Mbunge Eng. Ulenge: Maafisa Ugani Toeni Ushirikiano kwa Wakulima

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,030
974

MBUNGE ENG. ULENGE: MAAFISA UGANI TOENI USHIRIKIANO KWA WAKULIMA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga Mhe. Eng. Mwanaisha Ulenge amekabidhi Mbegu Bora za Kilimo kwa Wanawake wa Mkoa wa Tanga kupitia Halmashauri zote za Wilaya, Mbegu zenye Thamani ya zaidi ya Milioni 12.5 ikiwa na lengo la kuwainua Wanawake wa mkoa huo kiuchumi kupitia Kilimo.

Mhe. Ulenge amefanya zoezi la ugawaji wa Mbegu hizo Wilayani Korogwe Mkoani Tanga ambapo amewahimiza Maafisa Ugani kutoka Halmashauri zote za mkoa huo kuhakikisha wanasimamia na kutoa Ushirikiano ili kufanikisha utekelezaji wa upandaji wa mbegu hizo katika kuzalisha mazao kwa wingi na kuwainua Wanawake hao kiuchumi.

Mhe. Ulenge amesema Mbegu hizo zitasambwaza kwenye maeneo yote kulingana na Tafiti za Kitaalamu zilizofanyika ambapo kwa Mkoa wa Tanga kuna uwezekano wa kulima Alizeti kuliko maeneo mengine, ambapo kupitia kilimo cha Alizeti wataweza kuzalisha mafuta ya kupikia na kupunguza uhaba wa mafuta nchini ambapo pia ameweza kutoa Mbegu za Mahindi, Maharage, Nyanya, Mpunga, Mchicha, Ngano pamoja na nyanya Chungu.

Kwa upande wao wanawake wa mkoa wa Tanga waliohudhuria katika zoezi hilo wamemshukuru na Kumpongeza Mhe Mwanaisha Ulenge kwa kuweza kuwaheshimisha Wanawake wa mkoa huo katika kuwainua kiuchumi na kujiletea Maendeleo
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-04-08 at 09.00.48.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-08 at 09.00.48.jpeg
    946.2 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-04-08 at 09.00.48(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-08 at 09.00.48(1).jpeg
    1.2 MB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-04-08 at 09.00.49.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-08 at 09.00.49.jpeg
    1 MB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-04-08 at 09.01.31.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-08 at 09.01.31.jpeg
    956.6 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-04-08 at 09.05.22.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-08 at 09.05.22.jpeg
    323.7 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-04-08 at 09.05.23.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-08 at 09.05.23.jpeg
    406 KB · Views: 4
Back
Top Bottom