Mdahalo wa kwanza: Obama ambwaga Seneta McCain

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
51,636
23,073
Mdahalo wa kwanza: Obama ambwaga Seneta McCain


*Azungumza na Majira Jumapili

OXFORD, Marekani

SIKU 40 kabla ya upigaji kura, mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Democrat, Bw. Barack Obama, amembwaga mpinzani wake, Bw. John McCain wa Republican katika mdahalo wa kwanza uliofanyika juzi usiku na kisha kuwasiliana na gazeti, mawasiliano ya kwanza na chombo cha habari hapa nchini.

Kwa mujibu wa kura mbalimbali za maoni ya watazamaji walioangalia mdahalo huo uliofanyika kwenye ukumbi wa kitivo cha Sanaa na Sanaa za Maonesho wa Chuo Kikuu cha Mississipi, sera za uchumi, makosa ya Bush yaliyosababisha kuanguka kwa uchumi wa Marekani na tabia ya McCain kumjadili Obama badala ya hoja, vimechangia kumpa ushindi.

Obama amekuwa akiongoza kwa asilimia 52 ya waliotazama mdahalo huo kumuona aliweza kujieleza vyema dhidi ya asilimia 38 za hasimu wake, McCain, kwa mujibu wa kura za shirika la habari la MSNBC.

Watazamaji waliohojiwa katika kura ya pamoja ya kituo kingine cha televisheni cha CBS na gazeti la New York Times, asilimia 47 walimpa ushindi Obama dhidi ya 42 za McCain miongoni mwa wasiokuwa wapigakura huku asilimia 48 ya ambao ni wapigakura wakimuunga mkono Obama dhidi ya 43 za McCain.

Saa chache baada ya kutoka kwenye mdahalo huo, Obama amelitumia gazeti hili ujumbe mzito kuhusu mdahalo huo.

Katika ujumbe huo kwa njia ya baruapepe kwa Mhariri wa gazeti hili Obama alisisitiza kuwa McCain hakuwa na jipya zaidi ya kuendelea kung'ang'ania sera alizoziita muflisi za Rais George Bush.

"Hassan, punde tu nimemaliza mdahalo na John McCain. Mamilioni ya Wamarekani wamepata fursa ya kutuona tukijadilia suala muhimu-mabadiliko ambayo tunataka kuyafanya," ilisema sehemu hiyo ya ujumbe kwa njia ya baruapepe.

Bw. Obama aliongeza:"Tuwe wazi, John McCain hana kipya zaidi ya sera zile zile muflisi za Bush-iwe katika masuala ya ndani au ya kimataifa na ambazo amekuwa akiziunga mkono kwa zaidi ya asilimia 90 ya muda wake akiwa kwenye Seneti."

Wagombea hao wanatarajiwa kupambana katika mijadala mingine miwili zaidi mwezi ujao kabla ya uchaguzi utakaofanyika Novemba 4, mwaka huu.

*Kwa undani zaidi wa kilichotokea kwenye mdahalo huo soma makala zaidi ukurasa wa 21 wa gazeti hili.
 
Back
Top Bottom