JamiiTalks MDAHALO (Sheria za Kimtandao): Maalum kwa Wanachuo wa Kitivo cha Sheria

Asha D Abinallah

Senior Member
Apr 5, 2015
140
904
Habari Wakuu,

Katika kutaka kuchangia ongezeko la Wataalam wengi katika Sheria na Kanuni za Mitandao ya Kijamii, JamiiForums ikishirikiana na Freedom House imeandaa mdahalo kuhusu nafasi ya Kimtandao (Cyberspace) nchini. Mdahalo huo utahusisha wanafunzi wa Shahada ya Sheria, wakisimamiwa na wanasheria wabobezi na wadau wa Mtandao nchini.

Mdahalo huu utahusisha utakaofanyika Jijini Dar es Salaam Tarehe 19/20 Julai ukkiwa na lengo la kujenga kizazi kipya cha wanasheria wenye uelewa na watakaobobea katika Sheria za Kimtandao.
=> Je, wewe ni mwanafunzi wa Shahada ya Sheria ukiwa mwaka wa 3 au 4? Unapendelea kushiriki mijadala kuhusu matumizi ya mtandao na Sheria zinazoyahusu? Basi unaweza Kushiriki.​

Jinsi ya kushiriki ni kwa kutuma barua pepe ya maombi kwenda programs@jamiiforums.com yenye kichwa "MAOMBI YA KUSHIRIKI MDAHALO" ikijumuisha:-

  1. Jina la mshiriki,
  2. Jina la chuo,
  3. Mwaka wa masomo,
  4. Namba ya simu,
  5. Akaunti zako za mitandao ya kijamii(facebook, instagram au twitter) na;
  6. MAELEZO MAFUPI ya nini maoni yako kuhusu nafasi ya kimtandao(Cyberspace) nchini Tanzania kwa sasa, kwa maneno yaziyozidi 250.

Mwisho wa kupokea maombi ni Jumatatu tarehe 16 Julai, 2018 saa 11 jioni.

Karibuni.

Kujua yaliyojiri soma >"NAFASI ZA MITANDAO YA KIJAMII NCHINI" - Yaliyojiri katika Mdahalo wa Wanachuo New Africa Hotel - JamiiForums
 
Mkuu Aleppo,

Elimu na ufahamu unahitajika zaidi kwa pande zote mbili. Tunapokuwa na Wanasheria wenye utambuzi, huku upande wa pili hautaki kujisogeza, inakuwa changamoto kubwa hata katika kuendesha, kuelewa na kutoa hukumu kwa mashtaka yanayohusiana na sheria na kanuni za Mitandao ya Kijamii.

Serikali ikianza kushindwa kuwahudumia watu wake inachofuata ni kuzima sauti za raia wake wasiseme kitu ila inshalaahh wanasheria wetu mkaseme pasipo kuogopa chochote au la sivyo ufe maskini ukiwa na imani ya kuwa Tanzania tajiri hewa
 
Safi.. Wazo zuri..

Naamini kuwashirikisha wasomi kwenye masuala muhimu kama haya kunaweza kuleta tija sana.

Nitafuatilia!
 
Habari Wakuu,

Katika kutaka kuchangia ongezeko la Wataalam wengi katika Sheria na Kanuni za Mitandao ya Kijamii, JamiiForums ikishirikiana na Freedom House imeandaa mdahalo kuhusu nafasi ya Kimtandao (Cyberspace) nchini. Mdahalo huo utahusisha wanafunzi wa Shahada ya Sheria, wakisimamiwa na wanasheria wabobezi na wadau wa Mtandao nchini.

Mdahalo huu utahusisha utakaofanyika Jijini Dar es Salaam Tarehe 19/20 Julai ukkiwa na lengo la kujenga kizazi kipya cha wanasheria wenye uelewa na watakaobobea katika Sheria za Kimtandao.

=> Je, wewe ni mwanafunzi wa Shahada ya Sheria ukiwa mwaka wa 3 au 4? Unapendelea kushiriki mijadala kuhusu matumizi ya mtandao na Sheria zinazoyahusu? Basi unaweza Kushiriki.​

Jinsi ya kushiriki ni kwa kutuma barua pepe ya maombi kwenda programs@jamiiforums.com yenye kichwa "MAOMBI YA KUSHIRIKI MDAHALO" ikijumuisha:-

  1. Jina la mshiriki,
  2. Jina la chuo,
  3. Mwaka wa masomo,
  4. Namba ya simu,
  5. Akaunti zako za mitandao ya kijamii(facebook, instagram au twitter) na;
  6. MAELEZO MAFUPI ya nini maoni yako kuhusu nafasi ya kimtandao(Cyberspace) nchini Tanzania kwa sasa, kwa maneno yaziyozidi 250.

Mwisho wa kupokea maombi ni Jumatatu tarehe 16 Julai, 2018 saa 11 jioni.

Karibuni.

Nimei share
 
Back
Top Bottom