MARA: Kinana asema chini ya CCM hii hakuna mwenye haki ya kukatisha uhai wa mtu mwingine

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
2,581
2,207

Na Mwandishi Wetu, Serengeti

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulurhaman Kinana amepokea malalamiko mbalimbali yakiwemo madai ya mauaji ya wananchi katika hifadhi ya Serengeti mkoani Mara.

Amesisitiza kuwa hakuna mwenye haki ya kukatisha uhai wa mtu mwingine.

Akizungumza leo Mugumu, Serengeti mkoani Mara, aliposhiriki kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Serengeti, Kinana ameeleza kuwa ipo kwa viongozi kuendelea kuwaelimisha wananchi kuheshimu mipaka iliyopo.

“Mkuu wa wilaya ya Serengeti amelifafanua vizuri sana na huwezi kuulaumu upande mmoja peke yake, lakini tunawajibu wa kuwaelimisha wananchi kuhusu kuheshimu mipaka lakini jambo moja la msingi hakuna mwenye haki ya kuondoa uhai wa mtu. Hata katika Katiba haki ya kwanza ni kuishi,” amesema.

Kinana ameelezea hayo baada ya baadhi ya wana CCM akiwemo Diwani wa Kata ya Machochwe Joseph Magete kudai kuwa kumekuwepo na matukio ya kutatanisha pembezoni mwa hifadhi hiyo kwa watu kupotea, hivyo alimuomba Makamu Mwenyekiti kuliangalia suala hilo kwa nini linatokea katika maeneo hayo.

Kwa mujibu wa Kinana, serikali hairuhusu kundolewa maisha ya mwananchi yeyote na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama wajibu wake ni kufuata sheria.

Hata hivyo, alisema katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo tayari serikali imeunda kamati ndogo ambayo itafika mkoani Mara kufanya tathimini na hatimaye kutatua changamoto hiyo.

== ==
 
Sewa Baba

Screenshot_2024-04-15-18-13-27-1.png
 
Kumbe Kuna ccm fulani iliyopita kulikua Kuna haki ya kupoteza uhai was mtu sio!!?

Hiyo ninkauli yake au umekosea heading!!?

Kama no ya kwake bas amekosea sana,huwezi kituhumu chama kwa mauaji!!
Mbona sioni tatizo hapo kwenye heading?

KINANA anamaanisha watu wote wanayo haki ya kuishi chini ya CCM
 
Wakati uhai wa akina Saanane unakatishwa mbona hakukemea?Au huwa kuna awamu ambazo kukatisha uhai wa Mtu mwingine unakuwa legalized???
 
View attachment 2964480
Na Mwandishi Wetu, Serengeti

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulurhaman Kinana amepokea malalamiko mbalimbali yakiwemo madai ya mauaji ya wananchi katika hifadhi ya Serengeti mkoani Mara.

Amesisitiza kuwa hakuna mwenye haki ya kukatisha uhai wa mtu mwingine.

Akizungumza leo Mugumu, Serengeti mkoani Mara, aliposhiriki kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Serengeti, Kinana ameeleza kuwa ipo kwa viongozi kuendelea kuwaelimisha wananchi kuheshimu mipaka iliyopo.

“Mkuu wa wilaya ya Serengeti amelifafanua vizuri sana na huwezi kuulaumu upande mmoja peke yake, lakini tunawajibu wa kuwaelimisha wananchi kuhusu kuheshimu mipaka lakini jambo moja la msingi hakuna mwenye haki ya kuondoa uhai wa mtu. Hata katika Katiba haki ya kwanza ni kuishi,” amesema.

Kinana ameelezea hayo baada ya baadhi ya wana CCM akiwemo Diwani wa Kata ya Machochwe Joseph Magete kudai kuwa kumekuwepo na matukio ya kutatanisha pembezoni mwa hifadhi hiyo kwa watu kupotea, hivyo alimuomba Makamu Mwenyekiti kuliangalia suala hilo kwa nini linatokea katika maeneo hayo.

Kwa mujibu wa Kinana, serikali hairuhusu kundolewa maisha ya mwananchi yeyote na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama wajibu wake ni kufuata sheria.

Hata hivyo, alisema katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo tayari serikali imeunda kamati ndogo ambayo itafika mkoani Mara kufanya tathimini na hatimaye kutatua changamoto hiyo.

== ==
Kinana anahekima sana
 
Back
Top Bottom