Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 11,208
- 19,001
Hapa juzi nilisikia viongozi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakisema wale wote wanaokiuka mfungo wa Ramadhani watachukuliwa hatua. Lazima nikiri huwa inanikera sana ninapokuwa Zanzibar kikazi wakati wa mfungo wa Ramdahani kujikuta nalazimishwa bila kupenda kufunga kama vile na mie ni muislamu.
Hivi nikiwa Zanzibar na kuanzisha hoteli ambayo nitatoa huduma ya chakula cha mchana hata wakati wa mfungo wa Ramadhani, au kula ndizi yangi hadharani wakati wa mfungo wa Ramadhani, nitashitakiwa kwa sheria ipi?
Au suala ni kuogopa jazba ya Wana Harakati? Polisi watanilinda kwa mimi kula wakati wa mfungo wa Ramadhani?
Nchi yetu Tanzania haina dini, Zanzibar au Tanzania bara, sivyo?