MHE. DKT. ALICE KARUNGI KAIJAGE, Akichangia Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu Mwaka 2024-2025 ya Tsh. Bilioni 350.9.

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,037
974
MHE. DKT. ALICE KARUNGI KAIJAGE, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Akichangia Bajeti katika Majadiliano ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu Mwaka 2024-2025 ya Tsh. Bilioni 350.9.

"Ushauri wetu Wabunge utasaidia Serikali kuimarisha utekelezaji wa Vipaumbele ambavyo vimeainishwa kwenye mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2024-2025, mpango huu ni wa tatu katika mpango mkuu wa miaka mitano ambao una dhima ya kujenga uchumi shindani, Viwanda kwaajili ya maendeleo ya watu (mtu mmoja mmoja) na kipaumbele cha ukuzaji wa ujuzi (Rasilimali watu)" - Mhe. Dkt. Alice Karungi Kaijage, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani

"Wizara ya Mipango na Uwekezaji imejipambanua katika kutekeleza mpango wa tatu wa Taifa wa Maendeleo itazingatia misingi kumi itakayowaongoza kutekeleza mpango wa Maendeleo ya Taifa. Msingi (07) ni kuwa na Rasilimali watu ya kutosha iliyo bora inayokidhi matakwa ya wakati huu ambayo imetawaliwa na Teknolojia na ubunifu lakini Msingi mkuu tunaoutegemea sana ni kuwa na nidhamu ya utekelezaji wa Mipango yao waliyojiwekea" - Mhe. Dkt. Alice Karungi Kaijage, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani

"Wizara ya Mipango na Uwekezaji imeendelea kuboresha mazingira bora ya biashara na imefungua idara za biashara katika Halmashauri 184 ina maana kuna uhitaji wa watumishi. Imefungua Vitengo kwenye Halmashauri vya mazingira ya biashara. Imekuja na mfumo wa tathimini na Ufuatiliaji katika Wizara za Kisekta na taasisi za Serikali zinazojitegemea" - Mhe. Dkt. Alice Karungi Kaijage, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani

"Kwenye Halmashauri nyingi nchini ukikutana na watumishi amesimama kuongea au ameandika kwa maandishi jambo la kwanza utakalokutana nalo wanampongeza sana Mheshimiwa Rais, wanasema amejali maslahi yao, ameboresha mazingira ya wao kufanyia kazi. Hii inaonyesha wametambua mchango wa Mheshimiwa Rais" - Mhe. Dkt. Alice Karungi Kaijage, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani

"Suala la Elimu na Miundo; Wizara ya Utumishi imefanya kazi kubwa sana lakini watumishi wanakwenda kusoma, wanajisomesha kwa shida tena walio kazini, anarudi na ku Submit cheti kuna baadhi ya Miundo anashuka daraja, hawezi kupanda. Matokeo yake wakitoka kusoma wanaficha vyeti vyao wengine hawavi Submit. Naomba jicho la pili la Wizara ya Waziri Mkuu waende kuangalia wawasaidie Utumishi" - Mhe. Dkt. Alice Karungi Kaijage, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani

"Ni kweli hakuna Haki bila Wajibu lakini wajibu wanaofanya watumishi wawe wanalipwa kwa wakati. Kuna Halmashauri mtumishi (Mtendaji Kata) amefanya kazi kwa miezi 7 anakwenda na kurudi lakini hajawahi kulipwa posho yake na wengi wanategemea mapato ya Halmashauri lakini kuna Halmashauri hazina uwezo. Halmashauri zenye njia za ubunifu tuwasiadie maana hatuwezi kulipwa na Serikali Kuu wote" - Mhe. Dkt. Alice Karungi Kaijage, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani

"Ofisi ya Waziri Mkuu imekuja na Tume inayotembea (Tume ya kurekebisha matatizo ya wafanyakazi mahali pa kazi. Tume ina kazi kubwa sana ya kufanya maana kuna mambo mengi sana kwenye Halmashauri zetu na taasisi kule chini" - Mhe. Dkt. Alice Karungi Kaijage, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani

"Miaka Mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan ameweza kupandisha vyeo na madaraja zaidi ya watumishi 405, 500 iliyogharimu Serikali Tsh. Trilioni 1.11. Amebadirisha Kada na Miundo iliyogharimu Serikali Tsh. Bilioni 2.5. Amelipa malimbikizo ya watumishi 130,000, ziadi ya ajira 150,00 na juzi Idara ya Afya zimetoka ajira 8,900. Suala la kikokoto Rais amesema amelisikia, tumpe nafasi suala la kikokoto aweze kufanya maamuzi ya tija" - Mhe. Alice Karungi Kaijage, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani
 

Attachments

  • hqdefaultmnbvgytr.jpg
    hqdefaultmnbvgytr.jpg
    14.6 KB · Views: 1
Kwa mtu kama mimi sijawahi kuelewa maana na makadirio ya bajeti ... kwa ujumla tumezoea kuandaa bajeti ili kupima makadirio na matumizi ila hatujawahi kuona serikali ikituonesha matumizi ya bujeti iliyotenga na kilichobakia zaidi tunaona tu makadirio ya bajeti ...


By the way sio mzuri wa kuandika ila niseme tu kwenye hii bajeti ya wanayopitisha wabunge pesa nyingi zinaishia mikononi mwa waheshimiwa kuanzia mawaziri makatibu wa wizara hadi wakurugenzi

Kama huamini ... serikali haijawahi kuandaa bajeti na kufanya reconciliation ya kile kilichotengwa na kilichotumika.
 
Kwa mtu kama mimi sijawahi kuelewa maana na makadirio ya bajeti ... kwa ujumla tumezoea kuandaa bajeti ili kupima makadirio na matumizi ila hatujawahi kuona serikali ikituonesha matumizi ya bujeti iliyotenga na kilichobakia zaidi tunaona tu makadirio ya bajeti ...


By the way sio mzuri wa kuandika ila niseme tu kwenye hii bajeti ya wanayopitisha wabunge pesa nyingi zinaishia mikononi mwa waheshimiwa kuanzia mawaziri makatibu wa wizara hadi wakurugenzi

Kama huamini ... serikali haijawahi kuandaa bajeti na kufanya reconciliation ya kile kilichotengwa na kilichotumika.
Umenena vyema
 
Back
Top Bottom