Mfanyabiashara Alex Msama akamatwa kwa tuhuma za Utapeli wa Viwanja vya Tsh. Milioni 800

Du naona wana JF tumeshamhukumu Mr. Msama,tuangalie upande wa pili wa coin,je waziri kumpeleka suspect police ametumia sheria gani?,je suspect amefunguliwa docket police?je police wameshafanya uchunguzi na kuthibitisha tuhuma dhidi ya suspect?ni vema kama nchi tukaanza kuishi kisheria sio mihemko ya kisiasa,sasa huyu anatakiwa apelekwe kwa court within 48 hrs je police wana kesi dhidi yake?,KATIBA mpya ni muhimu maana walalamikaji wangeweza kwenda kwa PP kutoa malalamiko yao kama police haikuwasikiliza,kitendo hiki cha waziri kwangu ni NO na udhalilishaji,huwezi kumtoa suspect hadharani kabla ya kupanda kwa court
kwanza kaitwa na kaitikia wito, hata Polisi wangemuita angeenda.

Jeri kafanikisha lengo la kumdhalilisha jamaa.
 
Ila huyu bwana ana mazuri yake pia.

Binafsi sikuwahi kumjua Hadi pale nilipokutana Hospital usiku saa sita nikiwa na mtoto wangu ambae alizidiwa GHAFLA nyumbani na kumpeleka hapo hospital nikitegemea Bima mfukoni shi. Mia mbovu Sina🤣

Basi mtoto alipimwa akawa amelala kwa benchi.

Ndipo yeye alipotokea na kumkuta mtoto kalala akasema mtoto msiponji,

Kishaa akaagiza nesi ampe panado.

Mimi nikajua ndo Mganga Mkuu wa hapo.

Akaagiza apimwe na Homa ya dengue,Kipimo kulipia 50,000/ sisi tukasema hatuna pesa hiyo.

Yeye akamwagiza nesi ampime mtoto,atalipia yeye!!!

Majibu yakatoka hakuna kitu ila mtoto kachemka mbaya sana!!

Akatuambia tuchukue Bima atupeleke hospital nyingine! Mimi nikajisemea huyu ni MMILIKI wa hii hospital hivyo anatupeleka hospital yake nyingine kubwa🤣

Wale wahudumu wote walokuwa kaunta aliwapa 15,000 Kila mmoja na WALIKUWA kama 4 hivi.

Wakati nachukua bima yangu alikuja nesi mmoja AKANIAMBIA unahama hospital huyo mnamjua ??

Nikasema Mimi simjui na Mimi najua nyie ndo mmetujamisha.!!

Nikasema asije kuwa mtekaji,Nikaandaa meseji ya maelekezo kwenda kwa Kamanda wa polis nikaitegesha kabisa ili nikiguswa tu naisend🤣🤣

Nilipotoka nje nilikuta Gari jeusi V8 MPYAAA😀Kwa woga woga na kwa tahadhari ya hali ya juu nilipanda😀

Aliendesha Dakika 10 nyingi tulifika hospital hiyo ,Hapo bima hawatumii ni kulipa kwa kesho ,

Akaagiza tuhudumiwe Kila kitu gharama atakuja kulipa yeye!!!


Kweli mtoto alianza vipimo upya na kifupi gharama ilikuja 136,000/

Tylipomaliza matibabu tukampigia sekunde nyingi alikuja akalipa gharama zoote👏

Nilimuomba namba yake alinipa , Nilimuuliza upo wapi hakusema .

Siku Moja tulienda tena kwenye hiyo hospital wife anajuana na nesi mmoja alimuuliza yule mtu wa siku ile alikuwa nani,?

Akamwambia huyo ni Alex Msama huwa anapenda sana kusaidia wakinamama na hasa Watoto😀

Milima haikutani ,Binadamu hukutana !! Tulikutana nae tena baada ya miezi mingi hapo hapo na majira hayo,Tulimkumbuka tukamsogelea tukamkumbushia akaja akamuona mtoto akatuachia tena 50,000/=

Ndo mwisho wa kuonana nae tena Hadi Leo YAPATA miaka sita nyuma!!
Kuna mtego alikuwa anakuwekea. Una bahati sana na nakushauri ukimuona siku nyingine usijirahisi hivyo.

Iko siku atakubebesha madawa ya kulevya kama alivyomtumia Rose Muhando
 
Du naona wana JF tumeshamhukumu Mr. Msama,tuangalie upande wa pili wa coin,je waziri kumpeleka suspect police ametumia sheria gani?,je suspect amefunguliwa docket police?je police wameshafanya uchunguzi na kuthibitisha tuhuma dhidi ya suspect?ni vema kama nchi tukaanza kuishi kisheria sio mihemko ya kisiasa,sasa huyu anatakiwa apelekwe kwa court within 48 hrs je police wana kesi dhidi yake?,KATIBA mpya ni muhimu maana walalamikaji wangeweza kwenda kwa PP kutoa malalamiko yao kama police haikuwasikiliza,kitendo hiki cha waziri kwangu ni NO na udhalilishaji,huwezi kumtoa suspect hadharani kabla ya kupanda kwa court
Wewe kama ni TAPELI kama Alex Msama tambua kuwa dawa yako inachemka na huwezi kukwepa kikombe anachokunywa Msama.

Masuala ya Polisi na Mahakama watayatatua wenyewe, sisi hayatyhusu
 
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam kwa tuhuma za kutapeli viwanja vinne vya Beatrice Mshumbuzi, vinavyokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi milioni 800.

Msama amekabidhiwa kwa polisi leo na Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa.

View attachment 2968425
Mawaziri Jerry Slaa na Dorothy Gwajima wanafanya kazi kwa vitendo, pongezi kwao ikiwa hatua kama hizi zitachukuliwa kwa wakati basi malalamiko ya wananchi yatapungua kama si kuisha.
 
View attachment 2968415

Promota wa Muziki wa Injili , ambaye pia ni mlokole Alex Msama , akiwa pia ni Mkurugenzi wa Msama Promotion , amekamatwa na Polisi kwa makosa ya Utapeli wa viwanja

Msama Pia ni kada Maarufu wa CCM na Mgombea wa mara kadhaa wa nafasi mbalimbali za uongozi kwenye Chama hicho

Amedakwa leo alipoitikia wito wa Waziri wa Ardhi aliyemraka aripoti ofisini kwake kwa Mahojiano
Ndio kwanza namuona huyu mtu anaishi wapi!
 
Back
Top Bottom