Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,899
- 155,954
Ukimtoa Malkia Elizabeth II basi hakuna kiongozi mwengine wa kifalme aliyeiongoza uingereza kwa miaka mingi zaidi kumzidi Malkia Victoria kwa miaka 64 ....Ndio malkia Victoria ndio jina Lake limepewa ziwa la Victoria linalopatikana hapa afrika ya mashariki ....jina lake kamili aliitwa Alexandrina Victoria
Malkia Victoria aliipigisha hatua kubwa himaya ya Uingereza katika nyanja mbali mbali kuanzia kisiasa, kiuchumi, na kijamii
- Alianza kutawala mwaka 1837 akiwa na miaka 18 ambapo alirithi uongozi kutoka kwa mjomba wake William IV.
- Alikuwa na uwezo wa kuongea lugha zaidi ya moja kingereza, kijerumani, kilatini, kifaransa, kihindi, na kiitalia
-Katika utawala wake ndio miti ya Christmas ilivyopata umaarufu
-Ni mama wa watoto 9 aliozaa na mume wake mwana wa mfalme Albert watoto hao ni Victoria, Edward, Alice, Alfred, Helena, Louise, Arthur, Leopold and Beatrice.
- Katika utawala wake ndio mapinduzi ya viwanda yalivyopata kasi zaidi ... Haya mapinduzi ya viwanda ni mojawapo ya sababu iliyoifanya uingereza kuwa hapo ilipo sasa... Kwa sababu kupitia mapinduzi hayo maisha ya watu wa uingereza yaliboreka zaidi kwan makampuni yalitengenezewA mazingira ya kuwalipa vyema wafanyakazi wao na pia kuwapa huduma muhimu kama shule na makazi
-Alinusurika idadi kubwa ya majaribio yakuuwawa Zaidi ya majaribio 8 ya kuuwawa
- Chini ya utawala wake aliweza kuitanua himaya yake sehemu mbalimbali duniani kama Australia, New Zealand, Canada, South Africa and India.
- Ni katika utawala wake ndio aliboresha mifumo ya elimu na kusitisha biashara ya utumwa
-Ni katika utawala wake walifanya marekebisho mengi ya sheria yakiwemo ya kibiashara... Yaliyoweza kuwapa nguvu wafanya biashara wa kiingereza kufanya biashara kimataifa huku wakiwa wanalindwa na sheria
-Kwenye utawala wake ndio aliboresha miundo mbinu ya uingereza ikiwemo reli na meli pia mawasiliano yaliboreshwa kama simu, telegraph hata picha pia
Kiukweli amefanya mambo mengi