Mauaji ya kutisha na kuungama, ungekuwa ndo Padri ungefanyaje?

Prof Gamba

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
390
254
Padri amekaa katika ki-box cha kuungamisha, kanisani hakuna mtu. Mara muumini mmoja akaingia, akapiga magoti upande wa pili na kufanya ishara ya
msalaba akaanza kuungama.

"padri naungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana "
"endelea"

"bosi wangu aliniita nyumbani kwake akaniambia amegundua nimeiba shilingi
milioni 50, akasema nisipotoa maelezo ya kutosha atanipeleka polisi. Sasa
ukweli mimi naogopa kufungwa, nikatazama huku na huku nikagundua tuko
wawili peke yetu, nikachomoa bastola nikamuua. Yesu atanisamehe?"

"utasamehewa"

"Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa, kutazama loh,
mke wa bosi. Akaniuliza nimemfanya nini mume wake. Kutazama huku na huku
nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye. Yesu atanisamehe na
hiyo?"

"utasamehewa"

"nikatoka nje, nikawasha gari niondoke lakini mlinzi akakataa
kufungua
geti
akasema amesikia kama kishindo hivi!
Nikaona

ananiwekea

kiwingu.
Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Yesu
atanisamehe?"

"utasamehewa"

"nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja
kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi nikawaza mambo gani
tena.

Akasema
amerudi
nyumbani na kukuta

yaloyotokea, lakini akanionyesha diary ya baba
yake inayoonesha kuwa nilikuwa na appointment naye kabla hajafa.
Nikamuuliza nani mwingine anajua, akasema ameanzia kwangu kisha atakwenda
polisi. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua.
Diary
nikaichoma moto. Yesu atanisamehe na hilo ?"

-

kimya........

"padri, Yesu atanisamehe kwa hilo ?"

- kimya.........

Jamaa kutazama kwenye kibox padri hayupo. Lakini kwenye kona moja akaona

kabati la ngou za mapadri kama linatikisika. Kufungua akamuona padri
kajificha katikati ya
majoho
anatetemeka.

"sasa
baba mbona umenikimbia?"

padri kwa taabu akajibu

"nilitazama huku na huku nikagundua kuwa tuko wawili peke yetu........"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom