Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,988
- 960
Mbunge Dkt. Joseph Mhagama: Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu Kutumia Fedha za Ndani
“Kamati inapongeza jitihada za Serikali kuendelea kupanga bajeti ili kutekeleza miradi mingi zaidi kwa kutumia fedha za ndani. Kwa umahususi, Kamati inaipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya usimamizi mahiri, hodari na shupavu wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mara ya kwanza kutenga fedha za maandalizi ya uchaguzi Mkuu kwa kutumia fedha za ndani bila utegemezi wowote wa fedha za nje.”
“Hata hivyo, katika uchambuzi wake, Kamati imebaini kwamba, ipo haja ya Serikali kutenga fedha za ndani katika mradi wa Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi kwani hadi kufikia Februari 2024 mradi huo ulipokea asilimia 57.17 tu ya fedha za nje zilizoidhinishwa. “
Amesema Dkt. Joseph Mhagama, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati akitoa taarifa ya Kamati hiyo kuhusu Utekelezaji wa Bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu.