Marketplace for education purposes (Notes & Solved Past Papers)

Investaa

JF-Expert Member
Jul 3, 2015
795
658
Habari walimu!

Nimeona nitengeneze ajira kwa walimu wa secondary na chuo kikuu kwa kutengeneza APP ambayo mwalimu anaweza kuuza ebook (electronic book) kwa kutumia simu au laptop yake akiwa sehemu yoyote ndani ya Tanzania.

Nadhani hii itasaidia kupunguza unemployment rate kwenye upande wa elimu kwa kusubiri serikali itoe ajira.

Mwanzo nilifiriki nitoe ajira kwa walimu wa sayansi peke yake ila nikaa chini na kufikiria upya nikaona nitoa ajira kwa walimu wote wa ARTS, BUSINESS, SCIENCE kwa ngazi ya O-LEVEL , A-LEVEL NA CHUO.

Hapa mwalimu anajiajiri mwenyewe(self-employed) kwa kuuza notes za masomo yake anayoyaweza na kupakia kwenye APP na kulipwa kila mwezi kutokana na mauzo yake.

Na mauzo yote anaona kwenye akaunti yake atakayo kuwa anatumia kupakia vitabu kwenye app.

Mimi natoa platform ya walimu kujiajiri wenyewe kwa kutukia TEHAMA kwa kutengeneza notes na kusolve past papers kwa ngazi ya A-LELVEL & O-LEVEL.

Kwa upande wa chuo watakuwa anaandaa notes za topics mbalimbali kupitia course tofauti tofauti kama Dental, MD, Radiology, Pharmacy, Labs, Biomedical, Accounting, Marketing etc.

APP iko hatua za mwisho kumalizika na kuwekwa playstore, kwa mwalimu anayetaka kujiajiri mwenyewe kwa kuandaa notes na kusolve past papers na kuuza kwenye APP , atume namba PM mm nitaunga kwenye group la whatsapp tujadiliane namna ya kufanya hii biashara kwenye upande wa MALIPO.

Ata kama umeajiriwa unaweza ukatumia hii platform kwa PART TIME JOB , kukuongezea kipato kila mwezi; ukiwa vzuri zaidi kwenye masomo yako unaweza ukapata zaidi ya mshahara wako wa mwezi. Maana mshahara ni CONSTANT lakini mauzo yana vary kila mwezi kutokana na jitihada yako ya kuandaa notes na ku solve past paper nyingi.

Kuna format nitatoa kwa wale walimu ambao tutakubaliana kwenye swala la MALIPO. Format hii naamini itamsaidia mwanafunzi au mwalimu mvivu wa kuandaa notes kueleweza vizuri na kukufanya wewe uuze sana kila mwezi.

LENGO NI KUJIKWAMUA KWENYE DIMBWI LA UMASKIN KWA KUTUMIA TEHAMA...
 
Back
Top Bottom