PAZIA 3
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 1,078
- 1,870
Habari za Leo wapenda soccer?
Natumai kichwa/title ya thread hii imejieleza vizuri. Nimewaza nikaona nitumie platform hii kwenu ili kama itawezekana, tushawishi viongozi wa mpira kuiondoa michuano ya Mapinduzi cup na badala yake tubaki na Muungano cup. Nasema hivi siyo kwa lengo la kisiasa ila nikwasababu ya ratiba za ligi mbalimbali zinazozikabili timu zetu za mpira. Lakini pia ukichunguza kwa kina, utagundua kuwa, Mapinduzi cup inajumuisha timu za Muungano, yaani zinazotoka bara na zile za Zanzibar, kingine, muda wa Mapinduzi cup ni mwezi January na Muungano cup ni mwezi April, hapo tutalaumu timu zetu tu pale zitakaposusia Moja ya mashindano fulani. Kwakuwa viongozi wetu wamelifufua kombe la Muungano, ni vyema sasa tuondoe Mapinduzi cup tubaki na Muungano cup kwa mantiki kwamba kombe la Mapinduzi linataswila ya Muungano.
Cha kuboresha tu katika kulifanya kombe la Muungano, kuwe na timu at least 16, nane zitoke bara na nane zitoke visiwani. Makundi yapangwe mapema na mashindano hayo yaanze mapema ili mpaka kufikia kilele Cha mashindano hayo, tuwe na timu nne tu zitakazocheza nusu fainali na fainali katika wiki ya kilele Cha sikukuu ya Muungano.
Huu ni mtazamo wangu, mnaweza kuboresha mawazo yangu ili kupata wazo Bora zaidi.
Ahsanteni