Mikopo ya hazina, Maafisa Utumishi wanaomba 10% ili waweze kupitisha

Mwezi mmoja boss.....nimekunja mpunga wangu....mpunga Haina riba....unarudisha uliopewa....kifupi mshahara wako unapewa advance ya nusu ya mshahara wako....yaani unalipwa miaka SITA ijao nusu ya mshahara wako
Bora hii aisee kuliko kwa haya mabenki yenye riba kandamizi.
 
Shida sio halmashauri, Ni hazina wenyewe, kwa nini wasitangaze kuwa kuwa kuna mikopo, waorodheshe halmashauri zote fedha zilizopo na masharti ya kupata na deadline, hii mikopo Ipo miaka mingi Ila nauhakika 90% ya watumishi wa umma hawajawahi kuisikia, Ni kakundi ka watu kanajitangazia na kujikopesha
Ni kweli haisikiki kwa Sana....maana SERIKALI ikifanya hivyo mabenk yatafunga OFISI zao. Pia kumbukeni hata mkituma kwenye hazina portal bado harmashauli wanawajadili wakupe au wasikupe kutokana na vigezo vyako....pia mwisho wa siku Ili upate mkopo, ni lazima mkurugenzi apitishe......kwa hiyo maafisa utumishi hawaepukiki ndugu zangu.......ni kuomba mungu....ukipata ni mkopo mzuri
 
Halmashauri zingine pesa zimetoka mda tu....mwezi wa 11, hakuna rushwa ya aina yoyote Ile....Mimi nimepata bila kumjua mtu halmashauri, nimejisajili hazina portal,nikapigiwa simu niandike barua nitumie kwa watsap,baada ya hapo....nikapigiwa simu nidownload mkataba, nimpelekee boss wangu asign, baada ya hapo nikawekewa mzigo...Tena walinipigia wenyewe kuwa mzigo umeingia. Huo ndio uzoefu wangu....kwetu hatujaombwa hata mia. Wenzangu waliniambia huo mkopo kupata hauwezi maana wanagawana wakuu wa idara tu.....nikawaambia kuwa hacha niombe Ili niwe sehemu ya ushuhuda wa haya mnayosema.....mwisho wa siku nimepata.
Uko wapi huko nihamie, maana Kuna Halmashauri zina watu Wana njaa kaliiiiiiiiiiiio mixer roho za kichawi
 
Kumekuwa na matangazo mbalimbali yanayohusiana na mikopo kwa wafanyakazi nadhani ni Tanzania Nzima.

Mfano kwa wilaya ya Uyui kuna 400, Tabora manispaaa kuna bilion 3, kwanza tunashikuru viongozi wa wilaya na mkoa kwa kutangaza mikopo hiyo kwani kuna wilaya ya nyingine na mikoa hakuna kabisa matangazo ya mikopo hiyo. Changamoto ya mikopo ni vishoka ambao ni maafisa utumishi na watumishi wengine wasiowaaminifu kwenye majukumu yao.

Mfano, nimeona tangazo la barua ya Tabara mjini watu waandike barua kisha wapate semina, hapo ndio Rushwa inapoanzia kwani kikawaida huwezi andika barua bila kuweka maji ya kunywa vinginevyo barua yako haitofanyiwa kazi. Pia Rushwa ya ngono itatawala kwa wadada kwani ikumbukwe mikopo hiyo haina riba.

Mikopo wafanyakazi wameambiwa waombee hazina portal, watu wajisajili kisha waombe, na wakishaomba mikopo italipwa kupitia Mishahara yao na makato yataingizwa na maafisa utumishi kulingana kiasi kitachoombwa.

Sasa hii ya kuitana na kuanza kupeana semina ni ulaji mwingine ambao viongozi wanautengeneza. Wafanyakazi wamekuwa wanachukua mikopo katika taasisi mbalimbali za kifedha na hazijawahi kutoa semina.

Kinachofanyika mkoa wa Tabora ni kutengeneza mazingira ya Rushwa kwa sababu barua haziitajiki katika maombi haya.

Nimeona pia Uyui wamewaambia watu waombe kupitia hazinal portal lakini anayehusikana kuingiza makato amekuwa akipigiwa simu hapokei tangu tangazo litoke na pia anajuzingusha kukutengenezea mazingira ya ile 10% ambayo lazima iachwe.

Serikali imekuwa ikifanya jitihada za dhati kututoa katika analojia kutupeleka katika digital kupitia mifumo yake mingi ambyo imeianzisha mfano "EES" salary slip portal na nk. sasa tusirudi kwenye mambo ya kuandika barua kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunapingana na serikali.Tanzania ni yetu sote

View attachment 2842864View attachment 2842867View attachment 2842869
Mimi nimeomba tangu mwezi Oktoba, lakini hadi sasa hakuna(sijapata). Wazoefu hii mikopo inachukua muda gani hadi upewe?
 
Kauli ya Rais, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ni zaidi ya Sheria.
Na Rais ameishatamka kwamba, "KILA MTU ALE KWA UREFU WA KAMBA YAKE"
 
Hapa kwenye postcode, house number, street, address unajaza zipi wadau za kituo ninachofanyia KAZI au sehemu ninayoishi? Naomba msaada
 
Post code, muulize HR au mkuu wako wa idara,.....house namba ninamba unayoishi, address ni chukua ya kazini kwako,
 
Back
Top Bottom