Mbunge Ndaisaba Ruhoro Achangia Milioni 5 Ujenzi wa Kanisa Katoliki Rulenge - Ngara

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,033
974

MHE. RUHORO, MBUNGE WA JIMBO LA NGARA NA WANAJIMBO KATORIKI LA RULENGE - NGARA.

💒⛪🗓️12 MAY,2024.💒⛪

Mhe. NDAISABA GEORGE RUHORO, Mbunge wa Jimbo la Ngara, Sekreterieti CCM 'W' na M/kiti CCM 'W' Ndg VITARIS NDAILAGIJE amefanya ziara alimaarufu OPERESHENI JENGA KANISA katika Kanisa Katoliki kigango cha Rwishushi Parokia ya Rulenge, Kata ya Nyakisasa na kuchangia ujenzi wa kanisa Tsh. 1,000,000 taslimu na Tsh 500,000 Taslimu kwa kikundi cha michezo .

Halikadharika Mhe.Ruhoro amefanikiwa kufika Kata ya Bugarama na kukutana na waumini wa Vigango 14 vya kata ya Bugarama na Kibogora. Mbunge Jimbo la Ngara Mh. Ruhoro amepokelewa na Paroko wa Parokia hiyo FR HONORATUS NDARURA na viongozi wengine wa Kanisa, Chama na Serikali.

Mhe. Ruhoro amechangia fedha taslimu Tsh.5,500,000 na mchele mifuko 14 ya Kg 25 kama mchango wa ujenzi wa Kanisa la Parokia ya Rwinyana na madhehebu pia dini tofauti wameungana kushiriki harambee ya ujenzi wa Kanisa hilo kwa pamoja.

Mh.Ruhoro amewaomba waumini hao kuendelea kuungana Rais DR SAMIA SULUHU HASSAN katika kuleta maendeleo na kumpatia ushirikiano kwenye jambo la Mama la 2025 kwenye historia ya Tanzania ambapo Kwa mara ya kwanza tutamchagua Rais mwanamke kwa kura za kishindo.



WhatsApp Image 2024-05-13 at 14.36.47.jpeg


WhatsApp Image 2024-05-12 at 22.50.57.jpeg
 
Back
Top Bottom