Zaytun Seif Swai ahoji Bungeni Ujenzi wa Daraja la Mto Athumani - Ngorongoro

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,996
961
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha, Mhe. Zaytun Seif Swai Ameuliza, Je, ni lini Serikali itaanza Ujenzi wa daraja la mto Athumani?​

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amejibu na kusema;

"Daraja la Mto Athumani liko katika barabara ya Mkoa ya mto wa Mbu - Selela - Engaruka - Ngaresero - Sale - Wasso - Loliondo (KM 217) katikati ya Kijiji cha Selela na Engaruka Mkoani Arusha"

Maandalizi ya ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu ya barabara kutoka Selela - Engaruka (217) ikiwemo ujenzi wa Daraja la Mto Athumani yanaendelea. Kazi za ujenzi zimepangwa kuanza katika mwaka wa fedha 2024-2025.

Serikali ipo katika hatua za mwanzo zamaandalizi ya ujenzi wa daraja la mto Athumani lililopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha katika bajeti ya mwaka wa fedha za ujenzi na kikikamilika kitatoa fursa za kiuchumi.

Niwahakikishie wabunge na Wananchi wa eneo husika kwamba daraja la mto Athumani limepewa kipaumbele na Serikali na tayari Wizara imeshapeleka maombi ya fedha za ujenzi wa daraja hilo pamoja na madaraja mengine madogo kumi na tatu.

GGXMuLLXsAAa2j2.jpg
GMajW7sWcAAQsFD.jpg
 
Ukiachana na hilo swali aliouliza..,mjukuu wa Swai ni mzuri😋
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom