ya mradi Wa tushirikishane katika jimbo la Kigamboni.
Yapata mwezi mmoja sasa yangu kuzinduliwa kwa mradi Wa tushirikishane unaoendeshwa na jamii media katika majimbo kadhaa ya Tanzania bara likiwemo jimbo letu la kigamboni-Dar es salaam.

Lengo mahsusi la mradi juu likiwa ni kujenga ushirikiano baina ya wananchi na viongozi wao Wa kuchaguliwa (wabunge na madiwani) na viongozi Wa serikali za mitaa yote ikiwa ni katika kuweka mazingira wezeshi kwa viongozi hapo kutimiza kile walichokiahidi kipindi cha kampeni za uchaguzi.

Ahadi zilizopitishwa baina ya washiriki wa warsha na Mh. Mbunge Wa jimbo la Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile ambazo ni sehemu ya ahadi zilizokuwa katika sehemu ya Sera na ilani yake aliyonadi pindi alipokuwa akiomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi wa Kigamboni.

Vipaumbele hivi vilichaguliwa na kupitishwa na washiriki Wa warsha ya siku tatu kupitia mradi wa tushirikishane ulioendeshwa na jamii media katika ukumbi Wa mikutano wa south beach-Kigamboni ambao wadau mbali mbali walihudhuria.

Moja kati ya sehemu ya ahadi hizo ni pamoja na kuongeza miundombinu ya umeme na kujenga kituo kipya cha kufulia umeme kigamboni ambapo hadi sasa kinachoendelea kufanyika ni kufanyiwa marekebisho kituo cha umeme mbagala na kurasini ambavyo hutegemewa kukamilika mapema mwezi February mwaka 2017 na itapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la umeme Kigamboni.

Pia kuhusu ujenzi wa kituo cha umeme Kigamboni taarifa zilizopo ni kuwa Tanesco wameshanunua eneo la ekari 20 katika kata ya Somangila na pia ujenzi wa kituo hicho cha umeme umeingizwa kwenye makisio ya bajeti 2017/2018.

Kumekuwa na upungufu wa nguzo za umeme ambapo mahitaji halisi ni nguzo 650 huku nguzo zilizopo ni takribani 100, Mh.Mbunge amefuatilia suala hili Tanesco makao makuu na hivyo inatarajiwa baada ya muda mfupi Kigamboni ikapata ongezeko kubwa la nguzo za umeme.
 
Mh. Dr F. Ndugulile kwanza nakupongeza kwa uchapakazi wako na bidii unazozionyesha ingawa bado kuna changamoto nyingi zinazokukabili hasa wakati huu ambao Kigamboni inaenda kuwa wilaya. Mimi nna mambo mawili matatu bado nayaona kama changamoto kubwa kwako na pia ni kero kuu kwa wakazi na wazawa wa Kigamboni;

1. Utaratibu na Muongozo kuhusu Mradi wa Mjimpya.

2. Shule ya sekondari (high school) ni aibu kwa kigamboni ya leo hakuna sekondari ya form five na six

3. Stendi mpya, hii ni kero kubwa mheshimiwa pale nyumbani ferry sio mbali na stendi hebu siku uende ukajionee hali halisi ilivyo ni aibu yaani magari ni mengi sana na stendi ndogo mno.

Ni hayo tu mheshimiwa sina mengi, ahsante
 
Back
Top Bottom