SoC03 Mgawanyo wa Madaraka Kwa Utawala Bora

Stories of Change - 2023 Competition

Mamshungulii

Senior Member
May 3, 2023
124
66
Utawala-wa-sheria unahitaji kuwa mihimili mikuu, serikali, bunge na mahakama inatenganishwa. Kutenganishwa huko hakuna maana kuwa madaraka haya yanatumiwa na asasi mbalimbali tu ( kwamfano serikali, bunge na mahakama ), lakini pia kuwa watu-binafsi hawawezi kuwa wajumbe katika asasi zaidi ya moja kati ya asasi hizi ( kwa mfano waziri mkuu hawezi kuwa jaji wakati huohuo).

Ni wazi kuwa utenganisho madhubuti wa madaraka haujapata kuwepo: katika kila nchi kuna asasi zinazoshiriki katika matumizi ya madaraka ya aina mbili. Jambo la kawaida ni kuwa serikali inaweza kutoa aina fulani ya kanuni (amri, maagizo ya kiserikali.) au kuwa na mamlaka ya pamoja ya kutoa aina fulani ya kanuni. Zaidi ya hayo, katika sheria-za-madai na sheria zisizoandikwa sheria za kawaida za nchi huchukuliwa kuwa ni sehemu ya sheria zilizopo kwa namna sheria hizo zinavyofafanuliwa na kutumiwa katika hali maalumu . Hii ina maana kuwa wakati majaji wanapotumia madaraka yao ya kisheria huchangia vilevile katika kuendeleza sheria katika ngazi-ya-kitaifa.

Aghalabu,, nchi-nyingi huwaruhusu watu-binafsi kuwa sehemu ya asasi mbili kwa wakati mmoja kwa baadhi ya mambo. Kwamfano, nchini Tanzania waziri anaweza kuwa Mbunge vilevile. Kusema kweli, hali ilivyo katika nchi nyingi inaweza kuelezewa kuwa ni ile ya mfumo wa kudhibitiana na si ule wa utenganisho madhubuti wa madaraka. Madaraka-hugawiwa miongoni mwa asasi na watu binafsi mbalimbali kwa namna ambayo hakuna asasi au mtu binafsi anayeweza kuhodhi madaraka kamili kwa sababu matumizi ya madaraka kila siku yanadhibitiwa kwa kutumiwa madaraka mengine. Mfano mzuri ni jinsi mabunge yanavyoisimamia serikali. Mfumo madhubuti wa kudhibitiana ni muhimu sana kwa utawala wa sheria. Kwa mfano, kazi muhimu ya utawala-wa-sheria, kudhibiti matumizi-ya-madaraka, haitawezekana ikiwa madaraka-ya-serikali na ya kutunga-sheria yatakuwa chini ya asasi-moja au mtu-mmoja-binafsi.

Mahitaji muhimu ya utawala-wa-sheria ni kuwepo kwa mahakama isiyopendelea upande wowote na iliyo huru ambayo, ikiwa ndiyo kimbilio la mwisho, inaweza kutatua migogoro na kuhakikisha kuheshimiwa kwa sheria. Katika jamii yoyote ile migogoro lazima itokee. Baadhi ya migogoro hii hujitokeza kutokana na mahusiano kati ya serikali na raia. Migogoro mengine hutokea kutokana na mahusiano kati ya raia au vyombo vingine binafsi. Baadhi ya migogoro hii inahusiana na ukweli.

Polisi inamshitaki mtu kwa kushiriki katika ghasia au polisi inashtaki wanajamii waliohusika kumchoma moto aliyedhaniwa kuiba/kuwa mchawi-mtu/watu huyo anakataa kuwa alikuwepo hapo. Mwanamke anasema kuwa bado anamndai jirani pesa- jirani anakataa na kusema hakukopa pesa.

Migogoro mengine ni kuhusiana na sheria. Mtu-mmoja anadai kuwa ameona gari mtandaoni, na wakawasiliana kwa kutumiana uthibitisho wa gari za kutosha kwa njia ya mtandao,na akaamua kutuma pesa kimtandao. Muuza-magari anabisha kuwa hakuna mkataba na kuwa halazimiki kuliuza hilo gari, kwa sababu tangazo hilo lilikuwa ni mwaliko tu wa kutaka kuanza majadiliano wala si ahadi ambayo kama ikikubaliwa inakuwa ni mkataba wa kisheria. Na namba zilizotumika pia sio zake hivyo hausiki katika upotevu-wa-pesa hizo. Migogoro Lazima Isuluhishwe kwa Mujibu-wa-Sheria, Uamuzi lazima ufanywe kutokana na ukweli, sheria na matumizi-ya-sheria kuhusiana na ukweli.

Bila ya uamuzi kama huo, migogoro itaendelea au itasuluhishwa kwa namna nyingine, na labda katika hali mbaya, kwa kutumia-nguvu. Zaidi, ikiwa watumishi-wa-serikali na raia inawapasa watii-sheria, ni lazima wajue ufafanuzi upi wa sheria ni sahihi/vipi sheria itumike kuhusiana na ukweli. Uamuzi wa chombo-chenye-uwezo unaweza kutoa ufafanuzi huo. Umuhimu wa uamuzi huo unapindua usuluhishi wa mgogoro kati ya pande mbili kwa jambo fulani. Unasaidia kuhakikisha kwa ujumla kuwa watumishi-wa-serikali na raia wanazielewa sheria na wanaweza kuzitii.

Uhuru Uamuzi kama huu lazima utolewe na upande wa tatu, jaji au mahakama. Wale walio katika mahakama lazima wawe huru kutokana na shinikizo kutoka nje. Lazima waamue kwa mujibu wa sheria na si chochote kingine isipokuwa sheria. Hii ina maana, kwanza, lazima wawe huru kutokana na serikali. Hukumu zao zisishawishiwe na madaraka yenye nguvu.

Kwaupande mwengine, majaji lazima waheshimu kanuni za utendaji na uadilifu wa kiueledi, na wawajibike kwa utoaji wa hukumu kwa njia ya haki. Uhuru huu lazima uendelezwe na kuhakikishwa kwa mujibu wa sheria kuhusiana na mambo kama vile uteuzi wa majaji, usalama wa kuwa kazini, maslahi ya kazi na namna ya kupanga mishahara – yote haya inalazimu yatengwe na ushawishi wa serikali. Kutopendelea Upande Wowote Uhuru wa jaji kutokana na ushawishi wa nje ina maana, la pili, kuwa jaji hapendelei upande wowote, kwa maneno mengine ni kuwa yeye hapendelei upande wowote katika kesi iliyo mbele yake. Hii inahitaji, miongoni mwa mambo mengine, kama pande husika zina sababu za kutia shaka kuwa jaji anapendelea, wana fursa ya kumpinga. Matokeo yake yanaweza kuwa jaji huyo anatolewa kutoka katika kesi hiyo. Vile vile majaji lazima wawe na haki ya kujinusuru kama wana uhusiano na mmoja katika pande zenye mgogoro.

Kwa maneno ya Mwandishi mahiri wa Kisheria Chris Maina Peter, alisema “… jamii inatarajia mwamuzi awe mtulivu, mwenye malengo na asiyeegemea upande wowote; wakati huo huo wakati aina fulani ya uanaharakati wa mahakama hauonekani tu kama unaruhusiwa - lakini kama mila ndani ya sheria ya kawaida. Tamaduni inaweza kudumishwa tu na majaji na maafisa wengine wa mahakama ambao hawaogopi kusumbua hali ilivyo. Inapaswa kuwa maafisa wa mahakama ambao wamejitayarisha kusimamia haki hata kama hiyo ina maana kwamba mbingu zinapaswa kuanguka. Hali ilivyo inawanufaisha wengine wanachama wa jamii katika jamii yoyote iliyogawanyika. Kuibadilisha ni kubadilisha ‘mbingu zao”..

MWISHO
Tishio-moja kubwa kwa kutopendelea-upande-wowote na uhuru-wa-mahakama ni RUSHWA.
Kwasababu hii, lazima iwepo mishahara-ya-kutosha,mifumo ya kisasa ya kiteknolojia, usalama wa kuwa kazini na vitu kama hivyo.

Suala hili liwe na uiano na wajibu wa kuheshimu kanuni za utendaji na uadilifu wa kiueledi .
Maadili ya Kiueledi katika Kuzitumia sheria kwa namna iliyo sahihi, usawa-kwa-wote, kutoshawishika na sinikizo kutoka nje hakuhitaji kanuni na taratibu za kutosha tu. Kunahitaji vilevile viwango vya juu vya maadili ya kiueledi na tabia nzuri kwa wahusika wote wa mchakato wa kusuluhisha mgogoro.

Majaji wasijitie hatarini katika maisha yao ya faragha kiasi cha kuathiri uhuru wao na uwezo wao wa kutopendelea-upande-wowote kwa kujifanya waweze kuathirika kwa urahisi na shinikizo za ushawishi wa nje. Lazima wafuate sheria, hata katika mambo madogomadogo ambayo raia wengi wa kawaida huweza kuwa na tabia ya kutokuitii sheria.

Majaji lazima wachukue hadhari vilevile na kushiriki katika vitendo ambavyo hata kama ni vya halali, vinaweza kuwafanya waathirike na shinikizo kutoka nje.
 
Back
Top Bottom