Membe kuwania urais 2015...

acha kurusha mate
leta hoja hapa.
Otis

na wewe hoja gani uliyoleta kuhusu huyo membe? Membe kawafanyia nini watanzania mpaka sasa pamoja na kuwa hapo kwa muda mrefu? Usitake kutuhadaha sisi watanzania na vicheko vya ki-unafiiki anavyofanya membe. Kwa ufupi, membe hana uwezo wa kuongoza nchi hii tena.
Kumbuka, kwasasa tz ni nchi ya tatu duniani kwa ombaomba, je unategemea membe ambaye uwezo wake wa kiutendaji ni mdogo kuliko jk tutakuwa wapi?
Kwasasa tunahitaji kiongozi anayejua maendeleo yanaletwa kwa vipaumbele zipi? Si kiongozi kila akipata nafasi ya kuongea anaanza kutuletea mifano ya miaka 50 iliyopita na mambo ya shule za kata kuwa nyingi. Kiongozi gani asiyejua vipaumbele vya kimaendeleo? Membe akagombee tu ubunge, na nina wasiwasi hata akipatikana rais mwenye vision kama atapewa hata unaibu waziri.
 
Umetumwa wewe si bure maana uankurupuka na kuanza kumshambulia Membe (character assassination) . Mtu makini hukosoa huku akiwa na mbadala,, sasa wewe mbadala wako nani? EL?

Salimia,

Mtu makini husoma kwa ufasaha, hutafakari kwa kina na hupima maneno yake kabla ya kuyaweka hadharani.

Nimeanza hoja yangu kwa kuweka bayana kuwa No.2 kati ya wasionishawishi......ungesoma kwa umakini ungeniuliza No.1 ni nani? Ukiniuliza nikakujibu ni EL, nikikuuliza nami sasa basi nani kanituma utajibu nini?! Umekurupuka!

Mbadala ni upi? Ungekuwa makini ungebaini kuwa nahitaji kushawishiwa kwa hoja za upande wa pili ili nipime kama zinatosheleza kunifanya nimuunge mkono au nitafute mbadala. Ila kwa kuwa wengi mmezoea kulaghai, kushawishi hamjui! Umekurupuka!

Character assassination? Mh. Membe hajatoa msimamo wake na serikali juu ya OIC na Kadhi? Hajakutana na Mha. Pengo baada ya upepo kuvulugika? Mh. Membe hajaomboleza msiba wa shujaa Gadaff? Umekurupuka!

Salimia kajipange uje kunishawishi kwa hoja.
 
Anxiously waiting for Mbopo. Huyu memba napenda approach yake isiyo na jazba katika kumtetea Mh. Membe kwa hoja. Atakuja tu.......!
 
na wewe hoja gani uliyoleta kuhusu huyo membe? Membe kawafanyia nini watanzania mpaka sasa pamoja na kuwa hapo kwa muda mrefu? Usitake kutuhadaha sisi watanzania na vicheko vya ki-unafiiki anavyofanya membe. Kwa ufupi, membe hana uwezo wa kuongoza nchi hii tena.
Kumbuka, kwasasa tz ni nchi ya tatu duniani kwa ombaomba, je unategemea membe ambaye uwezo wake wa kiutendaji ni mdogo kuliko jk tutakuwa wapi?
Kwasasa tunahitaji kiongozi anayejua maendeleo yanaletwa kwa vipaumbele zipi? Si kiongozi kila akipata nafasi ya kuongea anaanza kutuletea mifano ya miaka 50 iliyopita na mambo ya shule za kata kuwa nyingi. Kiongozi gani asiyejua vipaumbele vya kimaendeleo? Membe akagombee tu ubunge, na nina wasiwasi hata akipatikana rais mwenye vision kama atapewa hata unaibu waziri.


Ngoja nianze na swali moja moja kwani inaonesha uwezo wako ni mdogo sana.
Niambie watumia vigezo gani kusema Membe ana uwezo mdogo kuliko JK
OTIS
 
Tanzania hii hakuna kiongozi hata mmoja wa CCM anafaa kuwa Rais wote ni mbwiga tu.

wanaweza kuwepo lakini mfumo mzima hauwapi nafasi hata chembe ya kuyatekeleza wanayoyaamini kwa mustakhabali wa watu wa Tanganyika. Kabla hawajaubadili mfumo, mfumo unawabadili wao!
 
Membe phew!!!!!!!!!!!!!!!!! Membe too low jamani kha!!!!!! me nashangaaa sana hata Six anzunguka kote kuna watu vijana tuwaunga mkono eti membe rais ,then Nyalandu prime minister phew!!!!!!!!!! yaani upuuzi mtupu kabisa kiukweli Membe hafai kabisaaaaaaaaa??????? na huyo Nyalandu ndio kabisa ambao sita anawapigia debe eti waadilifu kha,Kama Nyalandu alikuwa mwenyekiti wa bodi ya org moja (kapuni) analala na wanawake hoteli kubwa kubwa anawaambia wapeleke invoice kwenye org hiyo ambayo mwisho wa siku ilikufa kwa sababu ya ufisadi wake halafu watu wanasimama (sita) eti kuna vijana waadilifu wanafaa jamani kwa tunaowajua hao watu ni upuuzi mtupu na ndio hapo ni proove hata uelewa wa huyo sita ni mdogo sana na uliojaa chuki sioni uadilifu wa huyo Membe wala huyo Nyalandu anaozunguka kuwanadi before ajawanadi awe nafuatilia vizuri waliko pita kwa sababu phew!!!!!!!! kwa kweli tunahitaji mtu muadilifu na mchpakazi but not Membe
 
Tetesi....


nasikia membe hata familia yake haijui tanzania inafananaje! nasikia ni raia wa canada kama sijakosea... kama nimekosea nisahihisheni ila nilisikia dr exaveri lwaitama akisema, kama ni kweli je uyu ambae hata familia yake ina uraia wa canada atafaa kweli kuwa raisi au ndo tutauzwa kabisa! unaruhusiwa kunikosoa kama nimekosea.

kiukweli mimi ni ccm damu ila jamaa simkubali hata chembe, kwa kipindi alichokuwa waziri wa mambo ya nje sijaona jitiada hata ya kuomba tupunguziwe deni la taifa! yapo mengi ila hajanishawishi kwa upande wangu, bora hata mkapa agombee tena roho yangu itatulia.
 
Jaman rais wa nchi si Mungu. Na siasa ina kanuni ya biashara. Ushindani ndo sera yenyewe, hapa nchi 2nababaishwa sana na Tanesco kwa kuwa hawana washindani. Chukulia mfano kipindi kile TTCL ndo ilikuwa kampun pekee ya mawasiliano! Mambo yalikuwa ovyo na hayavutii atleast wakaja mobitel, celtel, vodacom, zantel, sasatel n.k hakuna asiyejua jinsi Tanzania sasa mawasiliano ni bwelele, siku watu wa South Africa wanatu beep tuliopo Tz. I mean kwamba tuache kufikilia habari za EL au Membe bali tujikite kuuimarisha upinzani usimame na uchukue awamu ndipo tuone tunaenda wapi? CCM ni wez, mafisadi, wasiojar wananchi na kila ubaya wao wanaona poa tu kwa kuwa hawajaona wenzao wanaongozaje the same nation. Nani kakuroga wewe Mtanzania mwenzangu mpaka hutaki kuelewa maana ya vyama vya upinzani? Please nakuomba tafakari na amua kuikomaza nchi yetu kisiasa. I mean it naumia sana hasa na utawala wa JK. Hivi unaogopa nini kuipa mwelekeo CHADEMA? CUF? PONA? NCCR? PPT n.k.
Binafsi nataka CHADEMA WAJARIBU KUONGOZA NDIPO IJE ITOKEE CCM Tena wakijipanga na kuwakosoa CHADEMA.
Ref. North AMERICA republican and democratic mambo si yale! Nani kakuroga wewe huitakii mema Tanzania?
 
Tetesi....


nasikia membe hata familia yake haijui tanzania inafananaje! nasikia ni raia wa canada kama sijakosea... kama nimekosea nisahihisheni ila nilisikia dr exaveri lwaitama akisema, kama ni kweli je uyu ambae hata familia yake ina uraia wa canada atafaa kweli kuwa raisi au ndo tutauzwa kabisa! unaruhusiwa kunikosoa kama nimekosea.

kiukweli mimi ni ccm damu ila jamaa simkubali hata chembe, kwa kipindi alichokuwa waziri wa mambo ya nje sijaona jitiada hata ya kuomba tupunguziwe deni la taifa! yapo mengi ila hajanishawishi kwa upande wangu, bora hata mkapa agombee tena roho yangu itatulia.

Ta Kamugisha,
Ilo lla familia ya Mh. Membe kuishi nje sina hakika nalo. Ila kwa ujumla familia ya mtumishi wa umma kuishi mbali na eneo analoongoza kuna athari kubwa kwa maendeleo ya anaowaongoza. Napanga tuje tulijadili hili kwa kina kwenye mada ya kutathmini "Mchango wa Mh. Sued Kagasheki toka achukue ubumge wa Bk mjini" Naye familia yake inaishi Uswizi kabla na hata baada ya kupata Ubunge.
 
Sioni sababu ya kujadili kwa kina nani anafaa kuja kuiongoza tanzania kama rais kutoka CCM, kifupi hakuna anayefaa kutoka CCM. Hii ni kulingana na mfumo mzima wa kifisadi&Kulindana wa chama hicho, hata kama Nyerere afufuke leo na kutaka kuongoza Tanzania kwa tiketi ya CCM bado hatatufaa. Jambo muhimu kwa sasa ni kujadili namna gani tunaweza kuiondoa CCM madarakani kuanzia ngazi ya vijiji,Vitongoji,Halmashauri,Bunge&urais.
 
Jamani naweza nisiwe na hoja ya kumtetea membe lakini jambo lililo wazi wala halihitaji matangazo ni kwamba Membe hahitaji kujisafsha makanisani kama alivyo Edward Lowassa. Hana kashfa ya ufisadi wala uwazili kama wengine na hasa kama bwana huyu wa Monduli.

La pili nimejaribu kufuatilia msimamo wa huyo Waziri. Katika swala la Pesa za radar, jambo moja ambalo niliona membe ana kigua kipana ni pale alipotamuka kwamba pesa lazima ziludi kuliko kuzileta kuwalipia helkopta ya chadema kwenye uchaguzi maana si munajua walitaka ziende kwenye NGO zinazofadhili chadema ili ziwasaidie.
 
Nakumbuka Mzee Mudhihiri M. Mudhihir aliwahi kumuita Mh, Membe eti ''NI NYOKA WA MDIMU'' Hali ndimu ila anavizia wanaotaka kuzichuma ili awagonge (awaume).

Am out
 
Maskini sasa wengime wanaochangia fanyeni utafiti wa kutosha. Tangia lini huyu Rwaitama amekuwa source wa taarifa za membe. Dr mwenyewe anataka kupata Uprofesa kwenye television ya Rowassa ile ya TBc.
 

Katika orodha ya wanaotajwa kuwania uteuzi wa ccm kwa nafasi ya urais wa JMT-2015, namba mbili (2) katika nisio shawishika nao ni Mh. Bernard Membe. Mh. Membe hanishawishi kuwa anastahili nafasi hiyo kwa sababu zifuatazo:


  1. 1. Historia halisi ya utendaji wake kama Mbunge na Waziri haina matokeo yanayosimama kumshuhudia Mh.Membe kama mtu wa kuleta mabadiliko chanya au maendeleo.

Asiyeweza katika dogo, ataweza katika makubwa? Mbele ya wapigakura wa Jimbo la Mtama, Mh. Membe anaonekana kama mtu aliyeshindwa kutimiza ahadi zake za muhula wa kwanza (2005-2010). Na walio wengi hawaoni umuhimu/mchango wa ukaribu wake na serikali katika kuwaletea mabadiliko. Ndo maana Mh. Membe alipata wakati mgumu sana kutoka kwa mgombea wa TLP, mtu ambaye hakuwa na jina, mali wala pesa bali support ya wananchi. Lakini kwa kutumia utaalamu aliojaaliwa, Mh. Membe aliweza “kumshughulikia” na kumdhibiti mpinzani huyu pekee na kuhakikisha wapiga kura wanakosa chaguo mbadala wakati wa uchaguzi. Ninashawishika kufikiri kuwa hata mpinzani mmoja angepenya na kusimama, matokeo ya Jimbo la Mtama yangekuwa sawa na ya Nyamagana.

Kuna jambo moja ambalo Mh. Membe ameshiriki na watu wasio na kumbukumbu nzuri au wafupi katika kuchambua mambo wanaweza kusema kalifanikisha. Ni suala la kurejeshwa kwa fedha za rada kupitia serikali badala ya NGOs kama wezi walivyotaka. Hii haiwezi kuhesabika kama jitihada ya Mh. Membe wala serikali ya Tanzania. Hili silielezi kwa ufasaha ili watu wajadili……………………..


  1. 2. Misingi ya mbinu anazotumia Mh. Membe katika kusaka kuungwa mkono na makundi yenye ushawishi mkubwa katika jamii haina maslahi kwa Taifa na inatengeneza viporo vya uporaji wa rasilimali za nchi na migogoro mikubwa ya kijamii hapo baadae.
Mathalani, katika suala la serikali kuanzisha na kuendesha Mahakama ya Kadhi na serikali ya JMT kujiunga na OIC, Mh. Membe akiwa mbele ya waandishi wa habari amekuwa akiwaondoa hofu wahusika kuwa haya mambo hayana shida na serikali iko katika hatua mbalimbali za kuyatekeleza. Mara tu upande wa pili wakianza kupaza sauti za kupinga, Mh. Membe hu-haha na hukimbia kimya kimya kwenda kwa viongozi wakuu wa upande wa pili “kutuliza mambo” kwa kificho. Katika hili, Mh. Membe anataka kuuma na kupuliza na ni ndumila kuwili. Ni vema, si kwa Mh. Membe tu, bali wanasiasa wote kuimarisha msingi wa msimamo ambao umekwishafikiwa na serikali katika suala hili nyeti.

Mh. Membe anasimama miongoni mwa viongozi wa Bara la Afrika waliosimama kidete kuomboleza kifo cha Shujaa wetu Mummar Gadaff. Lakini nyuma ya kilio na maombolezo ya msiba huu, kumefunikwa giza totoro la vitendawili juu ya nini haswa “majonzi” ya Mh. Membe? Wako wanaotoa nuru ili kutegua vitendawili kwa hadithi tofauti tofauti ambazo kwa ujumla wake ukizikusanya kwa ushambuzi makini unapata picha pana juu ya makubaliano/fadhila za utawala uliongushwa Libya kwa mgombea mtarajiwa. Watanzania tunapaswa kuwa tumejifunza madhara ya wagombea wetu kufadhiliwa na matajiri (nchi au mtu binafsi). Tutumie 2015 kuepuka kurudi chini ya utawala wa waliofadhili wagombea katika chaguzi kuu.

Mh. Membe anapigania uraia wa nchi mbili. Kwa faida ya nani? Binafsi sioni kama hili jambo lina tija kwa Taifa lenye uchumi unaomilikiwa na asilimia mbili (2%) ya wananchi wake na ndio asilimia tisini na nane (98%) ya hao hao tayari wana uraia wa nchi zaidi ya mbili. Hapa Mh. Membe hasimami kutetea rasilimali watu za Watanzania walioko nje bali kutafuta kuongeza wigo wa kuungwa mkono na watu wasiokuwa na uchungu wa nchi hii. Hawa tunaowaita “Watanzania wenye asilia ya Kihindi” ambao ndo wanashawishi sana suala hili tayari wanao uraia Uswizi, Canada, Marekani na hapa kwetu kutokana na udhaifu wa idara zetu za uhamiaji wanaishi na kufanya wanalotaka kwa jeuri ya pesa yao.

Nahitaji kushawishiwa kwa historia na utendaji upi Mh. Membe anastahili kuomba ridhaa ya kubeba bendera ya ccm katika uchaguzi mkuu 2015. Michango yenu ikiwemo matusi na dhihaka vinakaribishwa. Na kuwa na hakika, nitavipokea vyote kama vilivyo. Kwa namna ya pekee nausubiri mchango wa MBOPO, mtu ambaye mara nyingi hujitahidi kujibu hoja na si kujadili mtoa hoja katika kumtetea Mh. Membe.


Nawatakia Mwaka Mpya Mwema na Wenye Mafanikio.

Omutwale kutoka Kanyigo.

Omutwale,

Unanishangaza kidogo unapoanza kwa kusema kuwa Membe hajakuvutia na kukushawishi kuwa anafaa kuwa mgombea urais. Kwanza kabisa, hoja yako ingekuwa na mantiki ikiwa Membe angekuwa ametangaza nia na kuanza kushawishi wanachama wa CCM na wananchi kuwa anataka kuwa mgombea. Sasa unataka ushawishikaje na mtu ambaye si mgombea wala hajaanza kazi ya ushawishi? Pili, wewe ni nani haswa hadi ushawishiwe wa kwanza kwanza ikiwa anafaa au hafai kuwa mgombea? Isitoshe, mbona tunakuwa wapofu sana kutumia nguvu nyingi kujadili WATU badala ya kujadili MASUALA yanayoikabili taifa? Mgombea wa 2015 hawezi kujulikana sasa na mgombea yoyote makini hawezi kujitokeza sasa. Kati ya sasa na 2015 ni kipindi kirefu sana, uwanja wa kisiasa unaweza kubadilika sana na wote hao unaowataja kwa majina leo wakawa "irrelevant". Wengine wanaweza kuwa wagonjwa, wengine wakakumbwa na kashfa, wengine wakatupwa kwa umri na wengine wakatangulia mbele ya haki na wengine pengine wakakosa vigezo kutokana na matakwa ya Katiba mpya.
Umesahau kuwa hadi Julai, 2010 kabla ya kuingia Dr. Slaa kwenye ulingo hali ya kisisasa ilikuwa tofauti kabisa?

Mimi naamini kuwa mgombea anayefaa mwaka 2015 atatokana na mazingira na mahitaji ya wakati huo na matarajio na mahitaji ya watu ya wakati huo. Kwa sasa ni busara zaidi kujadili njozi zetu kwa taifa hili ni zipi? Mahitaji yetu ni yepi? Changamoto zetu ni zipi? Mambo yanayotuunganisha wote bila itikadi zetu ni yepi? Majawabu haya ndio yatatuambia mgombea anayetufaa ni yupi kati ya watakaokuwa wamejitokeza. Kujadili watu sasa kwa vigezo vya aina ya ulivyoviibua ni upofu!
 
Jambo lingine ambalo wanamtandao huu lazima wajue n kwamba sijawahi kumskia Membe kutangaza kugombea Urais. Ila watu ndo wanapenda huyu Membe awe rais nafikiri kwa sababu ya haiba yake na mvut kwa watu. Ninja mengi ya kuamini kwamba kiongozi huyo ni presidential material.

Kwanza ni mtu anayeweza kuweka na kutetea mipango yake. Mfano ametetea swala kurudisha change ya radar na imerudi lakini naskia hataishia hapo. Lengo ni kwamba lazima wote waliohusika na wizi huo wanachukuliwa hatua. Kama hiyo nisababu ya kumchukia basi endeleeni kumchukia.

La pili membe ni miongoni mwa mawaziri wachache ambao angalau wamejenga hata hospitali na shule katika majimbo yao. lowassa kaishia kujenga nyumba na kununua nyumba yeye na mwanaye huko London na Arusha kuchukua kila eneo na kujenga majumba.

Tatu huyo mswahili mudhihir alishindwa kwenya na kazi ya kijana huyo Bernard Membe maaana yeye alikuwa na ubnafsi lakin pia alitumwa na hao mafisadi lakini ameyapata aliyoyataka.

Membe habagui watanzania walio nje na wa ndani kama mnavyotaka. Yeye anaona ni watanzania wanaostahili kuheshimiwa na kuchangia katika maendeleo ya nchi yao. Ninyi mnataka wabaguliwe kwa sababu tu wameenda kuosha macho ulaya. Hii dhambi gani jamani.

Mwisho niishiye kusema kwamba membe hana record ya kujinyakulia mali wala kama wengine, hana uhusiano na wahindi wanaotichea kila kukicha na mikayaba ya umeme wala richmound. Inaskitisha kama mtu anaweza kutunga kwamba Membe ni raia wa Canada kwa sabBu tu alifanya kazi Canada ni suala lakuskitisha sana.
 
Membe mla rushwa mkubwa kala pesa za libya na genge la waarabu za kujenga kiwanda cha cement huko lindi!ushahidi ninao
 
Back
Top Bottom