Mbwa azikwa kwa heshima zote za serikali nchini India

CORAL

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
2,789
1,782
mbwa.jpg

Mbwa mmoja wa Polisi aitwaye Zanjeev amekuwa mbwa wa polisi nchini India kwa miaka mingi.

Amewasaidia polisi kutatua kesi nyingi za jinai ambazo bila yeye wangeshindwa kuwatia hatiani wahalifu.

Lakini tukio lililompa umaarufu mkubwa ni wakati magaidi toka Pakistan walipotega mabomu mjini Mumbai mwaka 2008. Bomu moja lililipuka na kuua watu 500.

Zanjeev aliwaongoza Polisi kwenye mabomu mengine polisi wafanikiwe kuyategua! Unaweza kuwazia ni watu wangapi waliokolewa ukizingatia kuwa bomu moja tu liliua watu wote hao!

Zanjeev alipozeeka akastaafishwa na sasa amekufa kutokana na uzee. Bila shaka alistahili mazishi ya heshima ikiwa ni pamoja na kufyatua risasi angani!

The Touching Story Of Indian Dog That Was Given A State Burial
 
Back
Top Bottom