Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile wa Mbeya akagua simu za waumini hadharani akiwa madhahabuni

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
2,920
7,942
Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile jumapili iliyopita wakati wa ibada katika kanisa lake linalojulikana kama, 'Kikosi kazi cha injili', alimuita mmoja wa waumini wake kijana anayeitwa Eliya na kuamuru ampatie simu yake, ambapo aliikagua na kukuta meseji ya WhatsApp kutoka kwa binti.

Kisha akampigia huyo binti akiwa hapo hapo madhahabuni kwa simu ya Eliya, na mwisho alimtimua Eliya ibadani.

Tukumbuke kuwa huyu mchungaji ametoka gerezani hivi karibuni baada ya kushinda rufaa yake ambapo awali alikua amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kuendesha kanisa bila usajili.

Nimeambatanisha clip hapa chini.

Je, unazungumziaje, hii ni sawa Mchungaji kukagua simu za waumini wake tena hadharani?

Mimi naona ni unajisi wa wazi wa haki ya faragha kwa waumini wake, mbaya zaidi inakua kama udhalilishaji kwa kufanya haya hadharani.

Hii inasikitisha sana.

Hataki kutumia nguvu zake za bure. Kila siku anawaambia waache uzinzi lakini wanaenda kinyume; acha alale nao kiulalo... 😁
Hahahaha...!! Kwa hiyo kukagua simu zao ndo suluhisho?

Atakagua ngapi? Wanaweza amua pia kuwa na simu mbili, ya matukio na ya kuendea kanisani.

Pia, ikitokea mchungaji akatangulia mbele ya haki, kwa hiyo itakuaje means ndo watajiachia sasa...
 
Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile jumapili iliyopita wakati wa ibada katika kanisa lake linalojulikana kama, 'Kikosi kazi cha injili', alimuita mmoja wa waumini wake kijana anayeitwa Eliya na kuamuru ampatie simu yake, ambapo aliikagua na kukuta meseji ya WhatsApp kutoka kwa binti. Kisha akampigia huyo binti akiwa hapo hapo madhahabuni kwa simu ya Eliya, na mwisho alimtimua Eliya ibadani.
Tukumbuke kuwa huyu mchungaji ametoka gerezani hivi karibuni baada ya kushinda rufaa yake ambapo awali alikua amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kuendesha kanisa bila usajili.
Nimeambatanisha clip hapa chini.
Je, unazungumziaje, hii ni sawa Mchungaji kukagua simu za waumini wake tena hadharani?
Mimi naona ni unajisi wa wazi wa haki ya faragha kwa waumini wake, mbaya zaidi inakua kama udhalilishaji kwa kufanya haya hadharani.
Hii inasikitisha sana.
Yaani hiyo nimeipenda maana vijana wengi wakiwa kanisani wanakuwa watakatifu wakitoka kanisani wanakuwa watakafujo na mingine inaimba na kwaya hapo hapo madhabahuni yanapanga kwenda kukutana kwenye magheto yao ........ Yaani yamegeuza kanisa kuwa chumba Cha kutunzia Siri za uzinzi wao ... ....... Vijana tubadilike tuache matabia mabaya yasio. Faa mbele za MUNGU kwani mwana wa adamu yuaja kutwaa kanisa lake ambalo ndiyo watu wenyewe
 
Back
Top Bottom