MDAU: Simba sio mnyama wa kutisha, mnyama wa kutisha ni yule aliyemuua Samson

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,671
4,929
Mdau mmoja wa anasema watu wengi wanamwogopa Simba, na kusema ni mnyama hatari na wakuogofya, lakini la hasha Simba sio mnyama wa kutisha katika macho ya binadamu kwa sababu binadamu huyo huyo ameshawai kuua Simba mara kadhaa. Wengi mnakumbuka kisa cha Mwamba mwenye nguvu iliyepiga na kuua wafilisti wengi kwa mikono yake, jeshi la mtu mmoja lililogopwa na utawala mzima wa kifilisti, Mwamba aitwaye "Samson", jitu lenye nguvu mara dufu. Samson alipigana na Jeshi la wafilisti akaua wote, Samson huyo huyo alipigana na Dume la Simba lenye nguvu na akaliua na kulichana mdogo, yani kwa kifupi samson alipigana na vitu vingi vya kuogopwa ila akashinda. Lakini punde Samson huyo huyo alipoingia katikati mikono ya mwanamke ndio ukawa mwisho wake.

Ukikutana na mwanamke sahihi anaweza kukujenga kimaisha mpaka ukashangaa, na ukikutana na mwanamke ambaye sio sahihi anaweza kukuboa kimaisha mpaka ukashangaa. Mwanaume hodari yeyote udhaifu wake ni mwanamke, na ndio maana enzi za utumwa walikuwa wanahasiwa kama njia ya kuwapunguzia nguvu na kuwaongezea umakini.

View: https://www.instagram.com/reel/C6izmLNoWJu/?igsh=MTd2MGlkdHI2Y2I0bQ==
 
Aliangukiwa na kuta za Jumba la sherehe la Wafilisti.
 
Back
Top Bottom