UZUSHI Mgonjwa wa Omicron aripotiwa Tanzania, alazwa Hospitali ya Amana

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
omicron_colourbox.jpg


Wakati Rais Samia akimpolea Rais wa uganda Yoweri Mseveni uwanja wa ndege jijini Dar kuna taharuki ya kuwepo mgonjwa wa kwanza wa kirusi kipya kilichogunduliwa Afrika ya Kusini siku tatu zilizopita.

Mgonjwa huyo Mzungu Rais wa Botwana aliyedaiwa kuingia nchini kutokea mjini Johannesburg Afrika ya Kusini leo asubuhi kwa ndege ya shirika la ndege la KQ la Kenya.

Rais Mseveni na mweyeji wake wamekutana eneo ambalo kwa sasa huenda ndio kitovu cha kirusi kipya cha Corona.

Tanzania haijachukua hatua zozote za kujilinda na kirusi hicho kipya huku nchi za nyingi zikizuia ndege kutoka mataifa kadhaa ya kusini mwa afrika kuzuia kuenea kwa kirusi hicho kinachoadaiwa kuwa kinasambaa kwa kasi zaidi.

Mgonjwa huyo alipimwa baada ya kuonekana kuwa na dalili zote za corona ikiwemo joto kali.

Bado mamlaka za Tanzania hazijatoa taarifa za uhakika kuwa mgonjwa huyo yupo nchini.
 
Tunachokijua
Mlipuko wa COVID-19 umeitesa Dunia tangu 2019. Nchi nyingi Duniani ziliathiriwa ikiwemo Tanzania. Mlipuko wa Ugonjwa huo ulikuja kwa aina tofauti tofauti, mojawapo ya aina ya virusi hivyo ilikuwa ni Omicron.

Kirusi cha Omicron kinatajwa kuwa na asili ya Afrika Kusini na kwa mara ya kwanza mtu aliyekutwa na virusi hivyo alionekana Botswana mnamo Novemba 2021. Kirusi hicho kilisambaa katika nchi nyingine mbalimbali.

Kwa taarifa ya Wizara ya Afya ya Tanzania, iliyotolewa Septemba 8, 2022. Tanzania ilikuwa na jumla ya maambukizi 35,747 na vifo 808 vimethibika, hata hivyo hakukuwa na kisa cha Omicron kilichorekodiwa.

Taarifa ya uvumi iliyotajwa kuwa kuna mgonjwa wa Omicron amelazwa Hospital ya Amana haikuwa sahihi.
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom