Maziwa kumi maarufu duniani yenye maji ya rangi ya waridi{Pink lakes)

Bitoz

JF-Expert Member
Aug 27, 2015
30,823
126,539
Umewahi kwenda ziwani kisha ukakutana na maji yakiwa na rangi ya pink kama vile yamemwagiwa rangi ya Sadolin?
Najua wengi kwenu ni jambo geni hata kwangu pia nilipoona picha kwa mara ya keanza nilifikiri ni photoshop na fix tu za mtandataoni
Yapo ambayo maji yake yana rangi ya kudumu huku mengine yakiwa na rangi ya pink kwa msimu

............................................................ . .. ........
10/Champagne Pool
b7634f693e15f771d4e1d7c4c7938fa9.jpg
Screenshot_20180727-215916.jpg

linapatikana huko nchini New Zealand likiwa na kina cha mita 62
Ziwa hili hutoa maji ya rangi mbalimbali...sababu kuu ikiwa ni hewa ya kabonidayoksaidi inayopatikana kwenye kina cha chini kabisa ambayo huchanganyika na mwani na kutokea rangi ya waridi
Rangi ya waridi huonekana mara chache tu kwa mwaka
 
9/Laguna Colorada
b1b2cc64db0020fc004f48ca4ddcd975.jpg
IMG_20180727_220937.jpeg
IMG_20180727_221002.jpeg

Ziwa hili lina kina cha mita 81
Linapatikana huko nchini Bolivia
Sababu ya maji ya ziwa hili kuwa na rangi ya waridi ni kutokana na kuwepo madini mekundu ambayo hujichanganya na mwani
Hivyo mchanganyiko huu hubadilika maji kutoka rangi nyekundu na kuwa waridi
 
Brother Bitoz unanondo nzuri za kutujuza ila jaribu kuaindika thread yako iwe moja au la ziwe mbili kuliko koment fupi fupi

Edit uzi hiyo sehemu ipo japo nimeona ukiwa unalalama hapana sehemu ya edit
But hongera kazi nzuri
 
8/Quiarading Pink Lake
bc0d088da273b235f3efe3b0c9a41abc.jpg
IMG_20180727_222801.jpeg
IMG_20180727_222834.jpeg

Ziwa hili dogo linapatikana huko Australia
Kwa kugundua kwamba linavutia watalii wameamua kupitisha barabara kati kati hivyo ntu unapita tu na gari lako na kujionea
Rangi ya waridi huweza kuonekana pande zote za barabara kwa mwaka mzima
Muonekano wake ni km kadimbwi tu lakini ni Ziwa
 
Brother Bitoz unanondo nzuri za kutujuza ila jaribu kuaindika thread yako iwe moja au la ziwe mbili kuliko koment fupi fupi

Edit uzi hiyo sehemu ipo japo nimeona ukiwa unalalama hapana sehemu ya edit
But hongera kazi nzuri
Shukrani mkuu
Hii ni kumi kubwa hivyo kupost moja moja ndiyo staili sahihi tofautisha na makala za Ze Bodi
Mnizoee tu mkuu
 
7/Masazir Lake
ecc983951a17939af28484190c5dd40f.jpg
IMG_20180727_224606.jpeg
Ziwa hili lina kina cha mita 1 tu yaani hata Le Mutuz anaweza kuogelea bila wasiwasi
Linapatikana huko nchini Azerbaijan
Sababu kuu ni uwepo wa chumvi kupita kiasi pamoja na madini ya sulphur
Shughuli kuu inayofanyika ni uchimbaji wa chumvi
 
6/Dusty Rose Lake
ff7a4853465671cff1a8b0280e1d432f.jpg
IMG_20180727_230201.jpeg
IMG_20180727_230216.jpeg

Linapatikana nchini Canada
Ziwa hili lina kina cha futi ksti ya 1 hadi 3
Halina maji chumvi wala mwani(algae) kipindi chote
Hadi sasa hakuna ajuaye sababu ya maji kuwa ya waridi
Kila mwaka watalii hufurika huko kujionea maajabu
 
5/Salina De Torrevieja
IMG_20180727_232019.jpeg
IMG_20180727_232046.jpeg
IMG_20180727_231940.jpeg

Ziwa hili la kuvutia linapatikana huko nchini Hispania jijini Valencia
Linapatikana kwenye uelekeo wa bahari ya Mediterrania
Lina kiwango kidogo tu cha chumvi
Ni miongoni mwa Ziwa la Waridi linalovitia zaidi duniani na Ulaya kwa ujumla
Watu wengi hupenda kutalii na kuogekea
 
4/Lake Spencer
IMG_20180727_234702.jpeg
IMG_20180727_234625.jpeg

Ziwa hili la maji chumvi linapatikana magharii mwa nchi ya Australia pia l
Maji yake yana mwani na ndiyo ubaosababisha maji kuwa ya rangi hii Pindi mchanga uliopo kandokando humulikwapo na miale ya jua kuonekana pia na rangi ya waridi
Limewahi kukaa miaks kumi bila kuonyesha rangi ya pink
 
3/Hurtt Lagoon
IMG_20180728_000712.jpeg

dd26678a8da885e2aa29260c3cd23116.jpg

Ziwa hili pia linapatikana kwenye pwani ya Magharibi ya Australia likiwa na kina cha futi 2 tu
Sababu kuu ya maji kuwa ya waridi ni kuwepo kwa chumvi na mwani
.Maji yake yanapata chumvi kutokea baharini
 
2/Lake Retba
IMG_20180728_001540.jpeg
60e48a5566e6e3df129180b625fe2333.jpg
f133d94bb104ebc301c852e95c35ce4e.jpg
IMG_20180728_001625.jpeg

Zuwa hili linapatikana huko Afrika ya Magharibi katika nchi ya Senegal likiwa na kina cha mita 3
Ni ziwa lenye kiwango kikubwa cha chumvi pengine kushinda hata maji ya bahari
Shughuli kuu ya kiuchumi ni uchimbaji wa chumvi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom