JamiiTalks MDAHALO (Sheria za Kimtandao): Maalum kwa Wanachuo na Wahitimu wa Kitivo cha Sheria

Asha D Abinallah

Senior Member
Apr 5, 2015
140
904
Habari Wakuu,

Kutokana na wanafunzi wengi wa chuo kuwa katika kipindi cha mitihani, JamiiForums tumepokea maombi ya wanafunzi wengi kuomba kusogezwa muda mbele ili wote wenye nia ya kushiriki kufanya hivyo bila kuwa na kizuizi cha masomo. Muda wa mwisho wa kupokea maombi umeongezwa hadi Jumatatu Julai 23, 2018 na mdahalo kusogezwa hadi Julai 27, 2018.

==> Tafadhali rejea tangazo letu la awali <==

TARATIBU ZA WASHIRIKI

Katika kutaka kuchangia ongezeko la Wataalam wengi katika Sheria na Kanuni za Mitandao ya Kijamii, JamiiForums ikishirikiana na Freedom House imeandaa mdahalo kuhusu nafasi ya Kimtandao (Cyberspace) nchini. Mdahalo huo utahusisha wanafunzi wa Shahada ya Sheria, wakisimamiwa na wanasheria wabobezi na wadau wa Mtandao nchini.

Mdahalo huu utahusisha utakaofanyika Jijini Dar es Salaam Tarehe 27 Julai ukiwa na lengo la kujenga kizazi kipya cha wanasheria wenye uelewa na watakaobobea katika Sheria za Kimtandao.

=> Je, wewe ni mhitimu au mwanafunzi wa Shahada ya Sheria? Unapendelea kushiriki mijadala kuhusu matumizi ya mtandao na Sheria zinazoyahusu? Basi unaweza Kushiriki.

Jinsi ya kushiriki ni kwa kutuma barua pepe ya maombi kwenda programs@jamiiforums.com yenye kichwa "MAOMBI YA KUSHIRIKI MDAHALO" ikijumuisha:-
  1. Jina la mshiriki,
  2. Jina la chuo unachosoma/ulichosoma
  3. Mwaka wa masomo/mhitimu
  4. Namba ya simu,
  5. Akaunti zako za mitandao ya kijamii(facebook, instagram au twitter) na;
  6. MAELEZO MAFUPI ya nini maoni yako kuhusu nafasi ya kimtandao(Cyberspace) nchini Tanzania kwa sasa, kwa maneno yasiyozidi 250.
Mwisho wa kupokea maombi ni Jumatatu tarehe 23 Julai, 2018 saa 11 jioni.

Karibuni.
 
"...Sheria kandamizi.." naona mnalitafuta JIWE...

Ila wazo ni zuri na na itapendeza mkitulitea walau mrejesho, pia muwe makini maana kwenye hicho kikao wanaweza penyezwa wasiojulikana waje wawa spy...
 
Pale taaluma ya sheria inapopataga kichwa na kujiona eti wao ni waheshimiwa na bora kuliko sisi madaktari, engeneers, waalimu, wakunga nk.


Vitu vingine sio lazima vijadiliwe na wanasheria pekee kwani kila kitu kinaeleweka ni kuwa tu na nyenzo na pia wanasheria kutafsiri na wengine ktoa mawazo yao.

NB,
SIPO KUDHALILISHA TAALUMA BALI KUKUMBUSHA TU.
 
Back
Top Bottom