Mbeya: Idadi ya Maofisa waliotiwa Nguvuni na TAKUKURU Kwa Kutafuna Bilioni 1 Kwa Posi bandia Wafikia 26.Msako na Uchunguzi Unaendelea.

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
44,457
51,280
Sakata la Maofisa wa Serikali waliojitengenezea mfumo bandia wa Makusanyo ya Fedha za Umma limezidi kushika Kasi na kuchukua sura Mpya.

Awali TAKUKURU iliwatia mbaroni watuhimiwa 40 lakini baada ya Uchunguzi watuhimiwa 20 waliachiwa huru.

Lakini baada ya Uchunguzi zaidi watuhimiwa 6 wametiwa mbaroni hivyo kufikisha watuhimiwa 26 ambao watapandishwa kizimbani kujibu mashtaka ya uhujumu uchumi na Kutafuna zaidi ya Bilioni 1 za makusanyo ya ndani kutoka Halmashauri 10 za Pangani,Mbeya Jiji,Tunduma, Sumbawanga,Mbarali,Makete,Rungwe,Ileje,Busokelo na Mbeya DC.

View: https://youtu.be/B7Mc-AD02hM?si=WAKQzIu9YMSoCAZl

My Take
Hawa wezi Walipishwe na wafungwe Ili iwe fundisho Kwa wesi wengine wa Mali ya Umma.
Screenshot_20240503-044027.jpg
 
Katika Sheria za jinai nchini, Sheria za Uhujumu uchumi ni legevu sana.

Mshitakiwa akipatikana na hatia, sheria inampa chaguo ama kifungo au kulipa faini ambayo mara nyingi huwa ndogo kuliko hasara aliyohukumiwa kusababisha.

Iwapo mtuhumiwa ana hela za kutosha na kazificha kibabe, basi analipa faini na kuachiwa huru.

Katika falsafa ya sheria, tunasema kuna sheria zimetungwa kwa ajili ya kupendelea watu fulani.

Mfano linganisha sheria ya Kanuni ya Adhabu ambapo mwizi anafungwa miaka 3,5 hadi 20 bila chaguo la faini, na Sheria ya Uhujumu Uchumi ambapo mtu anaambiwa aende jela miaka 5 au alipe faini ya milioni 5.

Kimbembe kinakuja pale ambapo masikini anatenda kosa la uhujumu uchumi; unakuta mfano, anahukumiwa aende jela miaka 20 au alipe milioni 20 kwa kosa labda la kupatikana na nyama ya digidigi. Fine inakuwa parefu, na kifungo nacho kirefu, basi anakuwa hana namna zaidi ya kusota jela.
 
Mshitakiwa akipatikana na hatia, sheria inampa chaguo ama kifungo au kulipa faini amabyo mara nyingi huwa ndogo kuliko hasara aliyohukumiwa kusababisha.

Iwapo mtuhumiwa ana hela za kutosha na kazificha kibabe, basi analipa faini na kuachiwa huru.

Katika falsafa ya sheria, tunasema kuna sheria zimetungwa kwa ajili ya kupendelea watu fulani.

Mfano linganisha sheria ya Kanuni ya Adhabu ambapo mwizi anafungwa miaka 3,5 hadi 20 bila chaguo la faini, na Sheria ya Uhujumu Uchumi ambapo mtu anaambiwa aende jela miaka 5 au alipe faini ya milioni 5.

Kimbembe kinakuja pale ambapo masikini anatenda kosa la uhujumu uchumi; unakuta mfano, anahukumiwa aende jela miaka 20 au alipe milioni 20 kwa kosa labda la kupatikana na nyama ya digidigi. Fine inakuwa parefu, na kifingo nacho kirefu, basi anakuwa hana namna zaidi ya kusota jela.
Sasa kwa nini Huwa wanawanyima dhamana wakati kumbe wanapewa uhiari?

Hii ni namna ya kulinda wezi ambao Huwa ni maofisa wakubwa wa Serikali
 
Kunyimwa dhamana kuna sababu nyingi, na sababu kubwa katika kesi za uhujumu uchumi ni kumlinda mtuhumiwa asije akadhirika na wale ambao pengine wamefaidika na wizi na wana hofu ya kujumuishwa.

Sababu nyingine ni kuepusha uchakachuaji wa ushahidi lakini pia kuepusha watuhumiwa kuendeleza uhujumu.
 
Katika Sheria za jinai nchini, Sheria za Uhujumu uchumi ni legevu sana.

Mshitakiwa akipatikana na hatia, sheria inampa chaguo ama kifungo au kulipa faini ambayo mara nyingi huwa ndogo kuliko hasara aliyohukumiwa kusababisha.

Iwapo mtuhumiwa ana hela za kutosha na kazificha kibabe, basi analipa faini na kuachiwa huru.

Katika falsafa ya sheria, tunasema kuna sheria zimetungwa kwa ajili ya kupendelea watu fulani.

Mfano linganisha sheria ya Kanuni ya Adhabu ambapo mwizi anafungwa miaka 3,5 hadi 20 bila chaguo la faini, na Sheria ya Uhujumu Uchumi ambapo mtu anaambiwa aende jela miaka 5 au alipe faini ya milioni 5.

Kimbembe kinakuja pale ambapo masikini anatenda kosa la uhujumu uchumi; unakuta mfano, anahukumiwa aende jela miaka 20 au alipe milioni 20 kwa kosa labda la kupatikana na nyama ya digidigi. Fine inakuwa parefu, na kifungo nacho kirefu, basi anakuwa hana namna zaidi ya kusota jela.
Kwa nini sheria zisifanyiwe marekebisho?
 
Sakata la Maofisa wa Serikali waliojitengenezea mfumo bandia wa Makusanyo ya Fedha za Umma limezidi kushika Kasi na kuchukua sura Mpya.

Awali TAKUKURU iliwatia mbaroni watuhimiwa 40 lakini baada ya Uchunguzi watuhimiwa 20 waliachiwa huru.

Lakini baada ya Uchunguzi zaidi watuhimiwa 6 wametiwa mbaroni hivyo kufikisha watuhimiwa 26 ambao watapandishwa kizimbani kujibu mashtaka ya uhujumu uchumi na Kutafuna zaidi ya Bilioni 1 za makusanyo ya ndani kutoka Halmashauri 10 za Pangani,Mbeya Jiji,Tunduma, Sumbawanga,Mbarali,Makete,Rungwe,Ileje,Busokelo na Mbeya DC.

View: https://youtu.be/B7Mc-AD02hM?si=WAKQzIu9YMSoCAZl

My Take
Hawa wezi Walipishwe na wafungwe Ili iwe fundisho Kwa wesi wengine wa Mali ya Umma.
View attachment 2979848

Nduguuu sabayaa yukoo nje na haooo maigizooo watatokaa kama wengine
 
Back
Top Bottom