Mbinu za kubaini kama picha uliyoiona imewahi kutumika mahali kwingine

JamiiCheck

Member
Nov 3, 2023
54
44
NAMNA_YA_KUTAMBUA_KAMA_PICHA_IMEWAHI_KUTUMIKA_KATIKA_VYANZO_VINGINE.jpg


Kuna wakati upotoshaji huweza kutokea kwa kutumia picha ya zamani au picha isiyo mahali pake kuwaaminisha watu kuwa picha hiyo inahusiana na tukio au taarifa husika.

Watumiaji wa picha hii hukusudia kuibua taharuki au kutaka kukupa nguvu upotoshaji wao kuufanya uaminika kirahisi.

Zifuatazo ni baadhi ya mbinu za kubaini kama picha ya kwenye habari imeshawahi kutumika sehemu nyingine:

1. Kutumia Google Image Search
  • Ingia kwenye browser na andika "Google Image Search."
  • Apload au paste picha unayotaka kuchunguza.
  • Ruhusu Google kuitafuta na angalia matokeo kama picha hiyo inapatikana kwenye vyanzo vingine.
2. TinEye
  • Nenda kwenye tovuti ya TinyEye.
  • Apload au paste URL ya picha unayotaka kuchunguza.
  • TinyEye itatafuta picha hiyo au zinazofanana na kuonyesha matokeo.
3. Kurejelea Metadata ya Picha
Metadata ni programu au mfumo unaosaidia kutoa maelezo yanayohusiana na data ya picha, kama vile tarehe ya picha ilipochukuliwa, eneo, na vigezo vingine vya kiufundi.

Unaweza kutumia programu hii ukapata maelezo kama tarehe na eneo zinaweza kutoa mwanga kama picha inaweza kuwa ya zamani au imebadilishwa.

4. Kulinganisha Picha (Photoshop)
Zana kama Photoshop zinaweza kutumika kulinganisha picha kwa kuchanganua maeneo na vipengele muhimu. App hii inakusaidia kukueleza chanzo cha picha hiyo, ikionesha pia endapo imewahi haririwa na kutengenezawa.

Hivyo, unaweza linganisha picha ya asili na ile inayodaiwa kuwa ina uhusiano na tukio au eneo. Tafuta tofauti au marekebisho ambayo yanaweza kubainisha kama picha imebadilishwa au kufanyiwa mabadiliko.

Kuleta picha yako katika Jukwaa la JamiiCheck
JamiiCheck ni Moja kati ya Majukwaa yanayopatikana ndani ya tovuti ya JamiiForums.com. Jukwaa hili limewekwa mahsusi kwa ajili ya kufanya uhakiki, kutafuta uthibitisho au uhalisia wa habari, taarifa, matukio, picha au video mbalimbali zinazojitokeza au kuibuka kutoka katika vyanzo mbalimbali ndani na nje ya mtandao.

Ikiwa utapata ugumu kupata chanzo cha picha usipate mashaka, wasilisha picha unayotamani ichunguzwe katika Jukwaa la JamiiCheck ambapo utasaidiwa kutafutiwa chanzo cha picha na kupewa ufafanuzi wa kina.

Zaidi, tembelea Jukwaa la JamiiCheck kwa kubofya HAPA.
 
Back
Top Bottom